PostGE2025 Watanzania wajitokeza kwa wingi kuomboleza kumbukumbu ya mauaji ya 29.10.2025

PostGE2025 Watanzania wajitokeza kwa wingi kuomboleza kumbukumbu ya mauaji ya 29.10.2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
WATANZANIA WAJITOKEZA KWA WINGI KUOMBOLEZA MAUAJI YA 29.10.2025.

Tume ya Uchunguzi iliyoundwa na serikali ilitangaza kuwa watu 518 walikufa katika ghasia zilizohusiana na uchaguzi wa Oktoba 2025.

Samia Suluhu Hassan ambaye anasema ni rais baada ya mauaji haya, hajatoa fidia kwa majeruhi na wafiwa kama tume ilivyo pendekeza.

Samia Suluhu Hassan mwanamke kutoka Zanzibari, alipoambiwa kuna watoto wamekufa zaidi ya mia tano, alisema hivi;

Nanukuu: "Lililotokea ni tukio la kutengeneza na waliolipanga walidhamiria kuangusha dola ya nchi yetu.”

“Je, tulipaswa kuwaangalia waandamanaji waliojiandaa kufanya mapinduzi mpaka wafanikiwe?”.

Yale hayakuwa maandamano. Zilikuwa vurugu zilizoandaliwa kwa madhumuni maalumu.

”Wanadai haki, haki gani? Kwa njia ipi? Hadi wachome vituo?"


”Nguvu inayotumika inaendana na tukio lililopo.”
Mwisho wa kumnukuu anayejiita rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokea huko Kizimkazi

UKIACHIA MBALI NUKU ZA WENYE MADARAKA, ZIPO NUKU ZA WATANZANIA HALISI WALIOPOTEZA NDUNGU ZAO

Christina John Richard, dereva wa lori mwenye umri wa miaka 22, alipigwa risasi Oktoba 30, 2025 akiwa anasubiri usafiri baada ya kwenda kazini.

Mama wa Christina (Tina) John Richard, dereva wa lori aliyefariki akiwa na miaka 22.

“Alikuwa nguzo ya familia yetu. Baba yake alifariki akiwa mdogo. Aliacha shule ili kusaidia familia, na ndoto zetu zilikatishwa na milio ya risasi.”

Ndugu wa Shabani Bakari Hamisi, kijana wa miaka 25 aliyepotea;

“Tumeenda hospitali zote na baadhi ya vituo vya Polisi vikubwa vikubwa… tunaomba Serikali ingetupa namna yoyote kama kuna watu waliopotea kutokana na maandamano yaliyotokea.”

Living Mtena, aliyefiwa na mwanawe wa miaka 19

“Maumivu bado hayawezi kuvumilika. Mwanangu ameacha mwenza aliyekuwa na ujauzito wa miezi mitano. Leo nimebaki na mjukuu mwenye miezi saba.”

Elirehema Mkama, kuhusu ndugu ambaye hakurudi nyumbani

“Tumetafuta kila mahali bila mafanikio. Hata tuliomba kupewa mwili wake, kama amefariki, ili tuweze kumzika, lakini hatujapata majibu. Hilo ndilo ombi letu kubwa zaidi kwa familia.”

James Mbatia, mwanasiasa

“Tupewe miili yetu ya mashujaa wetu waliouawa … ili twende tukawasitiri ndugu zetu, tukawazike kwa heshima … bila kuendeleza ghadhabu zaidi.”

Askofu Wolfgang Pisa, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania

“Ilikuwa tukio la kusikitisha, la kutisha na lililosababisha vifo.”

Agnès Callamard, Katibu Mkuu wa Amnesty International

“Kila familia inayoomboleza inastahili majibu, haki na fursa ya kudai fidia.”

Mhudumu wa afya kutoka Dar es Salaam

“Katika zaidi ya miaka 15 ya kazi, sijawahi kuona jambo kama hili.”

Maumivu si kumpoteza mwanao pekee; ni kuendelea kuishi bila kujua alipo, bila mwili wa kumzika na bila majibu ya kukuondolea maswali.”Hapo hapo wanaojiita viongozi wa Serikali wanajifanya kama vile hakuna kilichotokea.
View attachment 3700960
View attachment 3700987
View attachment 3700988
Ilikuwa ni siku ya Kanisa kuungama kushiriki mpango ulioua watu wengi nchini. Damu za watoto wale wasioijua Katiba wala Tume ya uchanguzi walikufa wakidai Katiba na Tume huru ya uchaguzi ambayo hawaifahamu inafananaje na inasema nini. Kanisa limewatumia vijana kwenye maslahi yao. Dhambi iko kwenye madhabahu zao, damu ya vijana wale inawachoma kwenye nafsi zao, wanajiona wahalifu na wasiostahili kulitaja jina la Mungu.

Mimi nilielewa kwanini kanisa liliendesha misa, damu za watoto zinawasumbua kwakuwa walijua kuwa vijana wale wanawatuma kufanya kazi ambayo ingewaua wengi sana.
 
 
 
Back
Top Bottom