Watanzania wafurahia kauli ya Rais Samia kushughulikia uchumi kwanza kabla ya Katiba Mpya

Watanzania wafurahia kauli ya Rais Samia kushughulikia uchumi kwanza kabla ya Katiba Mpya

Chee4

Member
Joined
May 17, 2021
Posts
35
Reaction score
125
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na hatua ya Mhe. Rais wa Samia Suluhu Hassan, juu ya jitihada zake za kuhakikisha anainua uchumi wa Watanzania na akisisitiza suala la Katiba Mpya apewe muda kidogo.

Watanzania hao kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, na Mbeya wamesema ni kweli Rais Samia anahitaji muda wa kutosha kuboresha uchumi wetu ambao umeshuka kutokana na Corona hiyo asisumbuliwe na porojo za Katiba Mpya na Mikutano ya hadhara.

Rais Samia akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo kuhusiana na suala la Katiba Mpya amesema[emoji116]

“Niombe sana kama mnavyosema nimeanza vizuri nipeni muda nisimamishe uchumi wa nchi, halafu tutashughulikia mingine iwe Katiba, na mikutano ya siasa.”

Hakika kwasasa Watanzania wanaelewa mahali gani ambapo Mhe. Rais Samia anawapeleka ili kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora zaidi, na si kuanzisha michakato inayogharimu pesa nyingi na mwishowe Wakina Mbowe na wenzake wataishia kukimbia.

#KaziIendelee #Siku100ZaSuluhu
 
Sema Mataga wamefurahia sio Watanzania.

Muda ndio utamfundisha vizuri kuhusu Katiba mpya na watanzania. Katiba mpya ndio kete pekee inayoweza kumpa political mileage. Kama hajui hilo, subiri atakachokutana nacho.
 
Hili suala la katiba liwe sambamba ikiwezekana mbele kuliko hata huo uchumi.

Umauti ni wakati wowote, akiondoka leo duniani tunaweza pata jendawazimu kuliko mwendazake majuto yakwa level ya SGR.
 
Acha kuwalisha maneno Watanzania. Sisi Watanzania tunataka katiba mpya wala hatuja furahishwa na porojo yeyote kwasababu katiba nzuri haizuii maendeleo ya nchi yeyeto duniani acheni kuogopa kuwajibika vinyamkera.

Katiba mpya ni sasa .
 
Mikutano ya Siasa ni muhimu sana kwa afya ya Demokrasia Nchini, kama anasema mchakato wa Katiba atafanya baadae lakini mikutano ya Siasa airuhusu iko Kikatiba ili tulumbane kwa Hoja kwenye Majukwaa.
 
“Niombe sana kama mnavyosema nimeanza vizuri nipeni muda nisimamishe uchumi wa nchi , halafu tutashughulikia mingine iwe Katiba, na mikutano ya siasa.”
Tunasisitiza chondechonde Mama usiende kuomba ushauri wa aina yoyote Msoga, ukienda utakachoambiwa changanya na zako
 
Ukiona watu wanafurahia kwamba hamna katiba mpya unaweza fikiri labda hawapo Tanzania.

Katiba ni kwa ajili ya Watanzania wote!
 
Sema Mataga wamefurahia sio watanzania.
Muda ndio utamfundisha vizuri kuhusu Katiba mpya na watanzania. Katiba mpya ndio kete pekee inayoweza kumpa political mileage. Kama hajui hilo, subiri atakachokutana nacho.
Mataga wanajifuraisha furaha ya bandia, baada ya hukumu ya kesi ya kina Mbowe kubatilishwa na leo Mdude kupata uhuru wake!
 
Sema Mataga wamefurahia sio watanzania.
Muda ndio utamfundisha vizuri kuhusu Katiba mpya na watanzania. Katiba mpya ndio kete pekee inayoweza kumpa political mileage. Kama hajui hilo, subiri atakachokutana nacho.
Bavicha mmepigwa chenga leo
 
Acha kuwalisha maneno Watanzania. Sisi Watanzania tunataka katiba mpya wala hatuja furahishwa na porojo yeyote kwasababu katiba nzuri haizuii maendeleo ya nchi yeyeto duniani acheni kuogopa kuwajibika vinyamkera.
Katiba mpya ni sasa .
Watz kwa takwimu zipi? Twitter?
 
Nawasalimu kwa jina la JMT. Kazi Iendelee.

Tuna haja ya kufanya marekebisho kwenye baadhi ya nukta zilizopo kwenye katiba tulonayo mikononi, ile ya 1977, tena haja kubwa tu! Hata hivyo kwa hali ya nchi yetu ilivyo sasa zoezi la mchakato wake usubiri kwanza.

Kuna mengi yanahitaji kuwekwa sawa kabla ya hiyo katiba tunayoidai. Na kwa kuwa ishara tumeanza kuziona juu ya kusawazishwa kwa hayo mambo, naona ni vema na hili la katiba tulipe muda. Tusiwe na haraka kama mkojo wa asubuhi, haraka haraka hukosa baraka baadae mambo yakaharibika.

Mh. Rais yupo sahihi kuomba tumpe muda, jambo nililolipenda kwake ni kwamba hajakataa kuhusu katiba mpya, na yeye anajua haja ya kufanya marekebisho baadhi ya vitojo kwenye katiba hiyo. Lakini kuliendea hilo kwa haraka na pupa kama inavyodaiwa haitokua na afya kwa makuzi na maendeleo ya nchi yetu.

Niwape mfano wa karibu tu, sasa tuna changamoto kubwa ya uhaba wa ajira hasa kwenye serikali, vijana wetu wengi hawajaajiriwa; kimkakati suala la ajira ndilo ambalo serikali inatakiwa kulipa kipaumbele kwa sasa na huku mambo mengine yakifanyiwa kazi. Kuanzisha mchakato wa katiba mpya wakati vijana wetu wana haja kubwa ya ajira kuliko hiyo katiba ni kiwapuuza na kupuuza uimara wa nchi yetu hapo baadae.

Huu ni mfano mmoja tu, na ipo mingi. Tukumbuke mchakato wa katiba unahitaji fedha za kutosha na si kidogo. Hivyo Mh. Raisi anaposema tumpe muda tumuelewe..! Hata yeye ni mdau na ni mhitaji wa hiyo inayoitwa katiba mpya..! Lakini tufanye kilicho muhimu kwa sasa..!!
 
Siasa za Majukwaani sio kitu cha kuomba ni haki yetu ya Kikatiba ya zamani.
Aahahhha nafahamu hilo mkuu! Ila kuna mengi tuliporwa na yanahitaji muda kuyarejesha kwenye main track. Hivyo haiwezekani yote yakafanywa kwa wakati mmoja. Njia mbili zilimshinda fisi
 
.
IMG_20210702_083930.jpg
IMG_20210702_084152.jpg
IMG_20210702_083922.jpg
IMG_20210702_083916.jpg
 
Back
Top Bottom