Watanzania tuweke attention yetu kwenye suala la kubinafsishwa kwa bandari, habari za uteuzi wa makatibu na wakurugenzi wa halmashauri sio ishu kubwa

Utapewa lini huyo kiongozi?.wakubadilisha mambo ni wananchi wenyewe.Na tutabadilisha mambo tukianza na katiba bora.sasa wewe endelea kusubiri Mungu akuletee huyo kiongozi.
Hata ipite miaka 100 atapatikana tuu. Kiongozi ni dira. Mkishakuwa na kiongozi huru asiye na viashiria vya kutumikishwa kimwili na kiroho hapo baraka za Mungu tutaziona na kila mtu atafurahi kuwa mtanzania.
 
Kweli kabisa. Kuna pattern fulani imeanza kutokea, kila suala lenye kugusa mustakabhali wa taifa ikitokea-Tunasikia uteuzi, saa nyingine tunabaki tunajiuliza kwanini imetokea ghafla bin vu!

Ukweli ni kwamba hakuna anayeweza kumpangia Rais mjadala, hakuna anayeweza kumpangia Rais muda, wala hakuna anayeweza kumpangia Rais Mteuzi wake. Ila tunaweza tusikubali kuyumbishwa na Mijadala isiyo na tija-atleast for now.

Sambamba, imekuwa dhahiri jamvini kusikia na kuona utetezi ambao, kwa namna moja au nyingine unatetea muendelezo wa Ukoloni mamboleo, mfano Utasikia Serikali iingie ubia na Raia au kwa lugha ya kigeni kuwe na uwepo wa "Private/Public partnership" na watetezi wa hoja hio huwa wanafunika hoja za wapingaji, yaani watetezi wa Serikali kuendesha mashirika.

...na utakuta kuna sehemu huwa wanakubaliana,(where there is harmonization au ndoa za hoja zinazokinzana kukutana) napo ni Ujengaji wa Miundombinu kwa kutumia nguvu za Serikali-ambayo ina maana fedha ya mlipa kodi au Mtanzania ndiyo inayotumika-hata ikiwa ni ya Mikopo;bado ni mzigo wa Mtanzania, hapo utasikia "uwekezaji huo" au Investment hiyo ni nzuri na itazungusha fedha mtaani, kweli hilo linatokea, ila baada ya mradi kuisha na wakandarasi kulipwa fedha hiyo hutoweka na kuwepo kwenye mifuko ya wachache., including, fedha nyinginre za kigeni kubakia katika nchi zilipotoka wakandarasi.....hapa unajiuliza, kwanini hawa wawekezaji wasije kujenga barabara au madaraja, au mtandao wa mawasiliano wakope wenyewe, walipe hao wafanyakazi wenyewe, halafu ndio waje waombe watoe ubia kwa Serikali au kwa lugha nyepesi a true Public Private partneship -yaani sasa waingie ubia na Wananchi wa Tanzania kutafuta hela za uendeshaji kama vile inavyotokea katika Nchi nyingi za Magharibi....Kwanini isiwe hivyo? Badala ya Watanzania kunyonywa hela, halafu tunaingia Ubia na makampuni ya Nje tena mengine yasiyokuwa na Fedha kwa kuwawezesha na kuwatwisha, mfano hapa Bandari halafu wao waende nje na kutafuta ipos wake huko nje...ikiwa ina maana wanalazimika kuwarudishia wawekezaji wao wa Capital makwao kabla hawajarudisha kwetu....wakati huohuo tushapoteza mabilioni kwa kuwekeza fedha za walipa kodi! it is absurd.
Haijalishi.... sasa unasikia watetezi hawa wa hoja ya kuuzwa kwa Bandari(whether true or not) wakieneza na kuanzisha, kwa lengo la kufunika mjadala muhimu kwa karne hii kwa mTanzania yaani, wanafanya hivi kwa makusudi wakiwa na Self-Interest yani kwa upendeleo wa Wawekezaji wa nje dhidi ya wawekezaji wa ndani au kwa lugha nyepesi kabisa upendeleo wa Makaburu dhidi ya Mzawa, Mwafrika.
Hawa jamaa wawekwe kwenye listi ya wasalaiti!

Fazil.....Haswa, tuendeleze mjadala wa Bandari badala ya kurukia hizi hoja za Nani kachaguliwa nani kaachwa, tena unakuta wanaleta Provocative contents....yaani maudhui yenye Uzushi na uchonganishi ili kuleta hisia kali na kukufanya "Binadamu" kuondoka kwenye reli ya majadiliano Muhimu kama hili la Bandari.

Naunga mkono hoja!

Aluta Continua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…