Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Ewe Mgalatia mwenye akili nani amekuloga? Mbona ulianza kwa roho sasa unamalizia kwa mwili?
Ndugu yangu Mayala umelogwa na nani?mbona umekuwa empty kiasi hiki?
Ni sisi wapinzani wenyewe tutaweza kujitetea, kwa sasa ccm wamepoteza ushawishi kwa umma, hivyo wamejishika na vyombo vya dola ili kuendelea kututawala kwa shuruti. Namna pekee ni sisi wapinzani kugoma kushirikiana na wanaccm.
Hakuna kushiriki msiba wala sherehe ama hafla yoyote ya mwanaccm, hakuna kununua chochote kwenye biashara ya mwanaccm, ama hata kupakia vyombo vyao vya usafiri labda iwe lazima sana. Tusiogope kuhamashana kwenye hili. Kwa vyovyote mbinu hii itamgusa kila mtanzania. Kwenye nyumba za ibada hakuna kutoa sadaka, na kuwaambia viongozi wa dini wanakalia kimya uovu. Mbinu hii haitatuacha na vilema wala kubambikiwa kesi, kutekwa ama kuuwawa. Mbinu hii ilitumiwa Zanzibar na ilifanya kazi.
Madai ya katiba mpya ni ya halali, kwanini wezi wa kura wasio na ushawishi waendelee kututesa na kutuumiza kwa madai yetu halali? Ni juu yetu wapinzani kujiokoa.