Watanzania waliokwama Ukraine kusaidiwa kuondoka na Russia kutaichafua Sana nchi kipindi ambacho Russia inatengwa na Dunia

Ngoja tuwatie mods majaribuni eti Maxence Melo mnaonaje huu uzi unastahili kweli..?
Uzi unastahili kuwepo kwa sababu ni maoni yake binafsi mleta mada, lakini ni maoni ambayo watu wengi wameyakosoa.
Kukosolewa kwa mada hii sio tiketi ya mada kufutwa.


Hata hivyo mleta mada ajitathimini.
 
Hatuna uadui na Russia... Kwa hiyo ni sawa tu...
 
Akili yako fupi
 
Sijaongelea picha unayoiongelea wewe. Na kwa taarifa yako si warusi wote walikaa Gymkhana. Tanzania ni kubwa. Inakambi za jeshi kila kona. Na Tanzania tumekuwa na warusi wengi nchini katika mikoa mbalimbali. Na kuna wengine wanakuwepo kinamna.
Hapa siongelei hiyo picha unayoisema na siijui.

Kwa taarifa Samora alikuwepo nchini, kabla ya kuwa Rais. Aliishi na kufanya mafunzo Kongwa. Tembelea Kongwa Sekondari utakuta handaki alilokuwa akikaa wakati wa mafunzo. Na kuna uwanja wa ndege walio utumia. Hapa warusi waliwapa Mafunzo. Ile sekondari ya Kongwa majengo mengi yalikuwa yaliyotumika na wapigania ukombozi wa Msumbiji. Warusi waliishi hapo. Na nilifanikiwa kukaa ktk moja ya nyumba zao miaka kadhaa ilopita.

Alipokuwa Rais 1975, baadae mwaka 1982 Samora alifanya ziara ya kiserikali chini Tanzania, hii ilikuwa ziara yake ya kwanza kama Rais, na baadae alielekea Musoma wakiambatana na Mwl. Nyerere alie kuwa Rais wa Tanzania. Nakumbuka wimbo wa "Samora Machel mamaaa...eeeh! Viva viva FRELIMO Msumbiji mamaa" Samora alikaa siku tatu Musoma na kugeuza, akiwa na mke wake Graca. Alifanya utani kuwa atalala na Nyerere kitanda kimoja kwani ni marafiki sana.

Wimbo mwingine ulioimbwa kipindi hicho ni "FRELIMO haina mwisho, haina mwisho FRELIMO haina mwisho... Ujamaa hauna mwisho, hauna mwisho ujamaa hauna mwisho..." na mmoja ulikuwa wa kireno nimeusahau kidogo. Hii ilikuwa ni mwaka 1982.

"Itewana Samora zoana, inataka kumozambique, FRELIMO Ooohoho...FRELIMO...Ooohoho...Zoana..Inataka kumozambique...Mondrane kupela vema zoana inataka kumzambique...FRELIMO...ooohoho....FRELIMO....oooohoho Zoana ....ine kupele zena zowana....."

Huu ni moja ya nyimbo tulizomwimbia Samora. Na ziliendelea kuimbwa mashuleni.
 
Nadhani hujui historia ya Tanzania na Urusi
Haijalishi, kwa kipindi hiki walichagua kuwa nyutro wangebaki hivyo hivyo.
Tunashindwaje kusaidia watu wetu hadi tuombe nchi iliyo na mgogoro?
 
Nashukuru kwa kumbukumbu nzuri za miaka ile. Samora pia alifanya ziara ya kiserikali na Graca mwaka 1984 nakumbuka kulikuwa na tukio fulani mwaka ule lilifanyika pale mnazi mmoja, yeye na Nyerere walikuwepo.
 
Yaan unafikiria mikopo ya wazungu kuliko vijana wetu.Aidha inaonekana haujui ,Mambo ya kimataifa yalivyo.Kwa kukusaidia tu,ikitokea vita raia huwa wanapewa misaada na kuepushwa na mapigano.Wanaotafutwa kuuliwa Ni wanajeshi.Sijui ulitaka vijana wetu wafe?Sikuelewi.
 
Non alingment feki-ukweli wa mambo nchi na sera ya kutofungamana na upande wowote zimeegemea urusi na uchina zaidi. Tuache unafiki.
 
Nimeshangaa sana kwa uzi wako huu.Kipaumbele cha kwanza kwa nchi yoyote makini ni kuokoa maisha ya raia wake. Hiki ndicho Tanzania inayofanya na nawapongeza sana. Wewe unataka watoto wetu wafe eti tu tunafuata mkumbo wa West. Una shida.
 
Kwa hiyo we ulitaka wakwame kisa wanasaidiwa na Russia!?
 
hivi huyu mleta mada hii ni kweli alikaa na kutafakari alichokisema hapa jamani? Hivi kweli huyu ndugu kama yeye angelikuwepo ukraine wakati huu angelichagua ni nani anamtoa katika eneo la kivita au angeliharakisha kuokoa roho yake? Hivi kweli kama ingelikuwa kati ya waliokwama huko ukraine yumo ndugu y ake au jamaa yake, angelimshauri kukataa msaada wa kuondoshwa na warusi? Hivi huyu ndugu ameona clips zinazozagaa mitandaoni ambazo zinaonyesha askari wa ukraine (anaita wenyeji wa wanafunzi) wakiwatowa wanafunzi wa kiafrika na jamaika katika mabasi na matreni yanayowaondoa watu katika sehemu za vita? Ni kwa nini ukatae msaada wa warusi ilhali ukraine ambao ni wenyeji wako wanakataa kukusaidia?

Hivi huyu ndugu anaposema kuwa Russia haijawahi kusaidia masikini, anajua lolote juu ya historia ya russia na misaada na mafunzo waliotowa kwa wapigania uhuru wa afrika wakati afrika ikipigania kujikomboa? Labda ndugu yetu hajui ni kwa nini nchi nyingi za afrika zilikataa kupiga kura katika azimio la UN juu ya ukraine.
 
Russia hakuitawala Africa sio kwa kupenda. Kwanza haikuwepo Urusi Kama Urusi. Na nchi zilizokuwepo maeneo hayo miaka ya 1800 zilikuwa dhaifu Sana. Zilizopigana Mara kwa mara na zisizoweza kutoka nje kuja Afrika kutawala.

Kumbuka ata Marekani haikuitawala Africa.
Sawa na Italy iliambulia eritria tu baada ya kuchelewa kwake.

So Urusi haikuja kuikomboa Afrika Bali kupigania maslahi yake dhidi ya mabepari Afrika. Na imehusika na kuwa karibu na madikteta na tawala za kijeshi akiwa ndio muuzaji mkuu wa slaa kwa Afrika kwa Sasa.
 
Waafrika tunalawama Sana hujui tu. Katika vita hutakiwa kuanza kuondolewa wazee, watoto na wanawake. Ila tulichotaka wageni huko NI kuondolewa wageni kwanza eti huku sio kwetu.
Ukrane inawageni wengi mno. Karibu milion 2.
Na utaratibu wa kuwatoa kwanza wazee, watoto na mama zao na Kisha wanawake ulikuwa sahihi. Na kuweka uwiano wa wageni na wenyeji.
 
Akili yako fupi sana.......
labda nikusaidie kidogo sehemu yyte ambayo amani yake imeharibika kitu cha kwanza ni safety, ww umekaa huko nyumbani kwako na mkeo unathubutu kuwaambia watz waliopo uwanja wa vita eti wachague nani awaokoe!
pumbavu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…