Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

Paskali, wewe ni mtu mmoja unaendika mambo kwa lugha rahisi ila ukiwa very analytical, detailed na unampa msomaji ku-connect dots.

Paskali ungekuwa makanisani huenda ungeitwa nabii.

Maandiko yako yanaweza kudurusu kesho na kesho kutwa wakati hakuna hata dalili za unayoyasema kesho kutokea.

Yesu alisema kwa mtini jifunzeni, kuna haja ya kuwa na moment ya kujifunza mengi sana kwako Kaka Paskali.

Barikiwa sana comrade.
 
Ni wangapi wameishapokea hongo yao kama wewe na wangapi wanaendelea kusubiri hiyo hongo yao nao zamu yao ifike?

Mwandishi habari nae atalalia upande ule ule akiwinda uteuzi.

Polisi na wengineo mawazo ni hayo hayo.........

Je tutafika tukiendekeza nguvu tumbo au Tumbo Talks....
 
Wanabodi,

Swali linabaki, Jee Samia ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania, 2025 ....

Sasa kama mpangaji ni YEYE, na ndie amepanga 2025 ni yeye, then who are we to say no?.

2025 Twende na Mwanamke!.

Paskali
P
 
Najisikia very proud kuwa Msukuma, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wachapa kazi, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wenye roho nzuri, ndilo kabila linaloongoza kwa watu wenye upendo na kuongoza kupenda. Ndilo kabila linaloongoza kwa watu wema, wapole, wanyenyekevu, wastahimilivu, wenye heshima. Licha ya wewe kunitukana humu kila uchao, mimi sijawahi kukutukana, naendelea kukuheshimu and besides everything, I always love you.
Karibu mitaa hii, ushuhudie huyu Msukuma Pasco, asivyo kubali kuongozwa na Mwanamke!
P.
 
Ukiona mtu anajisifia elewa kuwa huyo ni fala tu. Umesahau sifa ya kupenda sifa kwa wasukuma. Umeidhihirisha.

Hujatukwanwa unaona umetukanwa. Ndivyo wasukuma mlivyo, hamjifichi.
 
Atakuparura shauri yako mami.
No, sisi wengine ngozi zetu zimekakamaa na kuwa ngumu kama gamba la kobe, ukimparua utaishia tuu kuumiza kucha zako.

Hivyo akina sisi wenye ngozi ngumu, tutamkuna vizuri pale anapostahili kukunwa vizuri, ila pia kama kumpara ni kumsaidia zaidi kuliko kumkuna, pia tutampara.
P
 

Ukweli uwezo wa kiuongozi hana wala msitumie tafsida mtaani wananchi hawataki hata kumsikia kila unapopita sio wanawake wala wanaume hakuna anaetaka kumsikia na umaarufu wake umeshuka kwa kiwango kikubwa yaani marehemu magufuli mtaani kwa wananchi ni maarufu kuliko Rais aliepo madarakani mwelezeni ukweli.
 
Huu ni uongo!.
P
 
P huogopi??
 
P huogopi??
“Baada ya vipindi viwili vya Rais Kikwete atakuja rais ambaye ni mweusi mchapa kazi lakini mchekeshaji sana, hata hivyo atatawaka kwa kipindi kifupi tu hapo ndipo Tanzania itapata rais mwanamke.” Sheikh Yahaya, mwaka 2006

Hata hivyo, naye huyo aliyepo ni siri ya Mungu pekee
 
Leo ndio siku yenyewe ya wanawake duniani, hongera sana kwa wanawake wote duniani wakiwemo wanawake hawa!.
P.
 
Kwamba Samia amuombe Mwinyi 2025 angombee Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mmejiridhisha na utendaji kazi wa Rais Hussein Mwinyi Zanzibar?
Kwenye kufanya miradi ya ujenzi ni mtu wa kukurupuka,
Visiwa anatuhumiwa kuviuza,
Hadi sasa kipi alichofanya kikubwa Zanzibari?
Wafanyakazi wa ofisi za umma rushwa zimewajaa amepambana kiasi gani na rushwa?
Mkurugenzi wa Zaeca alishindwa kumwajibisha ataweza kupambana na mafisadi wa bara?
Uzembe kwa wafanyakazi wa umma bado unatawala,
Husseni Mwinyi hatoshi kuwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…