Watanzania watia moto vifaranga wengine 5,000 kutoka Kenya

Watanzania watia moto vifaranga wengine 5,000 kutoka Kenya

angalau hivi vya sasa hivi wamevipulizia dawa vikafa ndio wakachoma moto!!!wamerekebisha walipokosea awali
 
Hehehe, sasa nyinyi si ndo mnafata vifaranga hadi Kenya, Kenya vifaranga vinazalishwa kwa wingi sana, ila wafugaji wa kuku ndo wengi zaidi! Kama mikakati ya kuwazalisha vifaranga Tz ndo hiyo, basi mmepiga hatua kubwa sana.
Kaka hakuna anayefuata vifaranga Kenya wakati inajulikana kwamba Tanzania imepiga marufuku biashara ya kuingiza aina yoyote ile ya ndege, ni kama vile tulivyopiga marufuku miraa, bhangi, na heroin, sasa mtu akiamua kufanya hizo biashara kwa njia za magendo na akakamatwa, unategemea nini?
 
Aliyekamatwa na vifaranga hivo si ni mtanzania? Ama mmemkana kama mnavofanya na omba omba wenu ambao wapo kwenye miji ya Kenya?
 
Kitachofata na hawa wafanyabiashara tutawachoma moto

Hehehe! Tayari kwa kuchoma bidhaa zao ni sawa na kuwatia vibeiriti hao wafanyi biashara wenu.
 
Haijulikani hadi sasa kamani mtanzania au mkenya.
Soma taarifa upya, kisha utafute kamusi ya kiingereza ndo ujue tofauti ya importer na exporter. Kama ingekuwa mkenya vifaranga hivo baada ya wiki mbili vingekuwa kwenye menu za hoteli flani!
 
Hehehe! Tayari kwa kuchoma bidhaa zao ni sawa na kuwatia vibeiriti hao wafanyi biashara wenu.
Hawa wanabiashara watz ni maandas sana hata kukamilisha tu mishen simpo hivo ni kibarua? Angetafuta tu muhuri wa 'Made in Somaliyaa' na stakabadhi feki kutoka Kismayo. Kwisha! 🙂
 
Uchome mali ya Mtanzania mwenzako halafu utambie Wakenya, kweli nyie Nyerere aliwaharibu na itachukua muda mrefu sana kuja kufunguka kiakili, bado mpo kwenye giza sana.
Wale 6,400 walikuwa Mali ya mtz au mkenya?
 
Hawa jamaa wana matatizo makubwa kwa kweli, yaani hapo wamemrudisha nyuma mjasiria Mtanzania na kumpeleka hasara kubwa, halafu wanatutambia sisi Wakenya wakati Mkenya keshatia hela yake mfukoni. Ukishanunua kutoka kwangu na kuvuka mpaka, mtajuana wenyewe huko huko, mimi kuanzia hapo nawaza mengine.

Tatizo kubwa Tanzania ni ujamaa, uliwalemaza kiakili kwamba akiona mwenzake anatoka kimaisha anajaribu kila mbinu za kumkwamisha. Ujamaa ulikua hivyo, ilikua ukionekana umenunua gari kijijini yaani hata serikali inakuvuruga, sasa hilo tatizo limewaingia mpaka vizazi vya leo. Huwa wanafiki sana na kuchekeana na kuitana mkuu lakini kimya kimya wanatafunana sana hawa.
Utakuta aliyechoma hivyo vifaranga alipata raha sana kwamba amemkwamisha Mtanzania mwenzake na kumrudisha nyuma, hamna cha hizi rhetoric wanazozirusha humu eti safety bird flue sijui sheria, hizo ndio MACCM ambayo hukesha huku Kenyan forums bila hata kunawa uso yamekaririshwa kama PR.
Nenda Dar uone vile wao hukwamishana hata kwenye maofisi.

Hzo roho mbaya ndio zimesababisha ndugu zao wanaikimbia nchi na kuja kuwa omba omba Kenya.

Mwanzoni ilikuwa Mali ya mkenya, ndio maana Amina Mohammed alikuja Dar,but,hii ya 5,000 imekuwa Mali ya MTZ? Hahaha,mmeufyata.
 
Wale 6,400 walikuwa Mali ya mtz au mkenya?

Ndio tatizo lenu kubwa, huwa mnakurupuka humu bila kufuatilia taarifa, aidha uelewa wenu mdogo sana.
Yaani hao viranga 6,400 hukujua walikua wa nani.
 
Serikali ya awamu hii sio yakuibeep kabisa watu inabidi tubadilike,ukiambiwa acha basi ujue wana maanisha kweli uache na ukikaidi basi ujue utapigwa tu.
....Tatizo ni sheria kutekelezwa kwa double standards....msumeno unatakiwa ukate kote kote...
 
Soma taarifa upya, kisha utafute kamusi ya kiingereza ndo ujue tofauti ya importer na exporter. Kama ingekuwa mkenya vifaranga hivo baada ya wiki mbili vingekuwa kwenye menu za hoteli flani!
Mbona ninapata taabu sana kuelewa uwezo wako wa akili ulivyo?, importer katika immigration post ya Tanzania ni mtu yeyote anayeingiza bidhaa nchini, bila kujali uraia wake, mbona ni elimu ya darasa la tano huku Tanzania hiyo, hata hili pia unataka tukufunze humu JF?, kaazi kwelikweli.
 
Mara ya mwisho wewe kufika kwenye border post za Kenya ni lini? We jamaa bana, hujui unachosema. Hayo kando, ni wazi kwamba alikamatwa na immigration kwasababu yeye ni mtanzania! Labda aliomba asamehewe! 😀 Musee wakenya iko mfuko ndefu buana! 😀😀
 
Back
Top Bottom