Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema Wakuu!
Napenda Siasa Kwa sababu ni mchezo wa wenye wajanja. Napenda Biashara Kwa sababu ni mchezo wa wenye bahati, napenda Fasihi na Falsafa Kwa sababu ni uwanja wa Akili na hekima.
Napenda sheria Kwa sababu ni mto ubebao Haki na Dhulma. Itoshe!
Watanzania wengi ni watu wa ajabu Sana, ukienda vijiweni ukaanzisha Mada ya Siasa hutapata wachangiaji wengi, na wengi watakuambia hawapendi kujadili wala kujiingiza kwenye Siasa. Hilo sio tatizo kwani kila mtu anamaamuzi na Uhuru wake, lakini tatizo ni pale mtu asiyejihusisha na Siasa halafu muda huohuo utamkuta ananilaumu serikali au kuwasema viongozi. Huo Kama sio wendawazimu ni nini!
Siasa ni mchezo wa maslahi, vita ya kupata kikubwa, silaha ya kuitafuta kesho iliyobora kabisa.
Huwezi kuwa Mfanyabiashara mkubwa bila kuwa mwanasiasa, huwezi kuwa mtu Mkubwa bila kuwa mwanasiasa, huwezi kuwa Sheikhe, Imamu au Mchungaji au Askofu bila kuwa Mwanasiasa.
Huwezi kuwa Mwandishi, Mwanamuziki mkubwa bila kuwa mwanasiasa,
Kujitenga na wanasiasa kunamaanisha Jambo moja tuu, kutafuta kuwa mnyonge, mtu asiye na maslahi.
Msindikizaji,
Kama kuna Jambo ambalo watoto wangu nitawaambia wasije kujitenga nalo basi ni Siasa. Kujitenga na Siasa ni kutaka kutawaliwa, kukaliwa kooni, kuwa tabaka la chini.
Watu wote wakubwa katika sekta zote wanajihusisha na Siasa iwe Direct au indirect.
Kujiingiza kwenye Siasa Kwa watu wote ndio huitwa Demokrasia, yaani kila mmoja kuyapigania maslahi yake kivyovyote, Kwa Amani au kwa vita, Kwa mazungumzo au Kwa silaha.
Kugawana na sio kugawiwa.
Kupeana na wala sio kupewa.
Wanasiasa wote Duniani wanatabia zinazofanana, Hawana tungo isemayo; Kesho yangu ni bora kuliko leo.
Wao wananeno moja tuu, nalo ni; Leo ni leo asemaye kesho muongo.
Wanasiasa wanamsimamo wa tumalizane leoleo, kila mtu achukue chake leo, mambo ya kesho yatajijua yenyewe.
Wakiwa mbele za watu watasema, Mradi au mpango huu utaleta tija miaka kumi ijayo" ilhali wao wananufaika na mpango huo Leo hii,
Ni Kama Siasa za wachungaji na waganga wajanja, atakuambia Akuombee na mwaka ujao utafanikiwa tuu! Lakini wao watakuambia uwape pesa Leo hiyohiyo. Hiyo ni Siasa, janja janja na utapeli uliohalalishwa.
Watanzania wenzangu sijui nilikuwa nazungumzia nini, hapa nimeshajichanganya.
Ila niseme tuu; Kujitenga na Siasa ni kujitenga na maisha mazuri ya Dunia.
Kukimbia maslahi yako na familia yako.
Nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam