Watanzania walivyo wanafiki, makelele ya Palestina ilhali wana uswahiba na mkoloni Morocco

Watanzania walivyo wanafiki, makelele ya Palestina ilhali wana uswahiba na mkoloni Morocco

Wakristo baadhi huhalalisha dhulma ya Israel dhidi ya wapalestina wakihisi wanamfurahisha Yesu. Hata mngemuwekea Yesu kiwanja yerusalem akija hatakijenga maana hapendi dhulma

Weee bana udini huu sasa, kwani Waisraeli ni Wakristo?
Ugomvi wa Waisraeli na Wapalestina haujaanza leo, sasa wewe Mswahili na kimbelembele chako na njaa unafikiria utatatua?
Hapo Zenji umetatua?
 
Merry Christmass wakuu. Mkiendelea kulumbana za Ke vs. Tz kwa moyo wa krismsasi msije mkasahau kuonyesha upendo kwa jirani zenu.
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Linapokuja swala la mahusiano ya kimataifa Kenya wanakamata nafasi chini ya sifuri . Naomba tu muwaachie matatizo yao ya kikabila yanawatosha kuwapa stress . Sisi tupambane tu kujiondoa kwenye umasikini .
 
Pwani wapi na wapi.... vipi Moshi.
Mbege huwa naskia sifa zake, ni kukaa mbali nayo.
Mbege haina lolote la kutisha, Alooh Sijapanda kask ....nmeshakula likizo zangu zote apa sina ujanja..Vp apo 254 Mmeshaua viumbe hai wangap [emoji23][emoji23]Najua Leo kuku, mbuzi,ng'ombe wengi watapoteza Maisha
 
Hehehe Merry Christmas
Unakunywa mbege wapi nije.
Hahaa mbege nenda rombo, wakenya leo hadi mwakani wamejaa huko , maeneo ya tarakea hadi himo hapatoshi leo mazee....yaani mnapiga mdudu aka kiti moto alafu mbege kwa sana...wachagga tunawapenda sana[emoji3] [emoji119]
 
Baada ya tukio la juzi kwa Kenya kutokuhusika kwenye upigaji wa kura kwenye mswada wa Umoja wa Mataifa kuhusu uamuzi wa Marekani kwamba Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel, Watanzania wametokwa povu la omo huku wakishutumu Kenya, wengine wanakesha JF kabisa kwa ajili ya hili hadi nawaza hivi jameni watu huwa hawana muda wa mapumziko, hata muda wa kwenda kula, hata kama mnalipwa.

Sasa hawa hawa Watanzania kwa jinsi walivyo wanafiki, juzi wamemkenulia meno na kumpokea mfalme wa Morocco baada ya kuja kwao na kuwaahidi kuwajengea uwanja wa mpira na misikiti na vipochopocho vyote (hivi ahadi zake hizo alitekeleza? Au ndio yale yale). Huyu mfalme huko kwake ni mkoloni ambaye amelikalia taifa la Western Sahara kibabe, taifa hili limetambuliwa hadi na UN.

Leo mnajifanya kuwapigia Wakenya makelele kuhusu Wapalestina (ambao mgogoro wao na Israel wanaujua wenyewe maana hauishangi tumeuskia tangu tukiwa watoto) na hapa Afrika mnamuunga mkono na kumshobokea mkoloni Mwafrika anayelikoloni taifa la Kiafrika tena anatumia ubabe. Yaani bila hata aibu mnadhihirisha unafiki wa kiajabu.
hongera
tanzania ni nchi huru yenye maamuzi kamili,hatupaswi kuchaguliwa rafiki wala ADUI,hatupaswi kufuata mkumbo.
la mwisho siasa haina adui wala rafiki wa kudumu.kwa maslahi yetu tumeamua hivyo,bora kufanya mtihani ukafeli kuliko kukimbia mtihani
 
Mbege haina lolote la kutisha, Alooh Sijapanda kask ....nmeshakula likizo zangu zote apa sina ujanja..Vp apo 254 Mmeshaua viumbe hai wangap [emoji23][emoji23]Najua Leo kuku, mbuzi,ng'ombe wengi watapoteza Maisha

Dah kuna jamaa alinisimulia masaibu ya mbege ikabidi nikae mbali nayo, kipindi hicho nilikua mtu wa makonyagi. Kwamba ukinywa mbege kwa sana inabidi kuwa makini kwenye suruali maana hali itabadilika humo...hehehe
Pole aisei, hivyo haupo likizo yaani unaona watu wakijiachia.

Kwetu kijijini (come together ya relatives), mbuzi keshapigwa chini kwa kisu, chupa za beer zinagongana na kutoa milio utadhani ndio mara ya kwanza wanaume kuona Guineas.
 
