Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Madai ya profesa Cheeseman kupitia CNN kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!, hayana ukweli wowote ule.
Huyo profesa ni mjinga mno....

Nchi ina vyombo vya ulinzi na usalama ,yeye alipata habari za ushahidi kutoka wapi kuwa amri hiyo imetoka kwa mh.Rais wetu?!!!

Si kila wanachokiongea kina ukweli....

Miaka yote UFARANSA na wasomi wao wa siasa za kimataifa walikataa kuwa HAWAKUHUSIKA na mauaji ya KIMBARI ya RWANDA mwaka 1994......

#MaslahiYaNchiNiMakubwaKulikoNafsiZetu
#KaziIendelee
 
Kumbe Brown:Ni mawazo yako hayo siwezi kiyapinga lakini tatizo lako unabebwa na uchama Yani una mahaba na CCM kiasi kwamba huoni ubaya wa serikali kuwaonea watu.Jifunze mshahara wa dhambi ni mauti,katika maisha yako penda kuona watu wote bila kujali Vyama vyao wanatendewa haki huo ndo utu.
Mkuu wangu.....

Kwa hiyo una ushahidi kuwa ni mh.Rais SSH aliyetoa amri ya kukamatwa mh.Mbowe?!!!

Hivi si mh.Rais aliyeshajiisha kumalizika kwa kesi ya mh.Mbowe na Mdude Nyagali na mwishowe wakarudishiwa fedha zao milioni 300?!!!

Kwa hiyo unaamini kabisa mh.Mbowe na wenzake pekee ndio wenye UZALENDO NA NIA YA DHATI YA TAIFA hili kuliko sisi sote na Serikali yote?!!!
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Kwa vile hii ni lugha ya watu, na pia naufahamu uwezo wa wengi wetu kwenye uelewa hizi lugha za watu, hivyo ili kuwasaidia wale wenzangu na mimi, sikiliza kwa makini jibu la swali la pili.
"it is a crackdown, she has launched or pretended to launch all along"

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali

Kuna hip-hop ilisema hizi ni propaganda

That is it!!

Hawana kitu
 
Huyo profesa ni mjinga mno....

Nchi ina vyombo vya ulinzi na usalama ,yeye alipata habari za ushahidi kutoka wapi kuwa amri hiyo imetoka kwa mh.Rais wetu?!!!

Si kila wanachokiongea kina ukweli....

Miaka yote UFARANSA na wasomi wao wa siasa za kimataifa walikataa kuwa HAWAKUHUSIKA na mauaji ya KIMBARI ya RWANDA mwaka 1994......

#MaslahiYaNchiNiMakubwaKulikoNafsiZetu
#KaziIendelee
Mimi naipa lawama kidogo serikali ya Tanzania kwa kuwa kimya yanapotokea masuala kama haya.

Yanapotokea masuala kama haya ndo wakati wa kutoa taarifa sahihi kwa media platforms zote wakiwemo nchi za kibalozi kuwataarifu jambo lilotokea.

Kwa kuwa Freeman Mbowe ni public figure pia waandishi wanapaswa kuihoji polisi na hata kuwaita katika runinga ili kupata ufafanuzi wa kinachoendelea.

Kwani pia Tanzania haina wachambuzi wa demokrasia si wapo hata kule Mlimani?

Nimeandika sana juu la hili (KUKAA KIMYA) kwa serikali kuanzia awamu ya tano na ya sasa.

Hili ni tatizo kubwa na linahitaji hatua za haraka ili kuweka uwiano katika kutoa habari sahihi.
 
Pamoja na kumwunga mkono Mh.Madam President kwa asilimia mia lakini ndugu yetu P.Mayalla inabidi aelemishwe.Kwanza hakuna TENA mabeberu katika dunia hii ya leo.Pili aidha hakusikiliza vizuri mahojiano ya CNN kuhusu kukamatwa kwa Mwenyekiti Mbowe au Lugha imempiga chenga.Katika yote yule professor hakumshutuma madam President Samia bali alizungumzia sana kuhusu utamaduni uliopo katika nchi za kusini mwa jangwa la sahara kwa vyama kama CCM kutopenda upinzani na kutumia neno Ugaidi ili dunia iwasapoti.siwezi kutafsiri yote ila nitamtafuta Mayalla na kumpa tafsiri sahihi ya aliyeuliza na aliyejibu.Jamani kama umekosa cheo bora unyamaze,ujishughulishe na mambo yako ya kupata rizki.Pole sana Mr Mayalla.Keep it up Madam President.Tupo nawe daima.
Anaaabisha Huyo mzee hata Kama anatafuta kula sio kwa spidi hii

Unatafuta kuwa recognized kwa kusifia udhalimu .

