Watanzania waliokwama Ukraine kusaidiwa kuondoka na Russia kutaichafua Sana nchi kipindi ambacho Russia inatengwa na Dunia

Watanzania waliokwama Ukraine kusaidiwa kuondoka na Russia kutaichafua Sana nchi kipindi ambacho Russia inatengwa na Dunia

Wewe unaongea kwa hisia tuliza moyo then tumia akili sio moyo.

Unavyoongea ivyo unathihirisha ni namna gani bado hujajua washirika wa nchi yetu mpaka sasa na hufahamu kiundani historia kati yetu Tanzania na Russia tafadhali fanya research juu ya siasa za kimataifa hasa kati ya Tanzania na nchi za kibepari na ujamaa utapata jibu.

Kingine tuseme India ambao nao ni kati ya superpowers duniani pia ni wajinga kwakuwa raia wake wanaondolewa kwa wa Nazi Ukraine nao ni wajinga. Na kwa taarifa yako Russia inasaidia kuondoa raia wa India na Tanzania na wanchi zingine pale Ukraine japo pia bado kuna raia wa nchi zingine wameshikwa kama mateka na wanajeshi wa ki-nazi Ukraine na Urusi ndo taifa pekee lililojitolea kusaidia raia on battle ground.

Najua ww ni shabiki wa wa Nazi wa Ukraine ndo maana Ila pole kama kichapo wacha mtembezewe tu na uyo mnafiki Zelensky ambae ni puppet wa NATO na USA. Hayo yote yasingetokea kama Zelensky asingekuwa anauwa watu wanaompiga kwenye majimbo huru kwa miaka 10 na likifumbiwa macho. Isitoshe iyo sio vita ni Operation ya Kijeshi kama zingine tu za Libya na Iraq na Afghanistan. Tena wapigwe sana tu zaidi ya Libya na wakifanikiwa kumkamata Zelensky ndo kabsaa wengine tutasherekea
Unajua Nazi NI ant wayaudi. Unazi na uyaudi auingiliani ata robo. Na Raisi wa Ukrane NI myaudi ujue.
Usimeze probaganda broo. Mwaka 1989 Russia iliivamia Afiganstan kuondoa makundi ya kigaidi dunia ilikuwa upande wake. Ila ili NI Sanaa tupu
 
Nashukuru kwa kumbukumbu nzuri za miaka ile. Samora pia alifanya ziara ya kiserikali na Graca mwaka 1984 nakumbuka kulikuwa na tukio fulani mwaka ule lilifanyika pale mnazi mmoja, yeye na Nyerere walikuwepo.
Sisi tulimpokea Graca pale Iringa alikuja kutembelea chuo cha Kleruu!
 
Inaonesha hujui historia ya Russia na Tanzania. Unafuata mkumbo tu ati kisa dunia imeitenga Russia. Kwani ni Tanzania tu ambayo haikupiga kura. Sasa kuna nchi ambazo zimepiga kula ya kutokukubaliana na maazimio ya UN dhidi ya Russia.

Unajua kwanini Russia kaivamia Ukraine? Unahitaji kujua jambo kabla ya kutoa maoni yako. Eti Russia haijawai kuisaidia Tanzania? Ha ha ha! Unajua Russia haikuwai kuitawala Africa, bali ilikuwa mbele kusaidia ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Ndo maana hata huyu Puttin kaishi Tanzania. Russia ilikuwa na chuo cha Lumumba ambako wanadiplomasia na wanasiasa wengi wa Afrika wamesoma huko. Wewe unafuata propaganda za Kimarekani na kuamini kila kitu.

Hata wakati wa vita ya Uganda, tulisaidiwa sana vifaa na Russia, japo Marekani na mataifa mengine kama Uingereza walikaa kimya. Russia imeleta wataalamu wengi wa kilimo, na nyanja kadhaa nchini, Pia wataalamu wetu wengi katika fani tofauti wamesomea Russia. Haya yote ni mahusiano tuliokuwa nayo.

Mwl. Nyerere ni kiongozi mmoja wapo wa waanzilishi wa nchi zisizo fungamana na upande wowote toka tumepata uhuru. Tanzania tunafahamika hivyo, na tumekuwa hivyo miaka yote. Hatuna adui!
Mwambie hata chuo cha MUST [mbeya university of science and technology] kimejengwa na warusi. Tatizo watoto wengi hawataki kujifunza.
 
Russia hakuitawala Africa sio kwa kupenda. Kwanza haikuwepo Urusi Kama Urusi. Na nchi zilizokuwepo maeneo hayo miaka ya 1800 zilikuwa dhaifu Sana. Zilizopigana Mara kwa mara na zisizoweza kutoka nje kuja Afrika kutawala.

Kumbuka ata Marekani haikuitawala Africa.
Sawa na Italy iliambulia eritria tu baada ya kuchelewa kwake.

