Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Ewe Mgalatia mwenye akili nani amekuloga? Mbona ulianza kwa roho sasa unamalizia kwa mwili?

Ndugu yangu Mayala umelogwa na nani?mbona umekuwa empty kiasi hiki?

Ni sisi wapinzani wenyewe tutaweza kujitetea, kwa sasa ccm wamepoteza ushawishi kwa umma, hivyo wamejishika na vyombo vya dola ili kuendelea kututawala kwa shuruti. Namna pekee ni sisi wapinzani kugoma kushirikiana na wanaccm.

Hakuna kushiriki msiba wala sherehe ama hafla yoyote ya mwanaccm, hakuna kununua chochote kwenye biashara ya mwanaccm, ama hata kupakia vyombo vyao vya usafiri labda iwe lazima sana. Tusiogope kuhamashana kwenye hili. Kwa vyovyote mbinu hii itamgusa kila mtanzania. Kwenye nyumba za ibada hakuna kutoa sadaka, na kuwaambia viongozi wa dini wanakalia kimya uovu. Mbinu hii haitatuacha na vilema wala kubambikiwa kesi, kutekwa ama kuuwawa. Mbinu hii ilitumiwa Zanzibar na ilifanya kazi.

Madai ya katiba mpya ni ya halali, kwanini wezi wa kura wasio na ushawishi waendelee kututesa na kutuumiza kwa madai yetu halali? Ni juu yetu wapinzani kujiokoa.
 
Mwambieni mama yenu mwendazake alikuwa anabebwa na Vatican yeye Hana pa kushikia ooh ooh alafu awkward kuwa na female dictator..walikuwepo female dictators 1)Indira Gandhi (2)Jiang Qing (3)Imelda Marcos (4)Elena Ceaușescu..kwa hiyo siyo kitu kipya Kama mtangulizi wako au mumeo dictator lazima utakuwa female dictator..
One wonders who will be the next Indira Gandhi,Jiang Qing,Imelda Marcos or Elena Ceaușescu????????????
 
Mh Rais ashauriwe kuepuka kutoa kauli tata zinazopelekea watu kuunganisha matukio&kauli zake.
Kauli za Rais zinatoa kiashiria cha;
1.Kuwapa go ahead wenye nia
ovu kufanya uovu,hata kama
hawajaagizwa.
2.Kuweka uhalali wa matukio kutokana na kauli za Rais.
Hata kama si maagizo yake.
KUMBUKA kauli za Hayati dhidi
ya Lissu,na tukio la Lissu
kushambuliwa.
Ni muhimu kama kiongozi achunge maneno.
Hata hivyo bado ana nafasi kubwa
ya kukitendea haki kiti chake.
 
Hizi akili za njaa ni tatizo sana kwa taifa hili.
Mzee kama wewe bado huishi kujikomba kupata ubwabwa.
 
CNN mambo ya Tanzania wao yanawahusu kitu gan??

Fake mainstream media hawawez kuingilia mambo yetu ya ndan,so chadema wanadhan hao CNN watawasaidia kitu gan
Mambo ya ndani ni uonevu dhidi ya wapinzani ?!. Sasa mbona mnawaachia hata bila kuwafungulia kesi ?! Mnasumbuliwa kasumba na ulimbukeni wa ki dictator na ukoloni . Hayo mambo yameshapitwa na wakati [emoji107]
 
Rubbish
 
Kwa hiyo ungekuwa ndio wewe mwandishi wa habari....je tukupigie makofi kwa kunukuu taarifa nyeti kutoka kwa NON-AUTHORITATIVE SOURCE?
Na Mayala ni mwandishi au mwanaharakati? Kama ni mwandishi ningejiridhisha kwa tabia na kutokuwa na upande hasa kwa kuwabeza wapinzani, watanzania wote tunajukumu la kulea vyama vyote vya siasa, viwe bora ili baadae vikiweza kuchukuwa madaraka, pia viweze kuendesha Nchi kwa jinsi tunavyotarajia!
 
Huu ni ukweli wenyewe. Mkuu umemaliza. Wateule wa hovyo na wasaka vyeo, kutumia mianya kupitia kauli za Rais kutenda maovu . Rais achunge kauli zake. (Chokochoko)
 
Huyo mdada wa CNN anaijua vizuri katiba ya nchi yako na hali ya demokrasia Africa kwa sababu Ni msomi mwenye masters ya Uandishi, anasoma, anafuatilia, anauliza vyanzo makini kama mwandishi makini na serious anayeipenda kazi yake.

Nyie endeleni kujaza waandishi uchwara, bongo movies na makanjanja wapiga makele kwenye media zenu ambao kazi yao ni kufukizia deal za matangazo na bahasha halafu mbaki mnalia haiwezekani na huo utopolo mwingine wa CIA.
 
Mateso ya Erick Kabendera na kifo cha mama yake vitakuandama mpaka mwisho.
 
Punguza kelele wamwachie...

Tumechoshwa na kelele zenu, mmekamata hamtosheki mnakuja kufungua fungua nyuzi kila baada ya sekunde kama mna uhalo mkavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…