Watanzania tuwe makini na vyombo vya habari vya Kibeberu. CNN wazusha kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni amri ya Rais Samia!

Mkuu umemaliza yote kabisa. Tatizo liko hapa
 
Taarifa ya Msemaji wa Polisi, David Misime imesema kuwa Mbowe hakukamatwa kwa tuhuma za kupanga na kuandaa kongamano la Katiba mpya jijini Mwanza bali alifahamu tuhuma zinazomkabili .

"Mbowe alikuwa anafahamu fika kuwa tuhuma zinazomkabili zilikuwa zinachunguzwa na wakati wowote angehitajika Polisi kwa hatua za kisheria mara tu uchunguzi wake utakapokamilika.

Hatua hiyo imefikiwa sasa,"
alisema Misime.

Hivyo, kilichoongelewa CNN na profesa Cheeseman ni maoni yake mwenyewe na angetumia maneno kama "nadhani" na "nahisi" serikali imeamua kumkata kutokana na hayo angeeleweka kuwa haenezi propaganda.

Kisha akaenda mbali zaidi kueleza kuwa ndani ya serikali kuna hardliners na masalia ya hayati Magufuli, kwani walitaka masalia waende na Magufuli na yataondoka taratibu kama shida ni masalia?

Kwa kuwa dhamira yao ya kuona Magufuli hayupo imetimia sasa wanakuwa "frustrated" kuona hakuna dalili za kubadili kila kitu kwa faida yao.

Lakini pia Profesa Cheeseman hapaswi kutumia elimu yake kuwahadaa watazamaji na walaji habari walioko hukohuko majuu kwa maslahi yake binafsi.
 

Ingekuwa ni kuendeleza "mbagazo dhidi ya nchi ya Tanzania" ningekuunga mkono kukemea...

Lakini kama serikali ndiyo inayobagazwa, acha iwe hivyo maana serikali ni kikundi cha watu wachache chenye malengo na maslahi fulani mabaya au mazuri...

å Kuna serikali nzuri, kuna serikali mbaya na za kishetani

å Kuna serikali halali na kuna serikali haramu..

å Serikali hufa na kupita, nchi hudumu kizazi na kizazi...

å Hii serikali ya CCM ni haramu, acha ijisadie kujibagaza yenyewe..

å Hii serikali ya CCM na Samia Suluhu Hassan ni mbaya na si halali, ni lazima ibagazwe na kusemwa vibaya. Tatizo ni lake. Haitaki kujirekebisha ili iwe serikali nzuri...!

BACK TO THE TOPIC:

1. Kama hakukamatwa kwa "AMRI YA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN" ili kuzuia kongamano la kikatiba la ndani la CHADEMA, ukweli wa "amri ya Rais" ya kukamatwa kwake na sababu ni nini sasa? Ni Ugaidi kama ilivyosema?

2. Kama ni gaidi kweli, hapa ndipo tatizo lilipo...

Kwamba, inawezekana hujui kuwa polisi walisema kuwa wanamjua Freeman Mbowe ni gaidi wa "kuua viongozi wa serikali" kwa muda mrefu. Sasa kama walikuwa wanajua hili, ikawaje wakawa wajinga na wapumbavu wa kiwango kile hata kumkamata ktk mazingira yale...?

3. Mimi nadhani wasingekuwa wajinga na wapumbavu iwapo wangefanya hivi:

Kwamba wangewasuburi wafanye kongamano lao kesho yake huku polisi wa Mwanza na Tanzania yote wakiwa wamezunguka eneo la Kongamano na wakiwa na magari yao yote ya deraya, mabomu yote na bunduki zote ili CHADEMA wangemaliza tu kongamano lao, basi, wanamkamata gaidi wao Mbowe..

Unaonaje? Je, hwangefanya vile unadhani ingeleta maswali kweli?

Yes, obviously yangekuwapo maswali lakini si haya tunayojadili hapa leo. Yangekuwa mengine kabisa..!!

Lakini kwa kuwa, serikali hii iko so desperate na anguko lake, wote huko hawana akili mpaka na Rais wao...

CONCLUSION:

Hakuna mtu mwerevu atakayeshindwa kung'amua kuwa kukamatwa kwa Freeman Mbowe ni mpango mahususi ukihusisha serikali yote chini ya mwongozo wa Rais Samia Suluhu Hassan mwenyewe...

Anayebisha kwenye hili atakuwa ndiye mjinga pekee...
 
Umepiga kwenye mshono. Paskal alikuwa mwandishi wa viwango vya kina Jenerali Ulimwengu, Lula wa Ndali Mwananzela na kina Mzee Mwanakijiji. Lakini kwa sasa amekuwa useless anaongozwa na mkuno wa njaa ya tumbo.

Umempa za uso. Haaminiki tena.
 
Pascal unadhani ni wewe pekee umeskiza CNN?

Hakuna sehemu huyo Prof amesema Rais ameagiza Freeman akamatwe.

Kwanini umeamua kudanganya watu?

Of course, inafahamika mrengo wa utoaji habari wako ulibadilika baada ya kuletewa kashkashi na serikali iliyopita.

Lakini sikuwahi kujua ulibadilika kiasi cha kutumia uongo kujenga hoja.
 
Nadhani wewe ndo umezusha hapa kwa maslahi yako.Nilivyomuelewa huyo profesa amesema ni either Mama kaagiza hayo mambo au mama kazidiwa nguvu na watu wa mwendazake ambao bado wapo wengi serikalini,na akasisitiza kuwa kwa maoni yake mama mpaka sasa ameshindwa kuweka mfumo mzima utakoendana na maono yake
 
Paskali ninachokupendea wewe ni hustler usiekata tamaa. Bado unaendelea kufukuzia teuzi japo zimekuwa zikikulamba chenga ya mwili kila mara tokea enzi za mwendazake.

Tukirudi kwenye mada yako naona kidogo umeamua kujitoa ufahamu kwa maslahi yako binafsi. Haiwezekani mtu mwenye upeo wako tunaekufahamu wewe Pasco eti hujui kinachoendelea hapa nchini.

Huoni ukiukwaji wa sheria, ukandamizaji wa haki za binadamu, uvunjifu wa katiba, kodi kandamizi na zakinyonyaji kwa raia, unyanyasaji na ubambikiaji kesi unaonendelea?

Pasco kweli huyaoni yote haya? Huo upofu umeupata wapi Pasco?

Muogope Mungu mkuu.
 
Umeandika ironically, lengo ni kufikisha ujumbe kuwa Mbowe kakamatwa kwa amri ya Rais ili kupunguza harakati za katiba mpya na vuguvugu la kupinga tozo za miamala.

Umempamba kwa stahiki yake huyo proffessor kujenga picha kuwa report ya CNN imeshiba isipuuzwe.

Very few will understand you.

Well ploted.
 
Kama ni kweli kwanini polisiccm wanahaha kutafuta mtu wa kumuwekea Mbowe dhamana ili wanuachie? Gaidi anayepanga mpango wa kuwaua Viongozi wa juu wa Serikali tangu lini akapewa dhamana? Serikali haramu ndivyo zilivyo ndiyo ni haramu kwa sababu haikuchaguliwa katika uchaguzi huru na wa haki.

Hivi ni uongo kwamba Mbowe amekamatwa na polisi wa Ccm?
Kwamba vyombo vya nje ni mabeberu? Mayala una matatizo ya kujipendekeza
 
Tutawasifia wakitupa $600M za wizara za Afya na chanjo lakini kukosolewa hatutaki

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…