PostGE2025 Watanzania wajitokeza kwa wingi kuomboleza kumbukumbu ya mauaji ya 29.10.2025

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Hapo asiposikia basi kweli nitaamini ni CHURA KIZIWI kwelikweli. CHEZEA KATOLIKI WEWE....!!
 
Mungu awape pumziko la amani ndugu zetu ni vifo vinavyoleta simanzi kubwa,kila pando baya alilopanda mwanadamu Mungu atarudisha kwa watesi mara dufu ,kuvuna ulichopanda ni lazima hata maumivu ya watu hayaendi bure
 
Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Lindi, ameihimiza jamii kuomba huruma ya Mungu, kuliombea taifa na kuwaombea viongozi wa Serikali ili wawezeshe kupatikana kwa amani, haki, uhuru na ukweli katika jamii.

Askofu Pisa ameeleza hayo leo Oktoba 29, 2026 mkoani Lindi katika Adhimisho la Misa Takatifu ya kuwaombea watu walioumizwa, kupotea na kuuawa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

"Tuzidi kuomba huruma ya Mungu, tuliombee taifa letu, tuwaombee viongozi wote wa Serikali, ili Mungu bwana wetu aelekeze akili na mioyo yao kadiri ya mapenzi yake" amesema Askofu Pisa.

Amesisitiza kwamba ni muhimu kumilikiwa na ukweli, kuongozwa na ukweli hu, huku akikemea kuupotosha ukweli akisema kwamba ikiwa ukweli utapotoshwa bado utabaki kama ulivyo.
 
Wewe si ndio hata tarehe 29 October 2025 ulisema hizo ni taarabu tu. Siku ukiona hao bwana zako wanakimbia nchi tunaomba useme tena sio kweli hizo ni taarabu tu
Taarabu tu hio , kamtishe mama yako ..Mbona mmeshindwa kuiondoa serikali ? mnalialia nn?
 
Wewe si ndio hata tarehe 29 October 2025 ulisema hizo ni taarabu tu. Siku ukiona hao bwana zako wanakimbia nchi tunaomba useme tena sio kweli hizo ni taarabu tu
Polisi walikaa standby kuwashughulikia mbona hakuandamana tena ? mwaka jana TEC walikuwa na mdomo wa kuhamasisha vurugu leo wanatia huruma.
 
Hatujui miili iliyopotea ilizikwa wapi

"Tukasikia maiti zimepotea. Niliona wahusika wanazika nguo, viatu. Kuna mengi ambayo hatuyajui: miili iliyopotea ikapelekwa wapi? Wengine wanasema ikazikwa kwenye makaburi ya jumla. Hatujui wako wapi," Mama Lutgard Kagaruki akizungumzia kumbukumbu yake ya Oktoba 29.

Fuatilia kipindi kizima Youtube ya The Chanzo.
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