Mmngekua proud na uafrika, mngeanza kwa kukumbatia lugha zenu za asili, lakini wengi wenu hamjui hata salamu kwa lugha zenu. Mnaita ushamba, ukweli wa mambo kingereza kimewashinda na ndio maana mumekiogopa.
Hao Wachina uliokua nao wakiandika thesis in English maana wanatambua umuhimu wake, mamilioni ya Wachina, Wakorea, Warusi, Wahindi n.k. dunia hii wapo mbioni kujifunza kingereza, wewe maskini mswahili hutaki kujiboresha unadanganywa na wakuu wa kwenu ukomae na lugha moja ilhali watoto wao wanatumia kingereza balaa na kunyakua fursa zinazokihitaji.
Leo hii ukienda Urusi, Uchina au hata India inabidi mpatane nao kwa matumizi ya kingereza, sawa wao kwa wao wanatumia lugha zao, lakini ili mpatane au wawasialiane na wageni, kingereza kinatumika sana.
Mngekua mumejisimamia kiviwanda labda ningeelewa hilo la kukomalia lugha moja, lakini hadi chupi na nguo za ndani na sindano vyote mnaagiza, halafu kiuzembe hamtaki kujifunza lugha za hao mnaagiza kutoka kwao, mnaishia maisha ya tabu sana maana vitu vyote vinakuja vimeandikwa kwa lugha yao. Na ndio maana huwa mnaliwa sana kwenye raslimali za nchi, mikataba imeandikwa kwa kingereza, tena zenye kurasa nyingi sana na mlivyo wavivu wa kusoma hadi huruma....
Nimekuambia na narudia tena, Somalia nimeitaja kama mfano kwako kwamba ubaguzi unaweza kuja kwa kutumia vyanzo vingine nje ya lugha. Watu wanaweza kutumia lugha moja lakini wakabaguana na kupigana kwa misingi ya kiukoo, rangi ya ngozi n.k. Somalia sio vita vya madaraka tuu, kuna koo hazioani kabisa, na huajiriwi kwenye hoteli zinazomilikiwa na mtu wa ukoo fulani kisa ukoo wako huwa hauendani na ukoo wake. Kama hujaelewa hapo basi sitoweza kukusaidia.