Watanzania tutaendelea kusubiri mpaka lini Bunge likitunga Sheria batili na kuuchomekea ubatili huo ndani ya Katiba yetu? Tufanye nini?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Kama kawaida yangu kila nipatapo fursa huja na makala zangu elimishi za Kwa Maslahi ya Taifa, ambazo zinachapishwa kwenye gazeti la Nipashe kila siku za Jumapili.

Leo naendelea na sehemu nyingine ya Ijue Katiba ya JMT kwa jicho la mtunga katiba. Sehemu ya kwanza nilifundisha katiba ni nini na katiba ni ya nani Ijue Katiba ya JMT Kwa Jicho la Mtunga Katiba: Watanzania Tusishabikie Uhaini!. Hukuna Uhaini wa Kauli na Maneno, Uhaini ni Mipango na Matendo!.
Sehemu ya pili nikazungumzia Mtunga katiba alimaanisha nini aliposema Katiba ni Sheria Mama Ijue Katiba kwa Jicho la Mtunga Katiba: Mtunga Katiba alimaanisha nini aliposema "Katiba ni Sheria Mama"? Ni kweli Katiba ni Sheria Mama? leo nazungumzia jinsi Bunge letu Tukufu, linavyotunga sheria batili zinakwenda kinyume cha katiba na nyingine sio tuu Bunge letu limetunga sheria batili, bali ubatili huo ukachomekewa (kiubatili) mpaka ndani ya katiba yetu ya JMT ya mwaka 1977 ndio maana hitaji la katiba mpya ni hitaji very bonafide genuine kwa Watanzania kuweza kusonga mbele kimaendeleo kwa kuwapata viongozi able people wenye uwezo, ability, capacity and capability ya kututoa hapa tulipo na kutufikisha kule tulipaswa kuwepo kama Singapore, Taiwan, Malaysia, Indonesia, ambazo tulipata nazo uhuru wakati mmoja, sisi tukiwa with everything wao wakiwa with nothing!, lakini angalia leo wenzetu walipo compared na sisi tulipo!, the magic is, the right people and the right strategies, hatua ya kwanza is to get the right people!.

Bandiko hili ni la swali

Watanzania tutaendelea kusubiria mpaka lini wakati Bunge letu Tukufu likitunga Sheria batili na sometimes kuuchomekea ubatili huo hadi ndani ya Katiba yetu na kuifanya katiba yetu kuwa na vipengele batili?. Je Watanzania tufanye nini?, au tunaweza kulifanya nini Bunge la aina hii?.​


Sii wengi wanafahamu Bunge letu Tukufu linaporidhia mkataba wowote wa kimataifa, mfano ile IGA ya ajabu ajabu ya DPW, maana yake hicho kilichoridhiwa kwenye huo mkataba ulioridhiwa na Bunge, kinakuwa ni sehemu ya sheria zetu za ndani, under local laws!. Ina maana Bunge ni linatunga sheria zetu za ndani kupitia miswada ya sheria inayoletwa bungeni na kupitishwa kuwa sheria, na Bunge linaporidhia mikataba ya kimataifa, maana yake ni Tanzania tume imports sheria hizo za nje na kuzi domesticate kuwa ni sheria za ndani, hivyo hivi tunapozungumza ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni sheria yetu halali!.

Kwa mujibu wa sheria yetu ya Rasilimali za Taifa, ile IGA ya DPW na Bandari zetu ni batili!, lakini kwa mujibu wa katiba yetu, mamlaka pekee ya kutangaza ubatili wa katiba au sheria yoyote ni Mahakama Kuu ya JMT. Mahakama Kuu imeibariki IGA ile licha ya mapungufu yote ya kisheria ya ile IGA.

Kuna upungufu mmoja mkubwa ambao hakutajwa sana, huu ni upungufu wa illegality. IGA ile ya DPW na Bandari zetu, ina illegalities mbili.
Ya kwanza ni illegality ya the capacity of Dubai to contract an international Treaty, kwasababu Dubai sio nchi, haina sovereignty hivyo haina the capacity to enter into an international Treaty with a nation kama Tanzania, mwenye uwezo huo ni UAE tuu na hakukuwa na POA (power of attorney) kutoka UAE kuiwezesha Dubai kuingia an international Treaty!.

Illegality ya pili, mkataba ule una kipengele kilicho kinyume cha sheria zetu, hivyo it's an illegal contract, lakini Bunge letu Tukufu limeipitisha hivyo hivyo.
Hii sii mara ya kwanza kwa Bunge letu kutufanyia mambo ya ajabu kama haya!.

Leo naomba niwaletee mifano Bunge letu Tukufu kutunga sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba ya JMT. Kwa kuonyesha Katiba inasema nini, hiyo sheria batili ikasema nini, na mwisho kuonyesha sheria batili hiyo, imekinzana wapi na katiba ya JMT.