So Urusi haikuja kuikomboa Afrika Bali kupigania maslahi yake dhidi ya mabepari Afrika. Na imehusika na kuwa karibu na madikteta na tawala za kijeshi akiwa ndio muuzaji mkuu wa slaa kwa Afrika kwa Sasa.
Eti imehusika kuwa karibu na madikteta na tawala za kijeshi. Watu wanapolishwa maneno na watu wa magharibi. Ebu taja hao madikteta na tawala za kijeshi Africa ambazo Russia au Urusi amekuwa nazo karibu. Ingekuwa hivyo Urusi ingekuwa karibu na Dictotor Idd Amin Dada, cha ajabu Urusi ilisaidia Tanzania.
Marekani haikuitawala Africa lakini imekuwa chanzo cha migogoro na kuiba rasilimali za Africa ikishirikiana na wadau wake. Kwanini Marekani haimalizi migogoro ya DRC? Kwa nini marekani iliunga mkono Serikali ya kibaguzi dhidi ya Waafrika?
Unahitaji kujua baada ya ukoloni wa kuitawala Africa physical kuondolewa mbinu nyingine ilikuwa ni ukoloni mamboleo ambau umeendelea kutumika na mataifa makubwa hasa Marekani. Na huu ukoloni ni mbaya kuliko ule wa mwanzo.

nikujulishe tu, Italy iliitawala Ethiopia kwa almost miaka isiyopungua sita. Na waliimarisha miundo mbinu mingi tu kama reli, viwanja vya ndege, barabara, kuna majengo mengi hadi leo ya waitalia. Mpaka walipokuja kushindwa vita na kuondoka. Japo nashangaa Ethiopia wanapenda kusema kuwa hawajatawaliwa. Wakati Italia ilikaa na wakawa na mamlaka kamili. Baada ya waitalia kuondolewa, Ethiopia ilikuwa under British protectorate, na wakati huo Mfalme Haile selaise alikuwa wingereza alikoenda kuomba msaada wa kuondoa wa Italia.

Waethiopia usheherekea hiyo siku kila mwaka walivyojikomboa, na imefanyika tu wiki iliyopita. Cha hajabu wanajisifia hawajatawaliwa! Mie uwa nawaeleza nchi ambayo haikutawaliwa pekee ni Liberia. Cha ajabu wanadai ni wao tu hawakutawaliwa, huu ni uongo. Muitali kaja kaa kaimarisha utawala, utadai hajakutawala? Wanadai kulikuwa na resistance hivi ni nchi gani Africa haikuwa na resistance?

Hii uwa naifananisha na Zanzibar kudai mapinduzi yaliongozwa na Abeid Amani karume, na kutomtambua John Okero. Ukweli na historia kupindishwa.

Ok, Marekani ndiyo aneongoza kwa mikakati ya kimapinduzi katika nchi kadhaa Africa, wakishirikiana na Ufaransa wala si Rassia. Marekani ukienda kinyume na maslahi yake anakuita dicteta mara hakuna demokrasia, mfano walivyomgeuka Mugabe kisa kurejesha ardhi kwa weusi.

Urusi ilipigania ukombozi wa nchi mbalimbali Africa, na hasa Africa ya kusini ikipinga ubaguzi. Kumbuka Marekani ilikuwa side ya Makaburu. Sasa ni wapi Urusi imetetea madikiteta ebu wataje? Urusi ilikuwa against kinachofanyika DRC, wakati marekani wakimuweka dikteta Mabutu Seseseko wakishirikiana na wabeligiji.

Urusi ililaani kuuwawa kwa Gadaffi, japo Gadaffi alikuwa mshirika wa Marekani toka miaka na miaka. Hakuwa mshirika wa Urusi. Marekani ikamgeuka Gadaffi kwa maslahi yao.

Umesikia wapi Urusi au Russia imeingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine kama si Marekani. Chukua muda utafakari. Vyombo vinavyotumika kunyonya nchi zinazoendelea viko chini ya nani kama si Marekani? IMF na World Bank? Tafakari?
 
Sijui Diplomasia ya Tanzania ikoje. Jambazi anavamia sehemu. Alafu unaruhusu akuondoe wewe ni kuonesha taifa halijui Nini Cha kufanya wakati gani.
Kipindi ambacho Tawala za Afrika zenye democracy uchwara, Ubabe na uonevu mkubwa kwa wakosoaji wa viongozi zikijizuia kulaani uvamizi. NI ishara kuwa udkkteta duniani unasimikwa na Tawala Hilo.
Kipindi hichi ambacho mwenyeji wako anapigwa na adui unakubali vipi adui akusaidie kutoka kwa mwenyeji na kukusafirisha?
Ivi vita ikiisha Leo Kuna watanzania watapokelewa Ukrane kweli. Hilo sio sawa kabisa.

Kama Urusi inalinda udkkteta duniani Basi lazima tukubali tu kumtenga kwa Sasa.

Baada ya vita uchumi wake utaumia na watakuwa bize kuujenga Tena chini ya vikwazo na madeni kibao.

Russia haijawahi kusaidia masikini wananchi vitu vya msingi zaidi ya kusaidia madikteta kutawala na baadae kuleta machafuko.

Nashauri tujitenge na Russia mapema tusikose mema ya duniani. Yasitukute ya 1984. Tunaimba ujamaa tunapigwa njaa tunaenda kupigia magoti Mabepari yanatupa mahindi kulisha watu wetu.
Ukraine ilishaonywa na Russia kuwa akianza kuweka vituo vya NATO Ukraine ataipata fresh akadhania Putin anatania, isitoshe USA na NATO wakaamuahidi kuwa vita vikitokea watamsaidia. Sasa Putin amefanya kweli wameufyata, Zelensky amebaki kama mkiwa analialia tu wakati huo huo biashara ya mafuta kati ya Urusi na Marekani inaendelea.
You cannot choose your neighbors, just learn to live together and if you choose friends, choose wisely.
 
Back
Top Bottom