Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mwananchi wa kawaida mkoani akipata maji safi muda wote hana muda wa kujiuliza masuala ya makamu ya pili na wa kwanza wa rais eti ni yupo atoke Bara au visiwani.Hili la kudai katiba mpya linahitaji nguvu ya kuelimisha raia (public awareness), kwani huku mtaani watu wengi hawana hata habari na kitu kinaitwa katiba mpya.., muda wa kuwa wanaona pesa bado haijafika mikononi mwao. Raia wengi wapo na matumaini kwa Mh. Rais wakisubiri aibadilishe hali yao ya kiuchumi ambayo kwa kiasi kikubwa ni mbaya na wala sio aibu kusema.
Huko mijini hasa (Dar) wenye ulewa wa hitajio la katiba mpya ni wachache sana, na wengi wao ktk hao wachache ni wale ambao wana imani mchakato wa katiba mpya utawanufaisha kwa namna moja au nyingine. Kuna mchongo wa NGO's hapo...! (Hili silisemi sana)
Nikiangalia kwa jicho la nne, nazifananisha hizi harakati kama juhudi za kujikinga na korona hapa kwetu kwa sasa..! Kwani huku mtaani watu hawana habari tu kama kuna korona, hamna precaution measures zinazochukuliwa na watu wanaendelea na shuguli zao tu. Wakati kwa upande wa shuguli za kiserikali na shuguli rasmi na kwenye mijumuiko yake watu ni full face masks.
Nahotaka kusema ni kwamba kuna kazi kubwa ya kuwaelewesha raia waone umuhimu wa katiba mpya... Wengi huku hawajui...!!!!
Mtu wa kawaida mwenye mtoto mwenye akili anayefaulu shuleni wasiwasi wake ni kupata nafasi ya kuingia chuo kikuu hana huo muda wa kuwazia serikali mbili moja au nne.
Mkulima akiweza kusafirisha mauzo yake Kenya au Sudan na akapata malipo yake kwa wakati hana muda wa kujiuliza faida au hasara za wabunge wa viti maalum wanaolalamikiwa na CHADEMA kwamba hawatakiwi kuwepo mle bungeni.
Katiba mpya inaongelewa humu jukwaani na ndani ya vikao vya vyama vya siasa, haina mashiko ya moja kwa moja kwenye maisha ya mtanzania wa kawaida.