Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Nimekaa nikawaza ,kufikiria na kurudisha kumbukumbu nyuma mahali tulikotoka ,tulipo na tunakokwenda na kufikia hatua kusema kuwa kwa hakika Watanzania bila kujali itikadi za vyama vyetu, makabila yetu,Dini zetu,jinsia zetu,ukanda na rika.
Tuna kila sababu ya kusema Asante Rais Samia ,asante mama yetu Mpendwa kwa hapa ulipotufikisha.Mahali ambapo kila mmoja analiona tumaini lililo jema machoni pake,mahali ambapo kila mmoja anafuraha na tabasamu katika paji la uso wake,mahali ambapo watu wanatembea njiani wakiwa na amani na siyo mtu kuzungumza mwenyewe njiani utafikiri kichaa.
Embu angalia ndugu zangu Leo hii wanafunzi wanasoma bure kabisa mpaka kidato cha sita na kupewa mikopo ya Elimu ya juu kwa wote wenye sifa.leo hii wanafunzi wote wana ripoti shuleni kwa wakati mmoja kwa sababu ya uwepo wa madarasa ya kutosha yaliyojengwa na Rais Samia, tofauti na zamani ambapo wengine waliishia kuolewa baada ya kuwa wamefaulu lakini madarasa hayatoshi kuwabeba wote kwa wakati mmoja.
Leo hii miradi mikubwa ya umeme na SGR tunashuhudia ikikamilika na kuwa kama Ulaya .hakuna cha mgao wa umeme wala kukatika katika kwa umeme na ukiona umeme umekatika basi ujuwe kuna matengenezo madogo madogo yanafanyika . Leo hii hakuna makelele ya majenereta mitaani.
Leo hii vijana wanaomaliza vyuo vikuu wana matumaini ya kupata ajira serikalini,kwa kuwa serikali ya mama yetu mpendwa Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan inatoa ajira kila mwaka na kwa Secta zote.leo hii tunaona wakulima wakiuza mazao yao kwa bei nzuri kabisa yenye kuwalipa jasho lao.leo hii tunaona hali ya kiuchumi ikiwa nzuri na mzunguko wa pesa mitaani ukiwa mzuri.
Tunashuhudia kwa macho yetu biashara zikifunguliwa kila mahali , wawekezaji wakiongezeka kila siku,watalii wakimiminika kufikia Millioni 1.8,viwango vya furaha vikiongezeka kwa watanzania ,hali za maisha zikiendelea kuboreka kila uchao.watumishi wa umma wakiendelea kuboreshewa maslahi yao ili wafanye kazi kwa ufanisi na morali.
Tunashuhudia leo hii wagonjwa waliokuwa wakisafiri kwenda kupata matibabu nje ya nchi,sasa wanatibiwa humu humu Nchini baada ya kuboreshwa kwa huduma za afya pamoja na kuongeza madaktari bingwa na bobezi wa magonjwa mbalimbali katika maeneo mbalimbali.
Ni kweli changamoto huwa hazikosekani.maana hata Marekani tu iliyopata uhuru wake mwaka 1776 bado inapambana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto ya ajira kwa vijana ,gharama kubwa za matibabu n.k. lakini hapa Nchini tunaona namna Rais Samia na serikali yake anavyopambana katika kutatua changamoto.ikumbukwe ya kuwa maendeleo wakati mwingine huja na changamoto.
mfano kama ulikuwa na changamoto ya uhaba wa shule au madarasa na ukafanikiwa kujenga basi tegemea kupata changamoto ya walimu,maabara kwa masomo ya sayansi n.k.kwa hiyo tufahamu kuwa kila kitu huja na changamoto. Lakini tunaona namna mama yetu mpendwa anavyo pambana usiku na mchana kutatua changamoto mbalimbali.
Kipi ambacho hajafanya Mama yetu? Wapi ambako hajagusa Watanzania wenzangu? Wapi na nani ambaye hajafikiwa na Mama? Embu angali leo vyama vya siasa vinafanya siasa na mikutano ya hadhara kwa uhuru bila bughudha wala wasiwasi.leo watu wapo huru kuzungumza watakayo na yajazayo vifua vyao bila hofu wala uoga..
Ni nani ameruhusu haya kama siyo Mama yetu kipenzi Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan? Ni nani amefungua milango hii kama siyo 4R za Mama wetu zilizoliunganisha Taifa letu?
Naomba tuendelee kumuunga Mkono Rais na Mama yetu huyu mwenye moyo wa upendo,huruma, unyenyekevu,ukarimu na uzalendo wa hali ya juu sana.Tutambue hata hivyo kazi njema hii inayofanywa na mama yetu kuna baadhi ya watu hawafurahi .kwa sababu wao kiu yao ni kutaka ashindwe na apoteze muelekeo ili wapate nafasi ya kutimiza ajenda zao kwa maslahi yao binafsi na magenge yao.
Tumtie moyo Mama yetu,tusimuache mpweke wala kuruhusu mtu akamshambulia huku sisi tukiwa kimya.tuwe wakali kwa yeyote atakaye taka kumhujumu au kumkwamisha Mama yetu.maana yote afanyayo ni kwa ajili yetu watanzania wenyewe.tumlinde,kumtetea Na kumpigania Rais wetu zidi ya mafisi ya madaraka.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.