PostGE2025 Watanzania wajitokeza kwa wingi kuomboleza kumbukumbu ya mauaji ya 29.10.2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
WATANZANIA WAJITOKEZA KWA WINGI KUOMBOLEZA MAUAJI YA 29.10.2025.

Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na serikali ilitangaza kuwa watu 518 walikufa katika ghasia zilizohusiana na uchaguzi wa Oktoba 2025.

Samia Suluhu Hassan ambaye anasema ni rais baada ya mauaji haya, hajatoa fidia kwa majeruhi na wafiwa kama tume ilivyo pendekeza.

Samia Suluhu Hassan mwanamke kutoka Zanzibari, alipoambiwa kuna watoto wamekufa zaidi ya mia tano, alisema hivi;

Nanukuu: "Lililotokea ni tukio la kutengeneza na waliolipanga walidhamiria kuangusha dola ya nchi yetu.”

β€œJe, tulipaswa kuwaangalia waandamanaji waliojiandaa kufanya mapinduzi mpaka wafanikiwe?”.

Yale hayakuwa maandamano. Zilikuwa vurugu zilizoandaliwa kwa madhumuni maalumu.

”Wanadai haki, haki gani? Kwa njia ipi? Hadi wachome vituo?"


”Nguvu inayotumika inaendana na tukio lililopo.”
Mwisho wa kumnukuu anayejiita rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokea huko Kizimkazi

UKIACHIA MBALI NUKU ZA WENYE MADARAKA, ZIPO NUKU ZA WATANZANIA HALISI WALIOPOTEZA NDUNGU ZAO

Christina John Richard, dereva wa lori mwenye umri wa miaka 22, alipigwa risasi Oktoba 30, 2025 akiwa anasubiri usafiri baada ya kwenda kazini.

Mama wa Christina (Tina) John Richard, dereva wa lori aliyefariki akiwa na miaka 22.

β€œAlikuwa nguzo ya familia yetu. Baba yake alifariki akiwa mdogo. Aliacha shule ili kusaidia familia, na ndoto zetu zilikatishwa na milio ya risasi.”

Ndugu wa Shabani Bakari Hamisi, kijana wa miaka 25 aliyepotea;

β€œTumeenda hospitali zote na baadhi ya vituo vya Polisi vikubwa vikubwa… tunaomba Serikali ingetupa namna yoyote kama kuna watu waliopotea kutokana na maandamano yaliyotokea.”

Living Mtena, aliyefiwa na mwanawe wa miaka 19

β€œMaumivu bado hayawezi kuvumilika. Mwanangu ameacha mwenza aliyekuwa na ujauzito wa miezi mitano. Leo nimebaki na mjukuu mwenye miezi saba.”

Elirehema Mkama, kuhusu ndugu ambaye hakurudi nyumbani

β€œTumetafuta kila mahali bila mafanikio. Hata tuliomba kupewa mwili wake, kama amefariki, ili tuweze kumzika, lakini hatujapata majibu. Hilo ndilo ombi letu kubwa zaidi kwa familia.”

James Mbatia, mwanasiasa

β€œTupewe miili yetu ya mashujaa wetu waliouawa … ili twende tukawasitiri ndugu zetu, tukawazike kwa heshima … bila kuendeleza ghadhabu zaidi.”

Askofu Wolfgang Pisa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania

β€œIlikuwa tukio la kusikitisha, la kutisha na lililosababisha vifo.”

Agnès Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International

β€œKila familia inayoomboleza inastahili majibu, haki na fursa ya kudai fidia.”

Mhudumu wa afya kutoka Dar es Salaam

β€œKatika zaidi ya miaka 15 ya kazi, sijawahi kuona jambo kama hili.”

Maumivu si kumpoteza mwanao pekee; ni kuendelea kuishi bila kujua alipo, bila mwili wa kumzika na bila majibu ya kukuondolea maswali.”Hapo hapo wanaojiita viongozi wa Serikali wanajifanya kama vile hakuna kilichotokea.
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
#TANZANIA: SIO TUGANGE YALIYORO NA YAJAYO, TUTUBU, TUSIPOTUBU TUTAELEKEA KUBAYA ZAIDI-PADRE KITIMA

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Dkt. Charles Kitima leo Oktoba 29, 2026 katika misa ya kuwakumbuka watu waliouawa wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 amesisitiza umuhimu wa viongozi kutubu, kujirekebisha na kujiepusha na vitendo viovu vya zamani ili kujenga mustakabali mwema na kuzuia kurudiwa kwa makosa yaliyosababisha madhara katika
jamii.
 
Tanzania imekuwa na picha mbaya na inajulikana nchi yenye Mauwaji makubwa Afrika Kwasababu ya Wenye mamlaka wanaomiliki vifaa na wanaoweza kufanya mauwaji bila kuhofia sheria za nchi. WALIOUWA OKT 29 NI WENYE MAMLAKA MAANA UKIANGALIA SIRAHA NA VIFAA VILIVYOTUMIKA NI HATARI SANA SIO KAWAIDA - PONDA Sheikh Ponda Ameamua kusema ukweli na ahoji wauaji kuwa na mamlaka, kumiliki magari kama Landcruiser, vifaa na karakana. Huyu Sheikh Ameamua kuwa mkweli siku zote hajawahi hata siku moja kubadilika au kuyumba kama watu wengine. Sheikh anaonyesha sura ya haki na ya kweli mbele za watanzania wote.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…