Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Madai ya profesa Cheeseman kupitia CNN kuwa Freeman Mbowe, amekamatwa kwa amri ya rais Samia ili ku divert attention ya vuguvugu la katiba na tozo kwenye miamala ya simu!, hayana ukweli wowote ule.
Huyo profesa ni mjinga mno....

Nchi ina vyombo vya ulinzi na usalama ,yeye alipata habari za ushahidi kutoka wapi kuwa amri hiyo imetoka kwa mh.Rais wetu?!!!

Si kila wanachokiongea kina ukweli....

Miaka yote UFARANSA na wasomi wao wa siasa za kimataifa walikataa kuwa HAWAKUHUSIKA na mauaji ya KIMBARI ya RWANDA mwaka 1994......

#MaslahiYaNchiNiMakubwaKulikoNafsiZetu
#KaziIendelee
 
Mkuu wangu.....

Kwa hiyo una ushahidi kuwa ni mh.Rais SSH aliyetoa amri ya kukamatwa mh.Mbowe?!!!

Hivi si mh.Rais aliyeshajiisha kumalizika kwa kesi ya mh.Mbowe na Mdude Nyagali na mwishowe wakarudishiwa fedha zao milioni 300?!!!

Kwa hiyo unaamini kabisa mh.Mbowe na wenzake pekee ndio wenye UZALENDO NA NIA YA DHATI YA TAIFA hili kuliko sisi sote na Serikali yote?!!!
 
Kuna hip-hop ilisema hizi ni propaganda

That is it!!

Hawana kitu
 
Mimi naipa lawama kidogo serikali ya Tanzania kwa kuwa kimya yanapotokea masuala kama haya.

Yanapotokea masuala kama haya ndo wakati wa kutoa taarifa sahihi kwa media platforms zote wakiwemo nchi za kibalozi kuwataarifu jambo lilotokea.

Kwa kuwa Freeman Mbowe ni public figure pia waandishi wanapaswa kuihoji polisi na hata kuwaita katika runinga ili kupata ufafanuzi wa kinachoendelea.

Kwani pia Tanzania haina wachambuzi wa demokrasia si wapo hata kule Mlimani?

Nimeandika sana juu la hili (KUKAA KIMYA) kwa serikali kuanzia awamu ya tano na ya sasa.

Hili ni tatizo kubwa na linahitaji hatua za haraka ili kuweka uwiano katika kutoa habari sahihi.
 
Anaaabisha Huyo mzee hata Kama anatafuta kula sio kwa spidi hii

Unatafuta kuwa recognized kwa kusifia udhalimu .

Sio fair wewe mzee.



Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Basi njoo utueleze Mbowe Amekamatwa na nani?
Kwa kosa la kutaka kuwaua viongozi gani?
Na Lengo la kuwaua ni nini?
Alikuwa akishirikiana na nani ambao tayari wapo mashakani kama taarifa inavyoeleza?
Hiyo ni kazi ya MAHAKAMA....

Tujuacho ni kuwa anatuhumiwa tu....
 
Ni majuzi tu mlimwita kuwa Rais mwenye HURUMA baada ya Sabaya kutenguliwa na kupelekwa RUMANDE.....

Leo anakwenda Mbowe ,mh.Rais ni dikteta[emoji44][emoji1787][emoji1787]
Alifanya jema tutasema akifanya mabaya tutasema

Ni akili ya kipumbavu tu itayosifia hata mabaya.


Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Unaweza usiamini njia anayoipitia Mbowe na chama chake kudai katiba mpya ya wananchi wote. Lakini hupaswi kushabikia uonevu dhidi yake , hata kama uonevu huo hauna mkono wa Samia bali wateule wanaotafuta sifa , tena za kumharibia Mama.
 
Walioagiza lissu apigwe risasi wako wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…