joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,617
Sasa ndiyo maana halisi ya kuwepo na mazungumzo, ni muhimu sana kwa Morocco kurudishiwa uanachama bila masharti yoyote yale ili mazungumzo yaweze kufanyika ikiwemo hayo masharti unayoyataka Morocco wayatimize, kumbuka kuwa na misimamo mikali kabla ya kufika ktk meza ya mazungumzo ni kikwazo cha mazungumzo, kumbuka jinsi Makaburu walivyokuwa wanampa masharti Nelson Mandela ili waweze kumuachia, kwamba aseme kwamba hatojihusisha tena na siasa akiwa huru, Mandela aliwajibu kwamba, hilo liwe miongoni mwa ajenda za mazungumzo akishakua huru...siyo kweli.
..Morocco walibembelezwa sana waruhusu wananchi wa Sahara Magharibi wapige kura ya maoni.
..uamuzi wa kuwapa Sahara Magharibi uanachama wa OAU ulikuwa ukiahirishwa ikitarajiwa kwamba Morocco watalegeza msimamo wao na kuruhusu kura ya maoni.
..baadaye OAU ililazimika kuipa uanachama Sahara Magharibi na Polisario walikalia kiti chao nadhani ktk mkutano ambao Mwalimu Nyerere alikuwa amechaguliwa kuwa Mwenyekiti. siku hiyo Morocco wakatimka OAU na wakipinga uanachama wa Sahara Magharibi.
..Kwa hiyo ni kweli Morocco hawakufukuzwa OAU, walijitoa wenyewe. Lakini wapo wengi wanaoamini kwamba yalifanyika makosa kuwarudisha Morocco ktk AU huku wakiwa hawajabadilisha msimamo wao kuhusu Sahara Magharibi.
..Zaidi, tangu wamerudishwa AU, Morocco wameendelea kugomea juhudi za usuluhishi za AU kuhusu mgogoro baina yao na Sahara Magharibi.
Morocco kujitoa OAU hakukuwa kwasababu walipewa masharti yoyote, kwamba kwasababu ya kushindwa kuyatekeleza masharti hayo ndiyo sababu ya kujitoa, kwahiyo hawawezi kurudi hadi watimize hayo masharti, sio hivyo hata kidogo, walijitoa bila masharti na wanastahili kurudishwa bila masharti yoyote yale, ninarudia tena, kitendo cha Morocco kurudi, kinafungua ukurasa wa mazungumzo, kama wasingejitoa huenda hadi leo mzozo huu ungekuwa umefikia sehemu nzuri sana.
Africa na hizo nchi zinazopinga kurudishwa kwa Morocco ili mazungumzo yaendelee, zimefanya nini ktk kipindi chote hiki cha Morocco kuwa nje ya AU, ktk kuisaidia West Sahara kupata Uhuru?, je wamepeleka jeshi ili kuitoa Morocco kwa nguvu au japo kuwapa trainings na financial support kama tulivyofanya Tanzania huko kusini mwa Africa?, au ni kupinga Morocco wasirudishwe AU tu?