Nimefika Kenya mara nyingi lakini ukiondoa Raisi wa Tanzania hakuna kiongozi wa Tanzania ambaye Mkenya wa kawaida anamfahamu achilia mbali hata kumsikia!
Lakini hapa Bongo tuko obsessed na Kenya, tunajua na kufuatilia kila kitu, mpaka tunachukuwa upande wa vyama vyao vya Kisiasa, Kenya wanaijua CCM tu lakini Tanzania tunajua na kufuatilitilia kila chama cha siasa cha Kenya na viongozi wake, hata hapa JF tumeweka jukwaa maalumu kwa ajili ya Kenya na wachangiaji wakubwa ni watanzania, Kenya hili lisingewezekana, kwanza Mkenya wa kawaida anamdharau Mtanzania!
Ujumbe wangu ni upi? Tunawababaikia wakenya tukubali au tukatae, hakuna Mkenya anayejua TV ya Tanzania lakini watanzania wote wanajua TV za Kenya!
Kuna Watanzania hata wanasoma Magazeti ya Kenya lakini hakuna gazeti la Tanzania linaloweza kuuzwa Kenya na kununuliwa.
Mfano hai Tundu Lisu kakimbizwa Kenya hakuna Mkenya ambaye angeweza kukimbizwa Tanzania, CHADEMA wako obsessed na Rais Uhuru Kenyatta na chama chake lakini nina uhakika wanachama wa chama cha Uhuru Kenya hawajawahi hata kuisikia CHADEMA, achilia mbali hata tu kujua kama kuna mtu anaitwa Mbowe!
Tundu Lissu kalazwa Kenya lakini hakuna hata high ranking official mmoja wa Chama cha Uhuru Kenya aliyefika kumuona, kwa kifupi wakenya don’t give a shit about you, acheni kujipendekeza....