MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Baada ya tukio la juzi kwa Kenya kutokuhusika kwenye upigaji wa kura kwenye mswada wa Umoja wa Mataifa kuhusu uamuzi wa Marekani kwamba Jerusalem ndio mji mkuu wa Israel, Watanzania wametokwa povu la omo huku wakishutumu Kenya, wengine wanakesha JF kabisa kwa ajili ya hili hadi nawaza hivi jameni watu huwa hawana muda wa mapumziko, hata muda wa kwenda kula, hata kama mnalipwa.
Sasa hawa hawa Watanzania kwa jinsi walivyo wanafiki, juzi wamemkenulia meno na kumpokea mfalme wa Morocco baada ya kuja kwao na kuwaahidi kuwajengea uwanja wa mpira na misikiti na vipochopocho vyote (hivi ahadi zake hizo alitekeleza? Au ndio yale yale). Huyu mfalme huko kwake ni mkoloni ambaye amelikalia taifa la Western Sahara kibabe, taifa hili limetambuliwa hadi na UN.
Leo mnajifanya kuwapigia Wakenya makelele kuhusu Wapalestina (ambao mgogoro wao na Israel wanaujua wenyewe maana hauishangi tumeuskia tangu tukiwa watoto) na hapa Afrika mnamuunga mkono na kumshobokea mkoloni Mwafrika anayelikoloni taifa la Kiafrika tena anatumia ubabe. Yaani bila hata aibu mnadhihirisha unafiki wa kiajabu.