Watanzania wafurahia kauli ya Rais Samia kushughulikia uchumi kwanza kabla ya Katiba Mpya

Mwananchi wa kawaida mkoani akipata maji safi muda wote hana muda wa kujiuliza masuala ya makamu ya pili na wa kwanza wa rais eti ni yupo atoke Bara au visiwani.

Mtu wa kawaida mwenye mtoto mwenye akili anayefaulu shuleni wasiwasi wake ni kupata nafasi ya kuingia chuo kikuu hana huo muda wa kuwazia serikali mbili moja au nne.

Mkulima akiweza kusafirisha mauzo yake Kenya au Sudan na akapata malipo yake kwa wakati hana muda wa kujiuliza faida au hasara za wabunge wa viti maalum wanaolalamikiwa na CHADEMA kwamba hawatakiwi kuwepo mle bungeni.

Katiba mpya inaongelewa humu jukwaani na ndani ya vikao vya vyama vya siasa, haina mashiko ya moja kwa moja kwenye maisha ya mtanzania wa kawaida.
 
Aahahhhaa ww bro mbona umekandamiza sana..!!? Taratibu bhana..! Katiba kufanyiwa marekebisho baadhi ya maeneo kuna umuhimu lakini ni siala la kwenda ngazi kwa ngazi si kama wanavyotaka watu fulani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…