Watanzania walivyo wanafiki, makelele ya Palestina ilhali wana uswahiba na mkoloni Morocco

Sina uhakika kama unatatizo la kuelewa lugha au uwezo wako wa kuelewa mambo ndiyo shida, nimekuambia Tanzania msimamo wetu tangu enzi za Nyerere katika swala la Morocco vs West Sahara ni kwamba nchi zote hizi mbili zitambulike na zipewe uanachama OAU ili mazungumzo ya kufikia uhuru kamili wa west Sahara yaweze kufanyika, hatukufikia katika hatua ya kuwatenga na kuifukuza Morocco, huo ndiyo uliokuwa msimamo wa Africa na Tanzania, huu unaousema wewe haujawahi kuwa msimamo wa Tanzania hata siku moja, ni msimamo wa hizo nchi ulizozitaja(kama ni kweli huo ndiyo msimamo wao), pia ndiyo msimamo wako wewe binafsi.
Mwenzetu anataka kulazimisha mawazo yake binafsi yawe eti ni sera ya Tanzania. Ukimuuliza lini Tanzania imekataa kutambulika kwa morocco, hana majibu. Nimemuuliza unajua Dar es salaam kuna mtaa unaitwa Morocco je, anajua chanzo cha mtaa huo ni nini?
 
Misingi yao ya ukabila na rushwa imewafanya wawe vipofu na ukweli, ukiwa na rafiki akikosea sema, siyo kukaa kimya na kuwa naye bega kwa bega akikupa rushwa (viwanda 2000)..
 
Mwenzetu anataka kulazimisha mawazo yake binafsi yawe eti ni sera ya Tanzania. Ukimuuliza lini Tanzania imekataa kutambulika kwa morocco, hana majibu. Nimemuuliza unajua Dar es salaam kuna mtaa unaitwa Morocco je, anajua chanzo cha mtaa huo ni nini?
Morocco miaka yote imekua ikishiriki katika michezo yote ya Africa, na pia imeandaa michezo kadhaa ya nchi za kiafrika na hakuna nchi iliyokataa kwenda kushiriki, lini Morocco ilitengwa na Africa, ninahakika hata historia haijui vizuri iliyosababisha Morocco kusitisha uanachama wake wa OAU, ila twende naye mdogo mdogo.
 
Sina uhakika kama unatatizo la kuelewa lugha au uwezo wako wa kuelewa mambo ndiyo shida, nimekuambia Tanzania msimamo wetu tangu enzi za Nyerere katika swala la Morocco vs West Sahara ni kwamba nchi zote hizi mbili zitambulike na zipewe uanachama OAU ili mazungumzo ya kufikia uhuru kamili wa west Sahara yaweze kufanyika, hatukufikia katika hatua ya kuwatenga na kuifukuza Morocco, huo ndiyo uliokuwa msimamo wa Africa na Tanzania, huu unaousema wewe haujawahi kuwa msimamo wa Tanzania hata siku moja, ni msimamo wa hizo nchi ulizozitaja(kama ni kweli huo ndiyo msimamo wao), pia ndiyo msimamo wako wewe binafsi.

..Morocco waliondoka OAU wakipinga uanachama wa Sahara Magharibi.

..sasa kuna tatizo ktk msimamo wetu wa kuwarudishia Morocco uanachama huku wakiwa bado wameshikilia msimamo wao kuhusu Sahara Magharibi.

..hata juhudi za kuwakutanisha Sahara Magharibi na Morocco ktk vikao vya AU zimekuwa zikikwamishwa/zikisusiwa na Morocco.

..kwa hiyo utaona kwamba Tanzania tulifanya makosa kupiga kura Morocco warejeshwe AU bila kuwalazimisha kwanza waache kuikalia kimabavu Sahara Magharibi.
 
Je, ni nchi ngapi zilipiga kura kuwaruhusu Morocco warudi Au?
 
