Watanzania wafurahia kauli ya Rais Samia kushughulikia uchumi kwanza kabla ya Katiba Mpya

Watanzania wafurahia kauli ya Rais Samia kushughulikia uchumi kwanza kabla ya Katiba Mpya

Aahahhha nafahamu hilo mkuu! Ila kuna mengi tuliporwa na yanahitaji muda kuyarejesha kwenye main track. Hivyo haiwezekani yote yakafanywa kwa wakati mmoja. Njia mbili zilimshinda fisi
Mama anatakiwa ajifunge kibwebwe kwelikweli tunautaka Ugali wetu 😁
 
Mama anatakiwa ajifunge kibwebwe kwelikweli tunautaka Ugali wetu 😁
Aahahhhahaa usijali, naye ni mpishi hodari. Ile miaka alokaa ughaibuni imempika vizuri, hawezi kutuangusha...!
 
Aahahhhahaa usijali, naye ni mpishi hodari. Ile miaka alokaa ughaibuni imempika vizuri, hawezi kutuangusha...!
Ni kweli alichosema, unajua Uchumi uliuwawa na Magufuli, sasa tunataka Uchumi wetu wa Ugali mezani sio ule wa kwenye Magazeti ya kufungia Vitumbua.
 
Hili la kudai katiba mpya linahitaji nguvu ya kuelimisha raia (public awareness), kwani huku mtaani watu wengi hawana hata habari na kitu kinaitwa katiba mpya.., muda wa kuwa wanaona pesa bado haijafika mikononi mwao. Raia wengi wapo na matumaini kwa Mh. Rais wakisubiri aibadilishe hali yao ya kiuchumi ambayo kwa kiasi kikubwa ni mbaya na wala sio aibu kusema.

Huko mijini hasa (Dar) wenye ulewa wa hitajio la katiba mpya ni wachache sana, na wengi wao ktk hao wachache ni wale ambao wana imani mchakato wa katiba mpya utawanufaisha kwa namna moja au nyingine. Kuna mchongo wa NGO's hapo...! (Hili silisemi sana)

Nikiangalia kwa jicho la nne, nazifananisha hizi harakati kama juhudi za kujikinga na korona hapa kwetu kwa sasa..! Kwani huku mtaani watu hawana habari tu kama kuna korona, hamna precaution measures zinazochukuliwa na watu wanaendelea na shuguli zao tu. Wakati kwa upande wa shuguli za kiserikali na shuguli rasmi na kwenye mijumuiko yake watu ni full face masks.

Nahotaka kusema ni kwamba kuna kazi kubwa ya kuwaelewesha raia waone umuhimu wa katiba mpya... Wengi huku hawajui...!!!!
 
Hili la kudai katiba mpya linahitaji nguvu ya kuelimisha raia (public awareness), kwani huku mtaani watu wengi hawana hata habari na kitu kinaitwa katiba mpya.., muda wa kuwa wanaona pesa bado haijafika mikononi mwao. Raia wengi wapo na matumaini kwa Mh. Rais wakisubiri aibadilishe hali yao ya kiuchumi ambayo kwa kiasi kikubwa ni mbaya na wala sio aibu kusema...
Tangu mwaka 1961 mnajenga uchumi. Mmefikia wapi??

Swala la kujenga uchumi halina mwsiho
 
Nahotaka kusema ni kwamba kuna kazi kubwa ya kuwaelewesha raia waone umuhimu wa katiba mpya... Wengi huku hawajui...!!!
Kama hii ya Zamani inavunjwa na Viongozi sijui hata hiyo Mpya kama wataiheshimu ila Wafungulie Siasa za Majukwaani ili tuwafundishe Raia umuhimu wa Katiba Mpya kwetu na kwa Vizazi vijavyo
 
Kama hii ya Zamani inavunjwa na Viongozi sijui hata hiyo Mpya kama wataiheshimu ila Wafungulie Siasa za Majukwaani ili tuwafundishe Raia umuhimu wa Katiba Mpya kwetu na kwa Vizazi vijavyo
Hili ndilo la kufanywa sasa..!
 
