Pre GE2025 ‘Watanzania wanyonge’ wataka Paul Makonda agombee na kupewa Urais 2030

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wewe Kweli ni Bumunda, unajisifu nchi kuagiza sukari badala ya kuzalisha? Kuagiza ina maana huna uwezo wa kuzalisha, wakati huo miwa ya wakulima kilombero inaoza, watalipaje hiyo mikopo ya pembejeo? Hiyo bajeti ya kilimo iliyoongezeka imesaidia vipi ukuaji wa sekta ya kilimo?
AKILI ILIYOTENGENEZA TATIZO HAIWEZI KUWA NA SULUHU YA KULITATUA.
 
Wewe jamaa umeandika maelezo mengi lkin sijayaelewa. Labda nenda ukawambie NEC. hao labda watakuelewa
 
Serikali imeagiza sukari kutokana na ugumu wa kuvuna miwa mashambani hapa nchini, kunakotokana na wingi wa mvua zinazoendelea kunyesha. Kwahiyo mvua zikipungua miwa yote inayostahili kuvunwa itavunwa ili kuzalisha sukari
 
Mkianza kumtangazatangaza mapema mtamharibia sifa na kuukosa huo urais. Mbona mnajifanya hamjui mitandao na makundi ya wataka urais ndani ya chama chenu? Tulieni muda ukifika akitaka awanie tu ndio muanze kumpamba na kumpigia debe
 
Serikali imeagiza sukari kutokana na ugumu wa kuvuna miwa mashambani hapa nchini, kunakotokana na wingi wa mvua zinazoendelea kunyesha. Kwahiyo mvua zikipungua miwa yote inayostahili kuvunwa itavunwa ili kuzalisha sukari
Kwa hiyo tunaishi kijima, tunakula tunachovuna leo, kwamba hata bodi ya sukari na wazalishaji hawajui kuwa kuna msimu wa mvua? TMA toka mwezi wa kumi wametahadharisha kuwa kutakuwa na mvua nyingi kuliko kawaida, nini kilifanyika kama njia ya ku address risk ya kutokea kushindwa kuvuna, assessment ilifanyika? Mitigating factors gani zilichukuliwa?
Halafu eti mwenyekiti wa Bodi ya Sukari ni profesa, ndiyo maana akina Musukuma wanaonekana wa maana kuliko wenye elimu isiyosaidia taifa na machawa kama wewe wasiyotumia akili kidogo mlizojaaliwa.
 
Mjumbe hauwawi.

Msikie ujadili

Hakuma cha taarifa nyeti ndani ya mfumo na hakuna cha wazee wa chama, hakuna cha imeamuliwa mtoto wa MC wa serikali ndiye ataachiwa gaga.

Paul Makonda ni kijana mnoo ila imeamuliwa hivyo siyo​



 
Tuacheni tupumue Jamani
Mala Mavunde mala Bashite.
Tunahitaji kupumua na hizi habari lojolojo…
 
Ushashiba futari ya mihogo unaanza kutubeulia huku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…