Hapo ndipo unapoanza kujichanganya, kumbuka lengo la OAU kuwaruhusu West Sahara kuwa mwanachama wa OAU ni pamoja na kuweza kuwaleta pamoja wote wakiwa ndani ya vikao vya OAU ili wasikilizwe hoja zao, ilikuwa vigumu sana kwa West Sahara kusikika wakiwa nje ya vikao vya OAU, kitendo cha Morocco kujitoa kilirudisha nyuma sana hizi juhudi za mazungumzo kwa sababu Morocco haikuwa na wawakilishi ndani ya vikao vya OAU, hivyo kuifanya AU kukosa haki kisheria na uhalali wa kusuluhisha mgogoro huu, kwasababu moja kati ya nchi zinazo zozana sio mwanachama wa OAU/AU.
Kitendo cha Morocco kuomba uanachama AU ni kuirudishie tena uwezo wa kisheria AU kuendelea na mazungumzo ya upatanishi, sio jambo la kupingwa na kuikatalia uanachama, hatujafikia hatua za kuilazimisha Morocco, wakati huo haujafika, kumbuka Morocco ilikubaliana na mapendekezo mengi tu kabla haijajitoa, ikiwa ni pamoja na kuipa West Sahara mamlaka yake ya ndani ya kujitawala, kwahiyo nafasi ya mazungumzo bado ipo hivyo ni bora Morocco irudi ili mazungumzo yaendelee.