Tangu mwaka 1961 mnajenga uchumi. Mmefikia wapi??

Swala la kujenga uchumi halina mwsiho
Hata nyumbani ktk familia, wana familia wanaweza wakadai nguo za sikukuu wakati baba ndio anajua kiasi cha pesa kilichopo kinatosha kununua mahitaji ya pilau tu na vinywaji. Hivyo atawaomba wasubiri kwa sikukuu hii wavae nguo za zamani lakini atahakikisha wanakula vizuri na vitamu. Sikukuu ijayo mambo yatakua sawa.., watapata na nguo za kutokea...!

Ndio tangu 1961 lakini hata hivyo hali ya uchumi wa nchi ina badilika. Huwezi fananisha hali ya mwaka 1961 na mwaka 1985, na mwaka 1995, na mwaka 2005, na mwaka 2015 na mwaka 2021. Ukiangalia utaona kuna hatua zinapigwa kuonesha tunakaribia kufika tunakokutaka. Lakini hata hivyo vikwazo vipo pale pale..., ni kama hivi Mh. Raisi yupo kwenye structural adjustment wanakuja watu kumchanganya na madai ya katiba mpya..!
 
Chadema hawana kitu cha kufanya mda huu, hawana kazi wala ruzuku lazima watafute jambo ili wafadhili wao watoe hela...hizi kele zao haziwezi kumtoa Mama Samia kwenye reli
 
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na hatua ya Mhe. Rais wa Samia Suluhu Hassan, juu ya jitihada zake za kuhakikisha anainua uchumi wa Watanzania na akisisitiza suala la Katiba Mpya apewe muda kidogo...
Kila awamu ya serikali humu jf kuna id za wapigapanda wa upande wake.
 
Tangu mwaka 1961 mnajenga uchumi. Mmefikia wapi??

Swala la kujenga uchumi halina mwsiho

Kimsingi ni sababu isiyo na mashiko. Hakuna siku iwayo yoyote ile uchumi utasimama kujengwa. Kwa sababu hii maana yake katiba mpya haina nafasi. Lakini unaweza kuona upeo wa mtu ulipo.
 
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na hatua ya Mhe. Rais wa Samia Suluhu Hassan, juu ya jitihada zake za kuhakikisha anainua uchumi wa Watanzania na akisisitiza suala la Katiba Mpya apewe muda kidogo..
No research no right to speak. Hiyo tathmini kuwa watz wamefurahi umeipata kwa siku moja tu? Huu sio tu ujinga bali ni uongo uliorithiwa kutoka kwa mwendazake
 
Kwahiyo Matukio yeyote yakitokea yatapuuzwa hadi huo uchumi ushughulikiwe kwanza enh? hebu atutajie hiyo mikakati yake ya uchumi wetu sio raia utakavyopanda? au ndio kupandisha bei za kila kitu mafuta n.k? Ndio upuuzi huu wa katiba ya sasa one person show.... Yaani hadi uchumi wetu anasema yeye ndio atatupandishia gaddemed
 
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na hatua ya Mhe. Rais wa Samia Suluhu Hassan, juu ya jitihada zake za kuhakikisha anainua uchumi wa Watanzania na akisisitiza suala la Katiba Mpya apewe muda kidogo...
Kwa sasa mh. Rais tunakuomba uone umuhimu wa katiba mpya kwani hauna mipaka ya kuijenga na huwa haukamiliki kwamba hapa tayari sawa na tajiri ambavyo hatosheki
 
Tupo uchumi wa kati wa viwanda... Mnataka uchumi upande uwe kama wa china na Marekani ama?
 
Katiba Safi ndiyo itakayoleta uchumi endelevu, ni jukumu la serikali kuimarisha uchumi sambamba na kutii matakwa ya wananchi kuhusu katiba mpya.