Kama wewe sio mpenzi wa kusoma mambo marefu na huna interest na kujua vifungu vya katiba na sheria, unaweza ku skip sehemu hii, ukaibukia kule kwa Mchungaji Mtikila
Mchungaji Mtikila, licha ya kuwa ni mwanasiasa, Mwenyekiti wa chama cha siasa cha DP, (Democratic Party), lakini alikuwa ni mtu wa Mungu kiukweli kabisa, kwa sababu hakukubali kabisa katiba yetu inajisiwe!, hivyo akafungua kesi nyingine No. 10 ya mwaka 2009 kupinga marekebisho hayo ya 8 ya katiba na kuyaita ni ubatili!.

Kwa vile mimi ni Mtanzania na nawafahamu vizuri Watanzania walio wengi hawako deep kusoma makitu marefu, hivyo kwa wale wa short and clear mnaweza kuishia hapa and jump kwenye A way forward na conclusions, wale wa deep tuendeleeni

Katika kesi hiyo, Mchungaji Mtikila aliomba mambo mawili makuu
Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa kwa viongozi wa umma kuhama vyama na kupoteza uongozi wa umma.
  1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amirati Jeshi Mkuu, Samia Suluhu Hassan asiruhusu ule ujinga wa kuhama vyama unaosababisha hasara kwa taifa, kwa kuwashukuru kumuunga mkono na kuunga mkono juhudi zake, lakini wabaki huko huko kwenye vyama vyao, hadi 2025, wakiishamaliza muhula wao, ndipo wajitoe na kuhama vyama!.
  2. Ikulu ni mahali patakatifu, Rais wa Nchi, akiwa Ikulu yetu, atenganisha kofia zake mbili za rais wa nchi na Mwenyekiti wa chama cha CCM, rais wetu akiwa Ikulu yetu afanye kazi takatifu, asiendeshee vikao vya CCM, pale patakatifu petu, vikao vya CCM akavifanyie ofisi ya CCM Lumumba au kumbi za CCM Dodoma. Japo hakuna kosa lolote kuendeshea vikao vya CCM Ikulu yetu, lakini halileti picha nzuri kwa rais wetu, ambaye ni mpenda haki, kwa sababu yeye sio rais wa CCM ni rais wa Watanzania wote!.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe utaratibu wa proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, kwa rais tunaye VP, kwa mbunge au diwani, yule aliyemfuatia kwa kura katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama alipata zaidi ya 10% ya kura zote, kama hayupo aliyefikia asilimia hizo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  4. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya na nchi nyingine zenye kuheshimu demokrasia ya kweli na sio hii demokrasia fake ya vyama!.
  5. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
  6. Tuibadili Tume yetu ya Uchaguzi iwe Tume Huru zaidi na Shirikishi, tujenge uwanja sawa wa ushindani wa haki kwa vyama vyote, uchaguzi uendeshwe kwa transparency ya hali ya juu kwa kuruhusu mawakala hadi kwenye tallying, na vyama au taasisi zozote ziwe free kuwa na tallying centers zake, kitu ambacho hakitaruhusiwa na talling centers hizo ni kutangaza matokeo, kama matokeo yote ya uchaguzi hadi wa rais yanahesabiwa kituoni na kubandikwa ukutani, kama hakuna jambo lolote la kificho, yaani nothing to hide, kwanini uzuie independent tallying?!. Uchaguzi wa 2020, kila mwenye uwezo wa kufanya tallying aruhusiwe afanye ila sitangaze matokeo, hii itazuia bao la mkono!.
Hitimisho.
Mambo ya ajabu kulihusu Bunge letu ni mengi nineisha wahi kuyaulizia humu na miongoni mwake ni haya,
Japo maswali hayo kuhusu Bunge letu Tukufu hayajapatiwa majibu muafaka, madhali sasa tunaye mtu msikivu, tuendelee kuyauliza labda this time around, hatimaye yatapatiwa majibu muafaka!.

Watanzania tutaendelea kusubiria mpaka lini wakati Bunge letu Tukufu likitunga Sheria batili na sometimes kuuchomekea ubatili huo hadi ndani ya Katiba yetu na kuifanya katiba yetu kuwa na vipengele batili?. Je Watanzania tufanye nini?, au tunaweza kulifanya nini Bunge la aina hii?.​

Mhimili wa serikali unapotukosea tunaweza kuushitaki mahamani, lakini mhimili wa Bunge na mhimili wa Mahakama, niliwahi kuuliza humu, kiukweli in reality kwa mujibu wa katiba yetu, there is nothing anybody can do zaidi ya kumlilia Mama!.

Tanzania tumebarikiwa kumpata rais mpenda haki na mtenda haki, ni tumuombe tuu kutumia mamlaka yake as an executive president kubadili katiba na sheria ya uchaguzi kwa kutumia hati ya dharura, kwa jinsi ile ile ubatili huo ulivyochomekewa ndani ya katiba yetu, na afanye mabadiliko ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC kuifanya kuwa ni tume huru na Shirikishi na kuiwezesha NEC wasimamie chaguzi zote toka uchaguzi wa serikali za mitaa mpaka Uchaguzi Mkuu kwa kuajiri wasimamizi wa uchaguzi na sio huu mtindo wa sasa wa kuwatumia makada wa chama kimoja waliolamba uteuzi.

