Watanzania wako sahihi kukesha humu huku wakitumia Kenya kama benchmark maana siku zote unakimbia umfikie aliye mbele yako, lakini pia haiwezekani ukakimbia huku ukijilinganisha na uliowaacha nyuma, ndio maana huwapati Wakenya humu wakibanana na Watanzania kwenye hizi hoja za kulinganisha urefu wa dushe. Walio huku ni wachache kama mimi ambaye nimewahi kuishi Tanzania, na wengine ambao labda walikua wanapita wakagundua JF, hutupia neno moja na kuendelea na shughuli zao.
Wakenya tuna upweke sana hapa Afrika mashariki na kati hadi DRC kote huko, maana hatuna aliyefikia level yetu wa kuendana naye, hivyo huwa tunajikuta tukipimana na Afrika Kusini.