Baadhi ya sababu ni hizi
1. Maisha ya Russia yana stress nyingi sana, kumbuka kule kuna ubaguzi wa hali ya juu, lakini ni baadhi ya sehemu. Russia bado kuna makundi ya vijana wa kifashist ambao wakimuona mtu mweusi siyo tu kumtukana, lakini huwa wanatoa hadi vichapo.
2. Maisha ni magumu, Russia siyo kama nchi nyingi za Western Europe, kule life tilt na ngumu sana kuwa unafanya kazi na kuingiza kipato kingine nje ya boom. Vitu hasa vyakula vipo juu sana wanafunzi wanashindwa kumudu matokeo yake sasa watoto wa kike wanaishia kuwa machanguduo au kutafuta waarabu waweze kuwatunza, na wale wengine wanaishi kwa utapeli na kuiba vipodozi kwenye masupermarket. Vijana wa kiume huwa wanafanya mpango wa kuwa na wanawake wa kirusi wenye kazi nzuri au maisha mazuri ili waweze kukabiliana na maisha, haswa hapa ndipo tatizo linapoanzia manake mtoto wa kiume anajikuta hana kabisa uhuru wa kufanya lolote mbele ya mwanamama ukiangalia anapewa hela ya kula na kunywa.
3. Ingawa maisha ya Russia especially Moscow yapo juu sana, lakini anasa ni nyingi sana zikiwemo pombe na wanawake. Kwa ufupi Russia wanauza pombe na sigara kwa bei nafuu sana hii inasababisha hata kwa hela ndogo kabisa watu waweze kumudu. Kingine hapo ni hao wanawake, Russia imejaaliwa kuwa na wasichana wazuri na warembo haswa ukilinganisha na wazungu wengine, wasichana hawa wengi wao ni warahisi sana na unakuta wanapenda watu weusi, sasa hapo nipo kwenye tatizo, vijana wengi wanafanya umalaya wa kupitiliza hadi kusahau kabisa shule, au unakula mwanamke anamng'ang'ania ili abaki Russia masomo yake yatakapoisha. Sasa hii kitu huwa inawaconfuse sana vijana wetu kule.
4. Vijana wengi wa kiume huwa wanazaa na wanawake wa kirusi, lakini wanafanya hivyo bila ya kuwa na malengo maalumu angalau wapo wale wanaotaka passport(wachache sana). Sasa unakuta mtu anapomaliza anataka achukue mtoto wake na dada wa kirusi anagoma kwa hiyo unakuta mtu anachanganyikiwa kwa kuacha damu yake ughaibuni (hawa wapo wengi sana, nadhani ndiyo wanaongoza).
5. Angalau Russia kuna ubaguzi, lakini kwa upande fulani kuna ufree mkubwa sana kwa mtu kuamua aishi vipi, yaani mtu anaweza toka bongo ni ustaadhi au mlokole mzuri lakini akifika kule anakutana na ule ufree ambao bongo alikuwa haupati(kumbuka wengi wanaojifanya kushika sana dini kwa hapa kwetu tz ni kwa ajili tu ya mazingira na watu wanaomzunguka) sasa kwa Russia no one cares wewe fanya utakalo as long kwamba hauvunji sheria za nchi. Unaweza ukawa unakwenda club kila siku kuanzi j3, j4 hadi j3 nyingine, unaweza wewe ukawa unakunywa pombe kiasi utakacho, yaani hakuna atakayekufuatilia kabisa, that is your life.
6. Kingine ambacho nadhani ni kikubwa zaidi ni hizi Russian Vodka, hizi kitu aisee ni shida sana, ni pombe kali sana hakuna. Vijana wengi huwa wanazifakamia hizi kitu na hasa ukizingatia hata kama Tz zipo lakini siyo kali kama za Russia, zile za kule jamani ni balaa sana. Warusi wenyewe hasa wenye fezwa huwa wanakunywa sana Vodka, lakini wanakula matunda mengi na manyama nyama yao fulani ambayo yanasaidia sana kuua ukali wa pombe, sasa mwenzangu na mimi mwanafunzi wa kibongo na boom la dola 300 kwa mwezi hautoweza kumudu kununua hizi nyama na matunda, ni ngumu sana. (Hii ndiyo sababu kubwa zaidi kwa upeo wangu, Vodka ndizo zinawapa watu matatizo, narudia tena hii siyo kwa watanzania tu hata kwa warusi wenyewe hasa wale wa kipato cha chini huwa wanapata uchizi kutokana na hizi pombe kali za Vodka).
7. Winter, baridi la Russia ni baridi dume yaani usikae kabisa ukataka kulinganisha na kale kaupepo ka Makambako. Russia kuna winter la hatari, ila warusi wengi walio na kipato kizuri huwa wanaweza kujisitiri na hili baridi, lakini sasa wabongo inakuwa ngumu kwao kutokana na kipato hafifu walichonacho kuweza kununua nguo nzito kama vile sox za winter, viatu vya winter, makoti, sweaters, gloves, kofia nzito, blanket nzito za winter, kwa hiyo athari ya baridi huwa linawachukua taratibu sana mpaka ukifika muda wa miaka mitano mpaka kumi nipo unakuta mtu anaumwa sana tena magonjwa ya baridi ambayo kisayansi ungonjwa unaweza penya hadi kwenye ubongo na kumfanya mtu awe chizi.
8. Kingine angalau kinaweza kisichangie sana ni sigara, watu wengi wanaanza kujifinzia kuvuta sigara wakiwa kule, hii ni katika harakati za kupunguza baridi na stresses.
Ushauri: Serikali isiwe inawatelekeza hawa watoto na vijana wetu walio kule. Iwe inajaribu kufanya follow ups na kujua maendeleo yao academically. Elimu ya Russia ni nzuri sana, lakini kuna udanganyifu wa hali ya juu kwenye kupata marks na hatimaye cheti.