Mwaka juzi Nov 2017 tulikamata ng'ombe 1,100 wa Masai wa Kenya waliovuka mpaka wetu kuja kutafuta malisho, serikali ya Kenya ikatuomba tuwarudishe tukakataa tukawapiga mnada.
Mwaka jana Feb 2018 tulikamata vifaranga vya kuku 5,000 kwenye mpaka wa Namanga vyenye thamani ya Tsh.12m tu vilivyokuwa mali ya mfanyabiashara kutoka Kenya, wakatuomba tuvirudishe tukakataa tukavichoma.
Mwaka jana huo huo na mwezi huo huo wa Feb 2018 polisi ya Kenya ikakamata dhahabu kilo 35 na pesa taslim karibu Tsh 500m mali ya mfanyabiashara kutoka Tanzania, hatujawaomba wameturudishia.
Nini Rais Uhuru Kenyatta anataka kutuonyesha.
1. Uimara wa polisi ya Kenya ukilinganisha na polisi wetu.
2. Ulinzi wa viwanja vya ndege vya Kenya uko imara ukilinganisha na viwanja vyetu.
3. Usilipe ubaya kwa ubaya.
4. Jinsi Diplomasia inavyotakiwa iendeshwe.
5. Ujirani mwema ni vitendo siyo maneno.
6. Si kila tukio lazima Rais ahusike au lirushwe Live, balozi au DPP anaweza kushughulikia.
Tujifunze na tubadilike.
View attachment 1162058
View attachment 1162059