Watanzania wapo kwenye njia panda baina ya Kiswahili na Kingereza

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Kumekua na mjadala Tanzania unaoratibiwa na taasisi inayofahamika kama Hakielimu, ajenda kuu ni ipi lugha ambayo itumike kwenye kufanikisha elimu, baina ya Kiswahili na Kingereza. Baadhi ya waliotetea Kingereza waliwashutumu ambao wanakitetea Kiswahili kwamba wao ni wanafiki, maana watoto wao wanasoma kwenye shule za English medium na kuongea Kingereza halafu huku wale wa saint Kayumba wanaambiwa wakomae na Kiswahili.

Hili nimewahi kulisema humu, Watanzania matajiri au walio kwenye uongozi wao huhakikisha watoto wao wanasoma kwenye shule zinazofundishwa na aidha Wakenya, Waganda au za kimataifa na lugha ya kingereza inatumika pale, halafu walalahoi wengi wanaambiwa wawe wazalendo na kukomaa na Kiswahili.
Ukiangalia matangazo ya ajira Tanzania, hususan kwenye ngazi za uongozi au management utakuta humo wanachomekea kwamba wanakusudia muombaji lazima awe na uwezo wa kuzungumza Kingereza tena kwa ufasaha. Hii huwavunja moyo wale wa saint Kayumba maana wao na Kingereza hawaendani....

Mnafaa kuiga Wakenya, sisi tunaongea lugha zote, kwanza tunaenzi zetu za asili halafu pia tunakipenda Kiswahili lakini Kingereza huwa hatuchezi mbali nacho maana ndio lugha ya dunia, Mchina, Mrusi, Mjapani, Mwarabu, Mhindi n.k. wote wako mbioni kujiboresha kwenye lugha ya kingereza, wewe maskini Mswahili umejifungia ndani ya lugha moja halafu ukiulizwa unajitetea kwa kuwataja hao Wachina na Wajapani ilhali kwako huna hata kiwanda cha sindano.
-------------------------------------------------

Dar es Salaam. Tanzania is apparently at the crossroads over which language between Kiswahili and English to use as the medium of instruction. This became more evident in Dar es Salaam yesterday when experts failed to reach a consensus on the topic during a debate, which was organised by Hakielimu, a non-governmental organisation, which specialises in education issues.

The pro-English group believes that their pro-Kiswahili counterparts were supporting the widely spoken language in the country for personal gains.
Swahili or English? Tanzania education experts differ on medium
 
Wakubali tu kutumia kiingereza mashuleni ila wasikubali kiswahili kififie alafu mwishowe kife kama mbwa koko.
 
Wakubali tu kutumia kiingereza mashuleni ila wasikubali kiswahili kififie alafu mwishowe kife kama mbwa koko.
Our very Important ambition is to Brand Kiswahili to the Entire World,
It Started from Tz, Nyerere bolded the use of Kiswahili, and now You Kenyans, Ugandans, DRC, Zambia, Rwanda, Burundi, Mozambique are using Kiswahili,
Mark My Word, Kiswahili Kitakuwa Lugha namba Moja Africa Nzima.
 
Sio lazima uingize ligi kwenye kila jambo. Kiswahili kilianza kutumika pwani ya Afrika Mashariki miaka mingi tu kabla ya Nyerere kuzaliwa.
 
Sio lazima uingize ligi kwenye kila jambo. Kiswahili kilianza kutumika pwani ya Afrika Mashariki miaka mingi tu kabla ya Nyerere kuzaliwa.

Kwanza hawana habari kwamba Kiswahili kinafahamika duniani kwa ajili ya jitihada za Wakenya, cha msingi ni kwamba sisi hatukufungiwa kwenye lugha moja, tunakipenda hicho Kiswahili lakini pia tunapanua wigo kwa kuhakikisha ufasaha kwenye lugha zingine zikiwemo zetu za asili.
Hamna kitu hunipa raha kama ilivyo wakati naona wanangu wanaongea lugha kadhaa bila matatizo, yaani mtoto anatiririka Kikikuyu, Kiswahili, Kingereza, Kifaransa (hiki wanafundishwa shuleni) na hata Kiluhya.

Hata utafiti wa Kisayansi ulishabaini kwamba mtu akiganda kwenye lugha moja anaishia kuwa mbumbumbu wa kiaina. Inabidi kuwa mjanja wa lugha kadhaa kwenye dunia ya kisasa ambayo ishakua kijiji.
 
 
 
Una kichaa? Kiswahili kilianza Kenya na Tanzania kwa waswahili wenyewe. Waswahili wapo Tanzania na pia wapo Kenya.Usije tena ukaropokwa hivyo? Wewe bado kijana mdogo nenda kasome historia ya chanzo cha lugha ya kiswahili. Hata wengine husema kilianzia Kenya kisha baadaye kikasambaa kusini mwa pwani ya Kenya.
 
I totally agree with u% mimi ni mtanzania lakini na pinga kiswahili kutumika katika mfumo wa elimu wakati watoto wa viongoz wakubwa kama magufuli kikwetw na wengine wakisoma English medium school@ sisi watanzania wachini ni wapumbavu sana to accept swahili ad our medium language of instruction
 
Wewe naelewa unazeeka Vibaya.
 
Ni njia mojawapo ya kuwatenganisha masikini na Tajiri.
 
Tanzania mkikubali kiingereza, kitu kitachofuata ni kichaina.

Kenya wamepitia hayo yote
 
Huu utani mwingine mpunguze jamani, eti kiswahili kinajukikana dumiani kwa kwajitihada za Wakenya, ni sawa kusema kifarana kinajulikana duniani kwa jitiada za wabelgiji au Kichina kinajulikana kwa jitihada za Taiwan. Kumbuka vitabu vingi vya kiswahili 60s na 70s Kenya vilikuwa vinatoka Tanzania bila kisahahu biblia takatifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…