Sema baadhi ya Watanzania. Watanzania tunaojitambua hatuungi mkono huo upuuzi wala ule upuuzi mwingine wa kuhamisha mji mkuu wa Wayahudi.
Vichadema kila kitu ni kugeuka geuka tu.Hii mi watu inakera
 
..Morocco waliondoka OAU wakipinga uanachama wa Sahara Magharibi.

..sasa kuna tatizo ktk msimamo wetu wa kuwarudishia Morocco uanachama huku wakiwa bado wameshikilia msimamo wao kuhusu Sahara Magharibi.

..hata juhudi za kuwakutanisha Sahara Magharibi na Morocco ktk vikao vya AU zimekuwa zikikwamishwa/zikisusiwa na Morocco.

..kwa hiyo utaona kwamba Tanzania tulifanya makosa kupiga kura Morocco warejeshwe AU bila kuwalazimisha kwanza waache kuikalia kimabavu Sahara Magharibi.
Hapo ndipo unapoanza kujichanganya, kumbuka lengo la OAU kuwaruhusu West Sahara kuwa mwanachama wa OAU ni pamoja na kuweza kuwaleta pamoja wote wakiwa ndani ya vikao vya OAU ili wasikilizwe hoja zao, ilikuwa vigumu sana kwa West Sahara kusikika wakiwa nje ya vikao vya OAU, kitendo cha Morocco kujitoa kilirudisha nyuma sana hizi juhudi za mazungumzo kwa sababu Morocco haikuwa na wawakilishi ndani ya vikao vya OAU, hivyo kuifanya AU kukosa haki kisheria na uhalali wa kusuluhisha mgogoro huu, kwasababu moja kati ya nchi zinazo zozana sio mwanachama wa OAU/AU.

Kitendo cha Morocco kuomba uanachama AU ni kuirudishie tena uwezo wa kisheria AU kuendelea na mazungumzo ya upatanishi, sio jambo la kupingwa na kuikatalia uanachama, hatujafikia hatua za kuilazimisha Morocco, wakati huo haujafika, kumbuka Morocco ilikubaliana na mapendekezo mengi tu kabla haijajitoa, ikiwa ni pamoja na kuipa West Sahara mamlaka yake ya ndani ya kujitawala, kwahiyo nafasi ya mazungumzo bado ipo hivyo ni bora Morocco irudi ili mazungumzo yaendelee.
 
Siasa za kimataifa zinamambo yake ndugu yangu. Na kila nchi inastarategies zake. Nakushangaa sana kusema nchi yetu imekuwa ombaomba. Sitaki kuomgelea suala la Ethiopia kuhusu kutusaidia masuala ya kitaalamu kuhusu umeme, japo Ethiopia wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika jambo hili la umeme na usafiri wa anga. Kwangu mimi sioni kama ni tatizo kupata wataalamu waafrika wenzetu ili tusaidiane.

..wa-Tz tuna tabia ya kujidharau.

..Hale[1964],Kidatu[1976],Mtera[1979], Kihansi[2000]...tunapaswa kubadilishana uzoefu na Ethiopia na siyo kuwa omba-omba kwao.

..pia zile habari kwamba Ethiopia itakuwa inapitisha mizigo yake bandari ya Dsm unaziamini?

..kwa ujuzi wako wa jiografia na kuzingatia ujenzi wa reli ya Addis to Djibouti unaamini kwamba Ethiopia watatumia bandari ya Dsm?

cc BAK, MK254
 
Hapo ndipo unapoanza kujichanganya, kumbuka lengo la OAU kuwaruhusu West Sahara kuwa mwanachama wa OAU ni pamoja na kuweza kuwaleta pamoja wote wakiwa ndani ya vikao vya OAU ili wasikilizwe hoja zao, ilikuwa vigumu sana kwa West Sahara kusikika wakiwa nje ya vikao vya OAU, kitendo cha Morocco kujitoa kilirudisha nyuma sana hizi juhudi za mazungumzo kwa sababu Morocco haikuwa na wawakilishi ndani ya vikao vya OAU, hivyo kuifanya AU kukosa haki kisheria na uhalali wa kusuluhisha mgogoro huu, kwasababu moja kati ya nchi zinazo zozana sio mwanachama wa OAU/AU.

