Mkuu nchi yetu ya Tanzania ni Patrillineal, Mwanaume ni muamuzi namba moja katika nyanja zote/Top controller 😛H
Hapo mwanaume "kichwa cha nchi" inategemea ni jamii gani - patrilineal au matrilinear . Ukienda kwenye matrilineal societies, hicho "kichwa cha nchi hakionekani". Nimekaa kwenye matrilinear society miaka 8, angalau nina uzoefu huo. Mwanaume, mfano, among the Chewa ni 'ceremonial' hana mamlaka kwa watoto, hata kwa mkewe. Hata mtoto akitaka kuolewa au kuoa si yeye anayetoa idhini. Na pia anayeamua nani atoke nyumbani akaishi anakotaka (kati ya mwanaume na mwanamke) ni mwanamke, na si mwanaume. In fact, mwanamke ndiye anayemfulumusha mwanaume kwa kumwambia "Toka hapa nyumbani, rudi kwenu" au "katafute sehemu nyingine ya kuishi. Sikutaki." Sasa hapo kichwa cha nchi ni nani, anayefulumushwa (asiye na mamlaka) au anayebaki nyumbani (mwenye mamlaka)?