Watanzania walalamikiwa Zambia kwa kufungua biashara nyingi kuliko wazawa

Watanzania walalamikiwa Zambia kwa kufungua biashara nyingi kuliko wazawa

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Hii sio habari njema sana. Watanzania wenzetu walioko Zambia hasa maeneo ya kaskazini wameanza kulalamikiwa kwa kufungua kwa wingi biashara mbalimbali hasa maduka. Wazawa wanaitupia lawama idara ya uhamiaji Zambia kwa kuruhusu uwepo wa wageni wengi hasa kutoka Tanzania wanaochukua nafasi za wenyeji.

Watanzania wamekuwa tishio kubwa kwenye miji ya Kasama, Nakonde, Mbala, Mpulungu, Isoka na Mpika. Hata miji mikubwa ya Lusaka, Kitwe na Ndola ina wafanyabiashara wengi wa kitanzania.

Binafsi nawapongeza watanzania hao ila ninawasihi wafuate sheria za nchi hiyo huku wakijiepusha na uhalifu. Pia idara ya uhamiaji Tanzania isiwe na urasimu wowote kwenye kutoa passport.

Screenshot_20250318-175505_Facebook.jpg
 
Naonaa trampu kafunguwa watu waafrika akiliii aloooo 😄 ss Kila mtu arudi kwao ,,,,na cc watz tuwatimue wanaozidi nchi kwetu haswaa wachinaa 🤔
 
Hii sio habari njema sana. Watanzania wenzetu walioko Zambia hasa maeneo ya kaskazini wameanza kulalamikiwa kwa kufungua kwa wingi biashara mbalimbali hasa maduka. Wazawa wanaitupia lawama idara ya uhamiaji Zambia kwa kuruhusu uwepo wa wageni wengi hasa kutoka Tanzania wanaochukua nafasi za wenyeji.

Watanzania wamekuwa tishio kubwa kwenye miji ya Kasama, Nakonde, Mbala, Mpulungu, Isoka na Mpika. Hata miji mikubwa ya Lusaka, Kitwe na Ndola ina wafanyabiashara wengi wa kitanzania.

Binafsi nawapongeza watanzania hao ila ninawasihi wafuate sheria za nchi hiyo huku wakijiepusha na uhalifu. Pia idara ya uhamiaji Tanzania isiwe na urasimu wowote kwenye kutoa passport.

View attachment 3276602
Umeleta hii habari ili kuwatetea wachina
 
Mnavyotaka kuwafanyia wachina wanaofanya shughuli zao kihalali nchini ndivyo hivyo mtafanyiwa nyie huko nje.
Alafu tunawachimba mkwara kwa bidhaa zinazotoka nchini mwao badala ya kupambana kama nchi kuzalisha bidhaa zetu.....eti wanafanya kazi ambazo zinatakiwa kufanywa na Watanzsnia huku bidhaa hizo ni made in China

Ingekuwa wameingia Lugodalutali huko au Kafunjo kununua mazao directly kwa wakulima wetu at least tungesema jambo lakini sio hili suala la uchuuzi ambazo watu wanaagiza china
 
Dunia ni kijiji huku Kariakoo Dar es Salaam wanalalamika kuwa wafanyabiashara toka China, na kule Zambia raia wanalalamikia wafanyabiashara toka Tanzania.

Somo suala hili halihitaji hasira wala mihemuko bali kwenda kimkakati.

Mfano Mamlaka ya Mapato Tanzania-,TRA walilalamika watanzania kutumia umoja wao kushindilia mizigo yao katika container la futi arobaini kwa jina moja la kampuni ya kiTanzania kuagiza mzigo kutoka China bila wafanyabiashara 40 n.k kuenda huko mmoja nmoja.

TRA walitakiwa kuelewa kuwa wafanyabiashara hao 40 kwa kutokwenda China wanaokoa dola kibao kama nauli ya ndege ya abiria, matumizi ya hoteli, mizunguko yote hii huko China ingebidi wafanyabisshara hao waondoke na fedha za ziada za dola za kimarekani.

TRA wangetambua ubunifu wa wafanyabiashara kuchangishana kuchangia makontena wanaokoa fedha za kigeni ziwe sarafu ya China au Marekani.

TRA na waziri wa biashara na BRELA wangewasaidia wafanyabiashara hao wabunifu wa Kariakoo kuendelea kuchangia kutumia makontaina na kubuni njia rafiki ya kukusanya kodi za mzigo wanaochangia ku import toka China, hii ingepelekea bidhaa kuwa bei ya chini na kuweza kushindana kibei na waChina wanaochangia uagizaji chini ya kampuni moja.

Watanzania hao wafanyabiashara wangesaidia kuongeza mitaji yao ktk kampuni moja ya kiTanzania kuwa kubwa ku import mzigo mkubwa kwa bei nafuu na kunufaisha wafanyabiashara wa kiTanzania na kuifanya Kariakoo kuwa kitovu / hub ya kibiashara eneo hili la Afrika ya Mashariki na nchi za Maziwa Makuu pia kusini mwa Afrika Zambia, Malawi, Zimbabwe.

Kikurupuka kufungia ubunifu wa watanzania wafanyabiashara kukunua mzigo mkubwa na kushirikiana kutumia makontena ilikuwa uamuzi wa kujiumiza wenyewe waTanzania .

Mfano kampuni ya waTanzania wenzetu Silent Ocean kupitia wafanyabishara kununua hisa na kusafirisha mizigo kwa umoja ingefanya Tanzania kuwa na kampuni kubwa ya Biashara ya Import na Export tajwa duniani, na kuweza kushindana kimataifa na kampuni za China n.k


View: https://m.youtube.com/watch?v=SrOkn2SBxhs

Watanzania tuache roho mbaya wananchi wanapokuwa wabunifu, pia TRA na wizara ya Biashara ziwe kwa ajili ya kuunga mkono ubunifu badala ya kuwa kikwazo. China wanasapoti makampuni na raia wao wabunifu.
 
Alafu tunawachimba mkwara kwa bidhaa zinazotoka nchini mwao badala ya kupambana kama nchi kuzalisha bidhaa zetu.....eti wanafanya kazi ambazo zinatakiwa kufanywa na Watanzsnia huku bidhaa hizo ni made in China

Ingekuwa wameingia Lugodalutali huko au Kafunjo kununua mazao directly kwa wakulima wetu at least tungesema jambo lakini sio hili suala la uchuuzi ambazo watu wanaagiza china

Wabongo wengi hawana exposure. Hizi kazi wanazofanya wachina nchini wabongo na waafrika kwa ujumla wanafanya huko Ulaya na Asia. Wewe pambana na soko sio na watu. Zalisha mali mwenyewe au weka bei rafiki, wanunuzi wengi wanawapenda wachina sababu wana bei nafuu.
 
Wazambia wanaweka profit kubwa kwenye biashara zao, sasa ndugu zangu wakinga anacheza na mzunguko (Pesa nyeupe) yeye akiweka faida elfu moja kwenye mzigo wa piece 7000 hana cha kupoteza..!!

Watanzania wanachokifanya Zambia ndio hiko wanachokifanya wachina kkoo..!!
 
Back
Top Bottom