Kitendo cha Morocco kuomba uanachama AU ni kuirudishie tena uwezo wa kisheria AU kuendelea na mazungumzo ya upatanishi, sio jambo la kupingwa na kuikatalia uanachama, hatujafikia hatua za kuilazimisha Morocco, wakati huo haujafika, kumbuka Morocco ilikubaliana na mapendekezo mengi tu kabla haijajitoa, ikiwa ni pamoja na kuipa West Sahara mamlaka yake ya ndani ya kujitawala, kwahiyo nafasi ya mazungumzo bado ipo hivyo ni bora Morocco irudi ili mazungumzo yaendelee.

..siyo kweli.

..Morocco walibembelezwa sana waruhusu wananchi wa Sahara Magharibi wapige kura ya maoni.

..uamuzi wa kuwapa Sahara Magharibi uanachama wa OAU ulikuwa ukiahirishwa ikitarajiwa kwamba Morocco watalegeza msimamo wao na kuruhusu kura ya maoni.

..baadaye OAU ililazimika kuipa uanachama Sahara Magharibi na Polisario walikalia kiti chao nadhani ktk mkutano ambao Mwalimu Nyerere alikuwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti. siku hiyo Morocco wakatimka OAU na wakipinga uanachama wa Sahara Magharibi.

..Kwa hiyo ni kweli Morocco hawakufukuzwa OAU, walijitoa wenyewe. Lakini wapo wengi wanaoamini kwamba yalifanyika makosa kuwarudisha Morocco ktk AU huku wakiwa hawajabadilisha msimamo wao kuhusu Sahara Magharibi.

..Zaidi, tangu wamerudishwa AU, Morocco wameendelea kugomea juhudi za usuluhishi za AU kuhusu mgogoro baina yao na Sahara Magharibi.
 
..wa-Tz tuna tabia ya kujidharau.

..Hale[1964],Kidatu[1976],Mtera[1979], Kihansi[2000]...tunapaswa kubadilishana uzoefu na Ethiopia na siyo kuwa omba-omba kwao.

..pia zile habari kwamba Ethiopia itakuwa inapitisha mizigo yake bandari ya Dsm unaziamini?

..kwa ujuzi wako wa jiografia na kuzingatia ujenzi wa reli ya Addis to Djibouti unaamini kwamba Ethiopia watatumia bandari ya Dsm?

cc BAK, MK254

Yaani wewe jamaa ni wa ajabu sana. Sidhani kama unafuatilia international news na Politics.
Bwawa la Ethiopia linazaliasha 6,450 MW na wamejenga wao wenyewe. Swala la kuleta wataalamu kutoka ethiopia ni utaratibu mzuri. Hata watalaamu toka Uganda walikuja na tunashirikiana nao katika utafiri wa mafuta. Na nchi zao nao huwa wanakuja Tanzania kujifunza baadhi ya hatua tulizowazidi. Nimekueleza mwenzetu unaongelea cheap issues.

Halafu hili suala la Ethiopia sijui umelishikia kidete umelitoa wapi? Hapa Ndugu yako (Mkenya mwezio) ameleta suala la kuhusu Morocco na uhusuano wa Sisi kupiga kura juu ya Israel. Nakuona sasa umeende nje ya mada. Hicho kiashirio cha kwamba somo langu limekuingia kisawa sawa. Sasa na somo hili la ethiopia nitakupa bure.

Umesema TZ imekuwa ombaomba kwa Ethiopia, unaweza kuthibitisha hilo?
Suala la Ndege za Ethiopia kuchukua mizigo kupitia bandari ya Dar es salaam haya ni masuala ya kiusalama zaidi. Wenzetu toka ethiopia wananunua vifaa vya kivita Toka China na Russia kama sisi tufanyavyo. Lakini jirani zetu wakenya wao hununua toka USA.
Hilo nimeliongea tu kama wazo sitaki niongeezaidi. Kuna mambo mengine ya kiusalama zaidi.
Zaidi ya hapo nakuona huna hoja kuhusu thread hii. Zaidi ya kejeli nyingi zisizo na point zozote.
 