Tunahitaji katiba mpya jamani!
 
Yaani mama Samia katuahidi ongezeko la mishahara mwakani, anatokea mwana CHADEMA aliyezoea kula hela kwa kupiga domo anataka yaundwe makamati ya katiba,sijui bunge yalambe pesa zote mama samia alizopanga atumie kutuongezea mishahara,hatukubali asilani.

Mama Samia simamia kwanza la maslahi ya wafanyakazi,tuko wote, hao CHADEMA wanataka fungu la maslahi ya watumishi likaliwe kwenye ajenda za kisiasa.

Mama Samia kwenye hili tutasimama na wewe! Kataa wito wa CHADEMA, wanajenga mazingira ya upigaji.
 
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na hatua ya Mhe. Rais wa Samia Suluhu Hassan, juu ya jitihada zake za kuhakikisha anainua uchumi wa Watanzania na akisisitiza suala la Katiba Mpya apewe muda kidogo.

Watanzania hao kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, na Mbeya wamesema ni kweli Rais Samia anahitaji muda wa kutosha kuboresha uchumi wetu ambao umeshuka kutokana na Corona hiyo asisumbuliwe na porojo za Katiba Mpya na Mikutano ya hadhara.

Rais Samia akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo kuhusiana na suala la Katiba Mpya amesema[emoji116]

ā€œNiombe sana kama mnavyosema nimeanza vizuri nipeni muda nisimamishe uchumi wa nchi, halafu tutashughulikia mingine iwe Katiba, na mikutano ya siasa.ā€

Hakika kwasasa Watanzania wanaelewa mahali gani ambapo Mhe. Rais Samia anawapeleka ili kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora zaidi, na si kuanzisha michakato inayogharimu pesa nyingi na mwishowe Wakina Mbowe na wenzake wataishia kukimbia.

#KaziIendelee #Siku100ZaSuluhu
USITUSEMEE WATANZANIA SEMA WEWE UMEFURAHIA. UCHUMI UPI UNAOJENGWA SASA NA WAKATI TULIAMBIWA UCHUMI UMEIMARIKA NA SASA TUMEINGIA UCHUMI WA KATI. TUSISAHAU MLIYOYASEMA. HIVI MNATUONA WATANZANIA MAMBUMBU SANA
 
Watanzania kutoka maeneo mbalimbali wamefurahishwa na hatua ya Mhe. Rais wa Samia Suluhu Hassan, juu ya jitihada zake za kuhakikisha anainua uchumi wa Watanzania na akisisitiza suala la Katiba Mpya apewe muda kidogo.

Watanzania hao kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo ya Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, na Mbeya wamesema ni kweli Rais Samia anahitaji muda wa kutosha kuboresha uchumi wetu ambao umeshuka kutokana na Corona hiyo asisumbuliwe na porojo za Katiba Mpya na Mikutano ya hadhara.

Rais Samia akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari ambapo kuhusiana na suala la Katiba Mpya amesema[emoji116]

ā€œNiombe sana kama mnavyosema nimeanza vizuri nipeni muda nisimamishe uchumi wa nchi, halafu tutashughulikia mingine iwe Katiba, na mikutano ya siasa.ā€

Hakika kwasasa Watanzania wanaelewa mahali gani ambapo Mhe. Rais Samia anawapeleka ili kuhakikisha maisha yao yanakuwa bora zaidi, na si kuanzisha michakato inayogharimu pesa nyingi na mwishowe Wakina Mbowe na wenzake wataishia kukimbia.

#KaziIendelee #Siku100ZaSuluhu

imeisha hio
 
Aliyekupa ruhusa ya kuwasemea watanzania ni nani, mmekaa kwenye vikao vyenu vya kahawa mmeshajiona nyinyi ndio watanzania.
 
Back
Top Bottom