Mungu Ibariki Tanzania

Paskall
 
Mzee unatupeleka mbele, unaturudisha nyuma! Kuna wakati unakuja na hoja za Ki great thinker kama hizi! Kuna wakati unaunga mkono hata vile vitu visivyoeleweka!! Dah!! Yaani hata hueleweki eti!

All in all, nadhani ifikie wakati CCM ikubali kuwaachia wengine madaraka, ili tuone pia sura zao halisi. Na hii ni baada ya kukubali kuwepo na Tume huru ya uchaguzi, na pia Katiba yenye maslahi kwa Taifa! Na siyo maslahi kwa chama fulani cha siasa, au watu fulani wenye ushawishi.
 
Laiti ungekubali kukaa na rangi moja ya ngozi yako ungekua na nafas kubwa humu ya kutoa elimu! But umechagua kua na ngozi ya kinyonga na hapo ndipo tatizo linaanzia!! NB: Mkiambiwa suluhisho la haya yote ni katiba mpya na tume huru isiyokua nominated na Rais mnabeza na kusema katiba mpya itamsaidia nn bibi kule kijijin au itampelekea ugali mezani!!!
 
Wamekutoa kwenye pay roll nn mkuu, mbona kama umeanza kuwa na akili
 
Tangu lini watu wenye tabia za Zitto wakaaminika?, tangu uitwe na Magufuli kuwa Mayala maana yake ni njaa uligeuka chawa mkubwa tofauti na kipindi kile unajiita "Pasco".



Kila siku unatetea uuzwaji wa Tanganyika na WaTanganyika hivyo ni ngumu watu kukuamini kwa bandiko lako hili.
 
Ulizungumzia mpambano wa Mtikila mpaka mahakama ya rufaa, lakini marehemu Mtikila hakuishia hapo bali aliendelea kufungua kesi Hadi mahakama ya Africa na kushinda kesi ya mgombea binafsi lakini ilipokuja kusajiliwa mahakama kuu serikali ulikuja na utetezi kuwa Kuna mchakato wa katiba mpya na rasimu ya katiba ilipendekeza mgombea binafsi.
Lakini cha ajabu mahakama ilikubaliana na utetezi huo lakini cha ajabu katiba mpya haijapatikana Hadi leo Wala hakuna taasisi yoyote iliyoenda mahakamani na kuhoji juu ya Hilo swala.
Hata kituo cha Sheria za haki za binadamu kilichoungana na marehemu Mtikila hakikurudi kuhoji juu ya maamuzi ya serikali kuhusu mgombea binafsi.
Inaonekana huu mchakato uliisha na marehemu Mtikila.
 
Mkuu mimi nakuelewa sana. Lakini watanzania tunatatizo ha uoga, inawezekana ni malezi na shule tulizopitia ambazo mwanafunzi anatendewa kama mfungwa na kufundishwa kuiogopa mamlaka.

Katiba imeupa mhimili wa mahakama wajibu na mamlaka yote ya kutoa haki. Lakini kuna wakati mahakama hiyohiyo inapata kigugumizi kutimiza wajibu wake na kuja na visingizio vya kutotaka kuliingilia Bunge.

Hata tukiwa na katiba mpya, kama watu wanaendeshwa na hofu na wanashindwa kutimiza wajibu wao bado tutaendelea kuwa na sheria badili au sheria zinazopuuzwa na serikali.

Lengo kuu la lile sharti batili la kudhaminiwa na chama cha siasa ni hofu ya serikali kushindwa kuwadhibiti wabunge. Kwasasa wabunge wanafanya kile mwenyekiti wa chama chao ambaye pia ni mkuu wa serikali anakitaka.

Wakienda kinyume basi wanaweza kuvuliwa uanachama wao na kupoteza ubunge wao, wengi wao hawawezi kuwa na ujasiri wa kwenda kinyume na vyama vyao.

Laiti sharti hilo badili lisingekuwepo, basi wabunge hata baada ya kuvuliwa uanachama, wangeendelea kuwa wabunge. Hii maana yake ni kwamba serikali ingelazimika kuwaridhisha wabunge kuwa inafamya kazi yake inavyotakiwa na sio kinyume chake.

Kwa sasa, nchi yetu iko chini ya mfalme. Anadhibiti serikali, chama tawala pamoja na bunge. Mahakama inauhuru lakini majaji hawana ujasiri wa kuutumia uhuru huo kwenda kinyume na matakwa ya mfalme.
 
hayo ndiyo matokeo ya coup next mkitaka kufanya coup fikirieni consequences kwanza mnaweza kuwa na hali mbaya zaidi ya ile mnayoiondoa, coup zote huwa na reparations …
 
Ukiendelea kuwa muungwana kwa kuongea vitu vinavyoiponya Tanganyika kama hili bandiko la kizalendo, hakika tutakurudishia hadhi ya nyota 7 ambayo hapa katikati uliipoteza.
 
Sasa hivi akili zako zimerudi baada ya kukosa teuzi? Shenzi kabisa mnafiki mkubwa.ijiharibia mwenyewe pengine ili uanze upya nenda hukoupinzani ukaanze kupopoma
 
Hii hoja sio yako ni ya Mtikila wewe hauna uwezo huo wa kuchambua mambo haya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…