Uhuru wa kutoa mawazo upo kama haupo.
Ukiilaumu serikali ukaigusa pabaya upo matatani !
Ukilaumu Bunge ukaligusa pabaya upo matatani !
Ukiilaumu polis ukaigusa pabaya ndio usiseme !
CCM imevikalia vyombo hivi na havipumui havina sehemu katika kufuata katiba,hii hii iliokuwepo ,hawawezi kutekeleza majukumu yao kwa kujiamini,wanahofu,wanaogopa kupoteza kazi.
Kusema hakuna Chama kingine hio sio kweli ni kuzidi kudumiza mawazo,Hakifuatwi Chama kunafuatwa Katiba ya Nchi ,vyombo husika ni lazima vifanye kazi zake kwa mujibu wa sheria,CCM imejipenyeza na imeviteka vyombo hivyo. Tunaona Chaguzi hazifuati sheria wala katiba yaani mambo mengi yanakiukwa mchana kweupe. Unapoenda kusema unakutana na wale wale waliojipenyeza.
Nchi inazidi kuvurugwa na wanaovuruga ni hawa CCM ,tukubali wameteka kila kitu.