Hahaa mbege nenda rombo, wakenya leo hadi mwakani wamejaa huko , maeneo ya tarakea hadi himo hapatoshi leo mazee....yaani mnapiga mdudu aka kiti moto alafu mbege kwa sana...wachagga tunawapenda sana[emoji3] [emoji119]

Hehehehe!! Wachagga wote wametoweka Nairobi, lakini hivi kweli hata kwa sie, anayebaki jiji la Nairobi atakua pimbi.... Labda kama kazi itabana.
 
Dah kuna jamaa alinisimulia masaibu ya mbege ikabidi nikae mbali nayo, kipindi hicho nilikua mtu wa makonyagi. Kwamba ukinywa mbege kwa sana inabidi kuwa makini kwenye suruali maana hali itabadilika humo...hehehe
Pole aisei, hivyo haupo likizo yaani unaona watu wakijiachia.

Kwetu kijijini (come together ya relatives), mbuzi keshapigwa chini kwa kisu, chupa za beer zinagongana na kutoa milio utadhani ndio mara ya kwanza wanaume kuona Guineas.
HaHaha Mk nawe humo. ...Leo nyama zitaliwa sana...Wacha watu wajilambe kwakwel...
 
wakenya mmeniangusha sana kwa kitendo cha kukimbia kupiga kura.mnaogopa nini kujulikana msimamo wenu?
 
Kwa hili nipo pamoja na Serikal yetu ya Tanzania sio kwa kukataa Jerusalem kuwa Mji Mkuu wa Isarel Bali kwa kupiga kura iwe kukubali au kukataa, Mataifa yaliyoamua kutopiga kura kabisa yameonesha hayajiamini kabisa!
Ambao hawajapiga kura wanatekeleza kwa vitendo ile inayoitwa Diplomasi ya Uchumi.Kwenye kila jambo unaangalia linakunufaisha vip wewe kama nchi?

Kwa kufanya hivi, hawajaaribu urafiki kwa Waarabu na hawajaaribu kwa Israel na Marekani. Big up kwa majirani zetu Kenya, Uganda, Rwanda na Zambia kwa hilo, ndio utekelezaji wa vitendo wa diplomasia ya uchumi.

Mwaka jana Kenya ilikuwa nchi ya tano kwa kupewa msaada mkubwa na Marekani, waharibu hiyo kwa ajili ya Palestina?ingekuwa kosa kubwa. Mapema mwezi ujao Marekani itakuwa na kikao cha pamoja na marafiki zake hawa ambao hawakunga mkono hoja ile.

Yawezekana hatujui tunataka nini, ni wakati sasa tuangalie maslahi yetu na kutoingilia magomvi yasiyotuhusu.
 
Nimeuliza hili swali, kwani ilikua shuruti, ilikua lazima?? Tupige kura kuwafurahisha nyie?
Morocco inatuhusu maana amekalia taifa la Kiafrika wakati nyie mnamlambalamba na kupeleka kiherehere kwa Wapalestina na Waisraeli.
Onyesha ukomavu wako nyumbani Afrika kabla ya kujifanya mtetezi wa nchi za mbali, sio huu unafiki wa kwenda kucheka cheka kule ilhali hapa Afrika unafumba macho.
Vipi mfalme aliwajengea msikiti au kawatapeli...
Hata wewe mnafiki, Unapiga kelele Morocco ilioko ukooooooo mbali kabisa, wakati pembeni yako kuna Visiwa vya Unguja na pemba vimekaliwa na mabavu na mkoloni mweusi mwengine. Morocco inakuhusu nini wakati Zanzibar upo nayo jirani unafumbia macho?
 
Wakristo baadhi huhalalisha dhulma ya Israel dhidi ya wapalestina wakihisi wanamfurahisha Yesu. Hata mngemuwekea Yesu kiwanja yerusalem akija hatakijenga maana hapendi dhulma

wengi wao hawajui ya kuwa hao hao ndiyo waliomkana Yesu, hatimaye wakamuua. wale hawana utukufu wowote ni wazushi tu.
 
Hizi ni akili za kuku, mlikuwa wapi wakati wareno na makaburu wanawatesawaafrika huko kusini mwa Afrika?, si mlikua na wazungu wanawanyonya ndimi, kitu gani Kenya imeifanyia Africa, hata huko Morroco Kenya imefanya nini kuisaidia west Sahara?. Ubaguzi wenu umevuka mipaka, kwasababu Palestinians sio waafrika kwahiyo hawastahili kusaidiwa na nchi za Africa?, ninyi mliposaidiwa chakula na China kwani China ipo Africa?..Akili za kuku zilizojaa ubaguzi wa kikabila.
Wewe matusi tuuu ndio unajua hapa JF.
 
Back
Top Bottom