Wakuu,
jamii forums ni jukwaa la watanzania wote,ambapo ndani yake unapata kila kitu tena kwa ubora na weredi wa hali ya juu,ikiwemo,habari,burudani,michezo,mapishi,siasa,uchumi,lugha,nk
jamii forums faida zake ni nyingi sana,kama vile,ina'save' data/bando ukilinganisha na mitandao mingine ya kijamii, jamii forums inakupa wakati mzuri wa kuchangia hoja na mawazo au maoni kwa uwazi na uhuru zaidi tofauti na mitandao mingine.
vilevile jf inakukutanisha na watu wengi hasa viongozi wa nchi na watu mbalimbali maarufu wenye uelewa na maarifa makubwa yanayoihusu jamii ya watanzania na dunia kwa ujumla,ukilinganisha ya mitandao mingine kama tiktok facebook huwezi kukuta mwananchi wa kawaida anajadili jambo la msingi may be na waziri wa fedha.
watanzania wengi hawapendi kusoma/kujisomea ndio maana wengi hukimbilia tiktok,insta,X,fb nk, ili hali jukwaa hili la jf ni bora na linawafaa watanzania wote
ni mimi
holoholo.