..siyo kweli.

..Morocco walibembelezwa sana waruhusu wananchi wa Sahara Magharibi wapige kura ya maoni.

..uamuzi wa kuwapa Sahara Magharibi uanachama wa OAU ulikuwa ukiahirishwa ikitarajiwa kwamba Morocco watalegeza msimamo wao na kuruhusu kura ya maoni.

..baadaye OAU ililazimika kuipa uanachama Sahara Magharibi na Polisario walikalia kiti chao nadhani ktk mkutano ambao Mwalimu Nyerere alikuwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti. siku hiyo Morocco wakatimka OAU na wakipinga uanachama wa Sahara Magharibi.

..Kwa hiyo ni kweli Morocco hawakufukuzwa OAU, walijitoa wenyewe. Lakini wapo wengi wanaoamini kwamba yalifanyika makosa kuwarudisha Morocco ktk AU huku wakiwa hawajabadilisha msimamo wao kuhusu Sahara Magharibi.

..Zaidi, tangu wamerudishwa AU, Morocco wameendelea kugomea juhudi za usuluhishi za AU kuhusu mgogoro baina yao na Sahara Magharibi.
Mwenzetu naona unaongea tu pasipo na facts zozote. Sijakuelewa wewe msimamo wako binafsi kama wewe kuhusu Morocco. Je, unataka tusishirikiane na Morocco wakati tayari kwa sasa ni member wa AU? Nimekuuliza ni nchi ngapi zilikubali kuwa Morocco ijiunge na AU? Mbona vitu simple tu hivyo.
 
Kwa hili nipo pamoja na Serikal yetu ya Tanzania sio kwa kukataa Jerusalem kuwa Mji Mkuu wa Isarel Bali kwa kupiga kura iwe kukubali au kukataa, Mataifa yaliyoamua kutopiga kura kabisa yameonesha hayajiamini kabisa!
Bora kukaa kimya kuliko kuonesha unafiki, Tanganyika imeikalia Z,bar kwa mabavu, serikali ya Tanzania inapambana na raia wake wema kwa kuwashambulia kwa risasi kisa utofauti wa vyama, watu wengi sana wamepoteza maisha yao kwa sababu ya kuwa na misimamo tofauti na serikali, kwa hali hii mnatoa wapi nguvu ya kukemea ya mbali ikiwa ya kwenu tu yamewashinda?
 
Yaani wewe jamaa ni wa ajabu sana. Sidhani kama unafuatilia international news na Politics.
Bwawa la Ethiopia linazaliasha 6,450 MW na wamejenga wao wenyewe. Swala la kuleta wataalamu kutoka ethiopia ni utaratibu mzuri. Hata watalaamu toka Uganda walikuja na tunashirikiana nao katika utafiri wa mafuta. Na nchi zao nao huwa wanakuja Tanzania kujifunza baadhi ya hatua tulizowazidi. Nimekueleza mwenzetu unaongelea cheap issue.

Halafu hili suala la Ethiopia sijui umelishikia kidete umelitoa wapi? Hapa Ndugu yako (Mkenya mwezio) ameleta suala la kuhusu Morocco na uhusuano wa Sisi kupiga kura juu ya Israel. Nakuona sasa umeende nje ya mada. Hicho ki kiashirio cha kwamba somo langu limekuingia kisawa sawa. Sasa na somo hili la ethiopia nitakupa bure.

Umesema TZ imekuwa ombaomba kwa Ethiopia, unaweza kuthibitisha hilo?
Suala la Ndege za Ethiopia kuchukua mizigo kupitia bandari ya Dar es salaam haya ni masuala ya kiusalama zaidi. Wenzetu toka ethiopia wananunua vifaa vya kivita Toka China na Russia kama sisi tufanyavyo. Lakini jirani zetu wakenya wao hununua toka USA.
Hilo nimeliongea tu kama wazo sitaki niongeezaidi. Kuna mambo mengine ya kiusalama zaidi.
Zaidi ya hapo nakuona huna hoja kuhusu thread hii. Zaidi ya kejeli nyingi zisizo na point zozote.

