Watanzania tutumie JamiiForums badala ya Facebook, TikTok, Instagram na mitandao mingine ya Kijamii

Nina zaidi ya miaka 10 humu, nitakuja kutoa ushuhuda jinsi JF imenifkisha pazuri
 
HUWEZI KUFANANISHA JF NA INSTAGRAM FB AU X, NI KUIVUNJIA HESHIMU HIYO MITANDAO MIKUBWA DUNIANI, JF BADO SANA HUKU NI KUPOST KWENYE MAJUKWAA HAMNA JIPYA
 
JF ni nzuri ila ina kosa vitu vingi sana ambavyo ndivyo hasa vinafanya watu wakimbilie kwingineko.

Mfano, JF hauwezi ku edit heading ya thread yako mwenyewe, mpaka uombe waku haririe!

JF hauwezi kufuta thread yako mwenyewe! Mpaka uombe kufutiwa!

Pia, kimuonekano, JF hauwezi ukalinganisha na kwingineko! JF na TalkKenya vimefanana kimuonekano, maana yake ma developer walinunua template kutoka kwa mtu mmoja!!
Walipaswa watengeneze muonekano wao unique tofauti na kwingineko ili kujitofautisha!

Pia, JF ina community ndogo!

Hivyo, kuvutia watumiaji wengi zaidi nadhani wamiliki wanapaswa wafanye jambo!!

Nimesema hayo si kwa ubaya, na binafsi naipenda JF, basi tu naipenda bila sababu!
 
Jf ni kitovu cha maadili tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…