MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kumekua na mjadala Tanzania unaoratibiwa na taasisi inayofahamika kama Hakielimu, ajenda kuu ni ipi lugha ambayo itumike kwenye kufanikisha elimu, baina ya Kiswahili na Kingereza. Baadhi ya waliotetea Kingereza waliwashutumu ambao wanakitetea Kiswahili kwamba wao ni wanafiki, maana watoto wao wanasoma kwenye shule za English medium na kuongea Kingereza halafu huku wale wa saint Kayumba wanaambiwa wakomae na Kiswahili.
Hili nimewahi kulisema humu, Watanzania matajiri au walio kwenye uongozi wao huhakikisha watoto wao wanasoma kwenye shule zinazofundishwa na aidha Wakenya, Waganda au za kimataifa na lugha ya kingereza inatumika pale, halafu walalahoi wengi wanaambiwa wawe wazalendo na kukomaa na Kiswahili.
Ukiangalia matangazo ya ajira Tanzania, hususan kwenye ngazi za uongozi au management utakuta humo wanachomekea kwamba wanakusudia muombaji lazima awe na uwezo wa kuzungumza Kingereza tena kwa ufasaha. Hii huwavunja moyo wale wa saint Kayumba maana wao na Kingereza hawaendani....
Mnafaa kuiga Wakenya, sisi tunaongea lugha zote, kwanza tunaenzi zetu za asili halafu pia tunakipenda Kiswahili lakini Kingereza huwa hatuchezi mbali nacho maana ndio lugha ya dunia, Mchina, Mrusi, Mjapani, Mwarabu, Mhindi n.k. wote wako mbioni kujiboresha kwenye lugha ya kingereza, wewe maskini Mswahili umejifungia ndani ya lugha moja halafu ukiulizwa unajitetea kwa kuwataja hao Wachina na Wajapani ilhali kwako huna hata kiwanda cha sindano.
-------------------------------------------------
Dar es Salaam. Tanzania is apparently at the crossroads over which language between Kiswahili and English to use as the medium of instruction. This became more evident in Dar es Salaam yesterday when experts failed to reach a consensus on the topic during a debate, which was organised by Hakielimu, a non-governmental organisation, which specialises in education issues.
The pro-English group believes that their pro-Kiswahili counterparts were supporting the widely spoken language in the country for personal gains.
Swahili or English? Tanzania education experts differ on medium