Watanzania wasipopata mabadiliko kutokea ndani, Watayatafuta kutokea nje

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
17,047
Reaction score
63,206
Katika miaka ya 1990's Mwalimu Nyerere alipokuwa akiongea na waandishi wa habari. Aliongea kwa kirefu sana kuhusu watu kujaribu kutumia mataifa ya nje kushinikiza mabadiliko ndani. Akasema tujitahidi mambo yetu tuyamalize humuhumu sisi wenyewe. Akatolea mfano wa baadhi ya marais wa Afrika wa wakati huo ambao walikuwa wamewekwa madarakani na wazungu, mfano Mobutu. Akaeleza kirefu jinsi Mobutu alivyowekwa madarakani na Wamarekani na Wabelgiji.

Hata hivyo Mwalimu ambacho hakukiona au kukifikiria ni kuwa in the future tunaweza kupata mtawala ambaye kwanza hataki kusikiliza hata commonsense, ambaye yuko tayari kuteka, kupoteza na ikibidi kuua watu ili aendelee kubaki madarakani kiasi kwamba hiyo dhana yake aliyopropose ya sisi kwa sisi kukaa chini na kuyamaliza mambo yetu sisi wenyewe kwa wenyewe haiwezi kufanya kazi.

Hebu tazama kwa mfano, wakati mtu anaitisha mazungumzo anayoita maridhiano kumbe hayuko genuine, anayatumia kama tactic ya kuchelewesha mambo ili upepo upite (delay tactic).

Anapotakiwa afanye reforms za msingi yeye anaona njia bora ni kufungulia watu kesi kubwakubwa za uhaini au ugaidi.

Zinapoibuka damu changa zinazochemka za vijana kama Soka, Mdude akili inayomuijia dhalimu ni kuteka na kupoteza.
Yaani vijana wetu jasiri wanaohitaji kuwa groomed ili wawe na mchango chanya kwa Taifa wao solution yao ya kudeal nao ni kuwateka na kuwapoteza. Sijui wanataka Taifa la vijana mandondocha matupu ambayo ni hohehahe mzungu wa reli?. Taifa gani hilo la mambo ya ajabu ajabu namna hii?.

Leo limetokea wimbi la Wakenya kuinyooshea kidole serikali yetu, kutokana na utawala wa hofu nchini, ambapo mtu kutekwa na kupotezwa ni rahisi kama kula ugali. Cha ajabu Watanzania wengi mitandaoni wanafurahi, wanaunga mkono na wanahimiza. Hii maana yake nini?. Maana yake ni kuwa Ukiziba njia zote za Mabadiliko kupitia ndani mwetu sisi kwa sisi, Basi Watanzania watatafuta Mabadiliko kutokea hata nje ya nchi.

Athari ya hivyo ni kuwa, kwanza unapominya haki ndani, unamlazimisha mtu atafute alliance nje ya nchi. Na ukifanya hivyo unaweza kumkaribisha adui wa nje. Kwa sababu kama wewe ni adui wa mtu wa ndani, na uko tayari kumuua, basi ili mtu huyo asurvive anaweza kumuunga mkono adui wa nje ambaye yuko tayari kudeal na adui yako wa ndani (Adui ya adui yako ni rafiki yako). Leo ninaumia kusema kuwa nina hofu kuwa kama nchi yetu kama ikishambuliwa kijeshi kutokea nje, tumegawanyika kiasi cha kutosha kiasi kwamba inaweza kusababisha ama watu huenda wakatae mwito wa kuilinda nchi kwa kudhani kuwa kufanya hivyo ni kuufanya utawala udumu, au wampe ushirikiano adui kwa kudhani kuwa angalau huyu hatateka wala kuua watu au kufanya dhulma ya kutisha inayoendelea nchini ikiwemo ufisadi, wizi wa kura, na ubadhirifu wa rasilimali za nchi. Hiyo ni scenario ya kutisha kabisa kwa haya mambo yanayoendelea nchini. Wenye hekima wanapaswa kuliona hili na kulitafutia ufumbuzi.

Kama taifa tulikuwa na fursa ya kuiweka nchi ktk msitari sahihi baada ya zoezi la kujaribu kuandika katiba mpya mwaka 2011-2013, lakini watawala wakahujunu mchakato ule, wakatumia mabilioni ya pesa za umma kwa kitu walichokuja kukihujumu. Na walifanya haya kwa sababu ya kulinda tu madaraka yao, power yao, influence yao n.k., Lakini athari za ujinga wao tunaziona leo ambapo muundo wa sasa wa Kiutawala haulazimishi uwajibikaji kwa mtawala wa juu, na kwa wateule wake uwajibikaji wao ni mpaka aliyewatea awalazimishe kuwajibika!. Kwa hiyo hata matendo haya ya utekaji na kupoteza watu yanachagizwa na katiba ya sasa ya kutohimiza uwajibikaji. Ingekuwa tuna ile katiba ya wananchi ya Jaji Warioba leo haya mambo ya utekaji pangechimbika kwelikweli kuanzia kuwajibishwa kwa IGP mpaka Rais mwenyewe. Kiufupi haya mambo yangepungua sana!.

Mimi nawaonya tu watawala, Wakigeuka adui wa ndani wa umma, basi Wananchi nao wanaweza kujikuta wanaalika adui wa nje ili kuonyeshana makali. Hapo Taifa litakuwa salama kweli?.

Mwenye akili na afahamu.
 
umenena vyema

yana mwisho haya, ila kuna mmoja mwishow ake utakuwa mbaya sana

kajilimbikiz mali lakini hatazifurahia!
 
hakuna ishara wala dalili ya kutokea jambo hilo hivi karibuni labda baada ya miaka 200 ijayo gentleman 🐒
 
Back
Top Bottom