Sio fair wewe mzee.

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Basi njoo utueleze Mbowe Amekamatwa na nani?
Kwa kosa la kutaka kuwaua viongozi gani?
Na Lengo la kuwaua ni nini?
Alikuwa akishirikiana na nani ambao tayari wapo mashakani kama taarifa inavyoeleza?
Hiyo ni kazi ya MAHAKAMA....

Tujuacho ni kuwa anatuhumiwa tu....
 
Ni majuzi tu mlimwita kuwa Rais mwenye HURUMA baada ya Sabaya kutenguliwa na kupelekwa RUMANDE.....

Leo anakwenda Mbowe ,mh.Rais ni dikteta[emoji44][emoji1787][emoji1787]
Alifanya jema tutasema akifanya mabaya tutasema

Ni akili ya kipumbavu tu itayosifia hata mabaya.

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wangu.....

Kwa hiyo una ushahidi kuwa ni mh.Rais SSH aliyetoa amri ya kukamatwa mh.Mbowe?!!!

Hivi si mh.Rais aliyeshajiisha kumalizika kwa kesi ya mh.Mbowe na Mdude Nyagali na mwishowe wakarudishiwa fedha zao milioni 300?!!!

Kwa hiyo unaamini kabisa mh.Mbowe na wenzake pekee ndio wenye UZALENDO NA NIA YA DHATI YA TAIFA hili kuliko sisi sote na Serikali yote?!!!
Unaweza usiamini njia anayoipitia Mbowe na chama chake kudai katiba mpya ya wananchi wote. Lakini hupaswi kushabikia uonevu dhidi yake , hata kama uonevu huo hauna mkono wa Samia bali wateule wanaotafuta sifa , tena za kumharibia Mama.
 
Wanabodi,

Wiki iliyopita nilialikwa TBC kwenye kipindi cha Mizani, kinachoendeshwa na Dr. Ayoub Rioba. Mada kwenye kipindi hicho ni "Dhima ya Vyombo vya Habari Kulinda Maslahi ya Taifa".

Kwenye mjadala kuliibuka hoja jinsi Vyombo vya habari vya nje vinavyoibagaza Africa katika ripoti zake. Kwao kuibagaza Africa ndio maslahi kwao kwa mataifa yao.

Juzi Mwenyekiti wa Chadema, Mhe. Freeman Mbowe amekatwa na Polisi na tuhuma za kijinai.

CNN wameripoti hivi

Katika ripoti hiyo, kwanza CNN, hawakutafuta any authoritative source Kutoka nchini Tanzania, zaidi ya kuokoteza habari hiyo kama ilivyoripotiwa na media mbalimbali za ndani.

Kwa vile CNN ni chombo cha kibeberu, hivyo kina agenda ya kubagaza, CNN wakamtafuta Prof. Nic Cheeseman, ni Professor wa Democracy, University of Birmingham, kabla ya hapo, alikuwa Director wa African Studies Centre at Oxford University, ili kuichambua habari hiyo.

Prof. Huyo akatunga uongo wa wazi wa mchana kweupe kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!.

Huu sio uongo wa mchana kweupe?. Yaani hata kwa akili ya kawaida tuu, yaani Rais wetu Samia atoe amri ya Kukamatwa kwa Mbowe, kisa ni vuguvugu la mjadala wa katiba mpya na tozo za miamala?!, Watanzania tusijue, aliyemkamata Mbowe, amezungumza na sababu ametoa, CNN badala ya kutafuta the reliable sources, wanatuletea wazushi na kutuletea uzushi!. Ukisikia Ajenda hasi ndio hizi!.

Kwa vile hii ni lugha ya watu, na pia naufahamu uwezo wa wengi wetu kwenye uelewa hizi lugha za watu, hivyo ili kuwasaidia wale wenzangu na mimi, sikiliza kwa makini jibu la swali la pili.
"it is a crackdown, she has launched or pretended to launch all along"

Watanzania Wazalendo lazima tuwe makini sana na Vyombo hivi, unaweza kujikuta unasambaza taarifa ya kuibagaza nchi yako, rais wako na watu wako bila kujijua.

Uzalendo wa kweli ni kutanguliza mbele maslahi ya nchi yako, maslahi ya taifa lako, maslahi ya watu wako.

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
Walioagiza lissu apigwe risasi wako wapi?
 
Back
Top Bottom