konda msafi
JF-Expert Member
- Sep 5, 2018
- 1,752
- 9,046
Hotuba ya mama imenikosha sana. Nina imani watu wengi imewafurahisha na wanamwombea asibadirike bali azidi kuboresha zaidi. Kila mtanzania mpenda maendeleo na uhuru wa kweli anataka kiongozi msikivu na anayejali sauti za watu. Tanzania ni yetu sote na wote tunastahili kufaidi mema ya nchi yetu na si kikundi cha watu wachache.
Wote hatuwezi kuwa makatibu wakuu wa wizara au wakurugenzi wa taasis za kiserikali bali kupitia sera nzuri za uwekezaji, sera zinazopromote biashara na ujasiriamali na sheria zisizokandamizi na za kinyonyaji tunaweza kufaidi keki ya nchi kupitia kona tofautitofauti. Huko nyuma au kwa wakati huu keki ya taifa inaliwa na kikundi cha watu wachache. Watanzania walio wengi wanajitahidi kupambana ili watoboe lakini mazingira sio wezeshi kuwafanya wafaidi keki ya taifa. Sheria na tozo mbalimbali kwa mfano za importation ni kikwazo kwa raia wa kawaida kufaidi keki ya taifa. Just imagine kodi na ushuru wa gari unazidi bei yenyewe ya gari. Lakini angalia maisha ya viongozi wetu, angalia maisha ya wanasiasa. Wote hatuwezi kuwa wanasiasa au wabunge ili tufaidi keki ya taifa. Kwa hiyo lazima serikali iweke mazingira wezeshi ili kila mtanzania kwa nafasi yake aweze kufaidi mema ya nchi.
Unaweza kuona maisha ya kifahari wanayoishi viongozi wa kiserikali yanayotokana na keki ya taifa. Ma-V8 kwa asilimia kubwa yanaendeshwa na viongozi wakuu wa serikali kama vile mawaziri na manaibu wao, wabunge, makatibu wakuu, wakurugenzi wa mashirika ya kiserikali, wakuu wa idara, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya just to mention the few lakini raia wa kawaida walio wengi hawaifaidi hii keki ya taifa.
Kwa sababu wote hatuwezi kuwa na vyeo vikubwa serikalini ni wakati sasa umefika watanzania tuamke. Kwanza lazima tuachane na utitiri wa vyama lukuki tunavyoviunga mkono. Tuwe na vyama viwili au vitatu tu vyenye nguvu ambavyo vitakuwa vinabadirishana madaraka inapotokea chama kilichopo madarakani hatukielewi au kinashindwa ku-serve interest za watanzania. Kuwa na vyama lukuki vya kisiasa tutachelewa kufika. Mojawapo ya interest ya watanzania ni watanzania wote kufaidi keki ya taifa. Watanzania kupitia sera wezeshi waweze kuendesha ma-V8, kuishi maisha ya kifahari kupitia biashara zitakazofanyika katika mzingira rafiki ya uwekezaji. Mbona nchi nyingine raia wake wanaishi maisha ya kifahari tu wala hata hawatamani kuwa wanasiasa ili kuwa na majumba ya kifahari na kuendesha magari ya kifahali. Sera nzuri za uwekezaji zinawafanya raia kutotamani hata kuingia kwenye siasa maana wana hela kuzidi hata hao wanasiasa.
Mama yetu ameanza vizuri sana. Natamani aniteue niwe mshauri wake ili asipige kona, aendelee na njia hii hii mpaka mwisho ili kila mtanzania aweze kufaidi keki ya taifa. Natamani siku moja kuiona Tanzania kila mkoa kuna suburbs za kutosha, raia wengi wakiendesha magari ya kifahari na kuishi kwenye makazi bora, huduma bora za afya, elimu bora, barabara nzuri na miundo mbinu bora kabisa, watu wenye furaha na wenye uhuru wa kutoa maoni yao kwa watawala bila hofu.