..siyo kweli.

..mradi unatekelezwa na mkandarasi toka Italy.

..fedha za mradi ni mkopo toka China, na fedha zao wenyewe Ethiopia.

..nimekuuliza kama unajua jiografia ya horn of africa.

..pia kama unafahamu reli ya Ethiopia-Djibouti inafanya kazi.

..halafu uniambie kama Ethiopia anaweza kutumia bandari ya Dsm.

..kuhusu silaha Ethiopia amekuwa mteja wa China na Urusi miaka mingi na hajalazimika kutumia bandari yetu.
 
Je, ni nchi ngapi zilipiga kura kuwaruhusu Morocco warudi Au?

..Hoja siyo nchi ngapi zimepiga kura Morocco arudi AU.

..Hoja ni kama kura yetu inaakisi msimamo wa Tz wa kupinga ukoloni na kukaliwa kimabavu Sahara Magharibi.
 
Nimeuliza hili swali, kwani ilikua shuruti, ilikua lazima?? Tupige kura kuwafurahisha nyie?
Morocco inatuhusu maana amekalia taifa la Kiafrika wakati nyie mnamlambalamba na kupeleka kiherehere kwa Wapalestina na Waisraeli.
Onyesha ukomavu wako nyumbani Afrika kabla ya kujifanya mtetezi wa nchi za mbali, sio huu unafiki wa kwenda kucheka cheka kule ilhali hapa Afrika unafumba macho.
Vipi mfalme aliwajengea msikiti au kawatapeli...
Viongozi wa Tanzania wanatutia aibu sana Watanzania, ya kwao yamewashinda halafu wanarukia ya mashariki ya mbali! Yanayofanyika huko mashariki ya mbali kati ya Israel na Palestine ni sawa na haya yanayofanyika huku Tanganyika dhidi Zanzibar
 
..siyo kweli.

..mradi unatekelezwa na mkandarasi toka Italy.

..fedha za mradi ni mkopo toka China, na fedha zao wenyewe Ethiopia.

..nimekuuliza kama unajua jiografia ya horn of africa.

..pia kama unafahamu reli ya Ethiopia-Djibouti inafanya kazi.

..halafu uniambie kama Ethiopia anaweza kutumia bandari ya Dsm.

..kuhusu silaha Ethiopia amekuwa mteja wa China na Urusi miaka mingi na hajalazimika kutumia bandari yetu.
Hivi umesoma ulichokiandika? Nimekueleza masuala mengine ni ya kiusalama zadi. Nakusihi ufungue thread uweke dukuduku lako hili juu ya ethiopia maana tunachoongelea hapa ni tofauti kabisa na mada unayotaka kuizalisha.
Kwanini usiazishe uzi kuhusu Ethiopia na Tanzania ili tukutoe tongotongo?
Hapa jikite kwenye mada. Kama umeelewa sema umeelewa.
Nakuusihi suala la ethiopia liache kwanza kwa sasa isiwe issue ya kujifichia. Wenzako "Wakenya" wanajitahidi sana kuhakikisha wanaichafua TZ kwenye mitandao. Lakini bahati nzuri sisi wazalendo wa TZ tutapambana nao kuhakikisha via hivi vya kiuchumi tunaibuka washindi.
 
..Hoja siyo nchi ngapi zimepiga kura Morocco arudi AU.

..Hoja ni kama kura yetu inaakisi msimamo wa Tz wa kupinga ukoloni na kukaliwa kimabavu Sahara Magharibi.
Umeulizwa tangu lini Tanzania ilikataa Morocco isiwemo AU. Tanzania tangu mwanzo haijawahi kuikatalia Morocco kuwemo AU. Sasa wewe nakushangaa sana unapoleta hoja ambayo haipo. Labda ulitaka Tanzania wafanye nini?
 
Back
Top Bottom