Watanzania tutamlinda, kumpigania na kumtetea Rais Samia kwa gharama yoyote ile

Mara moja moja uwe una wapost Mama na Baba yako wao ndio walio kulea na kukutunza, acha kutwa nzima kuabudu Binadamu mwenzako.
Mama aliyoyafanya Rais wetu Mpendwa yamegusa hadi maisha ya wazazi wangu ambao ni wakulima. Ambapo kila siku wanaendelea kumshukuru sana Rais Samia kwa uthubutu wake wa kutupatia mbolea wakulima
 
Mimi niondoe kwenye hiyo list
Halafu Mwashamba ni muongo.

Kuna siku alisema eti alibubujikwa na machozi huku amepiga magoti kwenye picha ya Samia.

Kumbe anadanganya, hakububujika machozi wala hakupiga magoti.

Hawa ndiyo machawa uchwara, wanamchekea usoni pembeni wanamsonya.
Unamwambia nani sasa.....
 
Ana vyombo vyake vya dola vinavyomlinda ambavyo kwa upande wa wananchi,vinawabambikia kesi za uongo, vinawapiga,kuwatesa na kuwapoteza pale wanapodai haki ktk nchi anayoiongoza.
 
Pigana mwenyewe na madunduka wenzako.
 
Mbona munajitafutia dhambi muda mwingine🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…