Hayo madude ya viongoz wenuHii Injii Ina wajinga sana .. Kuna wale ambao Kila wakila KASA wanakufa ila hawajawahi kuacha Kula KASA, na wakila haipiti muda utasikia watu Saba wafariki Dunia.
Lakini sawa, tumekubali ni Wajinga, Kwann Serikali Huwa inazisajili hizo Taasisi uchwara, na Ukute na Kodi wanakupa ? Nini nafasi ya Serikali kushughulika na Hawa Wezi ??.
Mimi Huwa nafikiria, haya madude, ni Viongozi wenyewe , maana Kwa Tanzania, hamna kinachoshindikana.
Nature ya biashara yao Ni hiyo hiyo Upatu hao GNLD 2013 nili itwa kufika uko n habari hizo hizo za kuuza madawa ya kilimo na bidhaa zinginezo na ukijiunga una ombwa ulete watu wajiunge chini yakoHivi GNLD na FOREVER LIVING bado yapo
Imeshawahi kufanya mfanyakazi mwenzangu akaacha kazi baada ya muda akawa anaishi kwa msoto mkubwa mno.
Haya sio makampuni ya upatu isipokuwa ni makampuni ya kuuzwa madawa ya virutubisho au supplements
Intelejensia ya uchumi full kurugenzi inahitajika.Hii michezo huwezi kuelewa kwa vile hakuna close monitoring na watanzania wengi hawana ufahamu.
Mfano serikali inaweza kuwapa vibali ila mnajua vibali gani? kama ni financial ishu lazima wawe subjected to finance act ili wapete vibali kutoka BOT .
sasa wengi mnaonyesha usajili wa kampuni sijui brela na zile namba pale chini hmafuatilii ndo maana bongo cheti ndo kinatambulisha uwezo wa mtu hata kama kichwani ni zero.
unaweza kuta kampuni imesajili kufanya shughuli zake binafsi wakachomekea uwekezaji kwa nia ya kutapeli lazima mpigwe tuππ.
Mambo ya uwekezaji yanahitaji kusoma sana sio kukurupuka wacha wapigwe
Mkuu miezi mitatu haipiti watapigwa na wengi ni hao wasomi ππ.Intelejensia ya uchumi full kurugenzi inahitajika.
Madawati ni kupoteza tu
Nakuunga mkono. Hapa bongo utakuta msomi mkubwa tena alikuwa kipanga sana shuleni lakini linapokuja suala kuwekeza fedha yake izae nyingine hawezi chochote. Kuna Branch Manager flani mstaafu wa CRDB alikuwa miongoni mwa waliolizwa noti ndefu sana na Mr Kuku.Mkuu hii nchi hata ambao unaona wanaakili wanapigwa kizembe mnoo. Kuna wanajeshi flani hivi walipigwa hela Kama milioni kumi hivi kwa haya maswala ya upatu. Ila hata maprofesa na mawaziri wanalizwa Sana pesa na matapeli kwa tamaa zao. Usiwaone wanavaa matai na suti hamna kitu vichwani. Ndoo maaana mkiwatukanaga walimu humu kuwa ni kada ya watu wasiojielewa huwa na cheka Sana. Watanzania wengi uelewa Mdogo Sana.
Utapeli wa upatu uko duniani kote, huu hapa Tanzania ni kidogo sana. Msiilalamikie serikali katika hili.
Mjomba wangu alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi huko Mbeya. Kastaafu mwaka 2017 na kalipwa mafao mwaka 2019. Aliwekeza Tsh 30,000,000. Zimepotea. Wala wasimsumbue RaisNashangaa kusikia watu wanataka RAIS aingilie kati kwenye suala ambalo linatokana na utashi wao weneyewe!! Unapowekeza mahala popote ujue kuna kupata na kukosa; mbona mwanzoni wenyewe wanakili kuwa walikuwa wanapata gawio na hawakulalamika!! Sasa mambo hayakwenda vizuri inabidi wawe wapole na kuvumilia machungu bila kumuhusisha Rais.