Watanzania wengi hawajui kwamba aliesimamia na kupanga mchakato wa ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2000 - 2025 ni Prof. Mark Mwandosya!

Watanzania wengi hawajui kwamba aliesimamia na kupanga mchakato wa ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2000 - 2025 ni Prof. Mark Mwandosya!

Mara nyingi nimesoma humu JF watu wakiubeza uwezo wa mtu makini sana hapa nchini, Prof. Mark Mwandosya, na wengi hawajui kwamba uandaaji na upangaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2000 - 2025 yeye ndie alipewa jukumu hilo na Raisi Benjamin Mkapa. Sisi tuliokuwa karibu na serikali tunalijua hilo.

Japo Mkapa alijua kwamba jukumu hili lilipaswa liende Tume ya Mipango, aliamua kwamba Prof. Mwandosya, ndie angesimamia uandaaji wake, akitumia utaalamu na ufahamu wake kwa kiasi kikubwa. Hivyo, mpangilio wote wa Dira ya 2000-2025, nini kiingizwe humo, maoni yakusanyweje, wataamu gani wawe consulted, ilikuwa ni Prof. Mwandosya.

Mkapa alimwamini sana na aliuelewa wazi uwezo wa huyu mtalaamu, na kama sio kuwa blackmailed na JMK kwamba asingepitishwa kuwa mteule wa ugombea uraisi angehamia Chadema na kushinda, Mkapa alitaka Prof. Mwandosya amrithi uraisi.

Huenda Tanzania ilifanya kosa sana kumkosa Prof. Mwandosya kama raisi wa nchi. Mtu ambae anaweza kukaa na kuandaa mchakato wa Dira ya Maendeleo kama ile ya 2000-2025, bila shaka angekuwa na mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya Tanzania, kama angefanikuwa kuwa raisi, iwapo JMK asingetoa majina toka mfukoni!

Katika maraisi wa Tanzania waliopita, ukimwondoa Nyerere, nani angeweza au anaweza kukaa na kutengeneza Dira ya niaka 25? Ukijiuliza hili swali utakuta tumeongozwa na tunaongozwa na maraisi wanasiasa na sio viongozi. Wamejaa porojo tu hawana lolote la kusaidia nchi kwenda mbele.

Ningewashauri waandishi wa habari mfanye mahojiano na Prof. Mwandosya kuhusu hitimisho la Dira ya Maendeleo ya 2000 - 2025 na kuanza kwa hii Dira mpya ya 2025 -2050.
Huyo mwandosya si amewahi kuwa waziri wa wizara nyingi nyingi nchi hii? Amefanya nini cha maana?
 
Nimeipitia hii
Mara nyingi nimesoma humu JF watu wakiubeza uwezo wa mtu makini sana hapa nchini, Prof. Mark Mwandosya, na wengi hawajui kwamba uandaaji na upangaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2000 - 2025 yeye ndie alipewa jukumu hilo na Raisi Benjamin Mkapa. Sisi tuliokuwa karibu na serikali tunalijua hilo.
Nimepitia hii dira inayokwisha, sijaona popote inaposema au kuonyesha kuwa iliandaliwa na Prof Mark Mwandosya

Tafadhali weka uthibitisho
 
Sanaa, gilba na magumashi yetu.... 😀 😀 😀 😀 😀

Tunakwama sana
Uchaguzi kila baada ya miaka 5, alafu tunatengeneza dira ya miaka 25.

Ndiyo maana mnaingia mkataba wa uendeshaji wa bandari kwa miaka 30 halafu hamfanyi juhudi zozote kuelimisha watu wenu wajao baada ya hiyo miaka kuisha wajiendeshe.

Kila anayekuja anatafuta muwekezaji wake anapiga zake anatulia.

Ticks walifukuzwa sasa tuna Dp world, sijui rais ajaye atamleta nani?
 
Uchaguzi kila baada ya miaka 5, alafu tunatengeneza dira ya miaka 25.

Ndiyo maana mnaingia mkataba wa uendeshaji wa bandari kwa miaka 30 halafu hamfanyi juhudi zozote kuelimisha watu wenu wajao baada ya hiyo miaka kuisha wajiendeshe.

Kila anayekuja anatafuta muwekezaji wake anapiga zake anatulia.

Ticks walifukuzwa sasa tuna Dp worls, sijui rais ajaye atamketa nani?

Halafu tukiwa tunafanya haya magumashi, tunajidanganya ndio watu wenye akili na nguvu kuliko wengine wote Tanzania.
Hakuna kitu kibaya kama kuidanganya nafsi yako mwenyewe.
Kweli mchimba kisima hutumbukia mwenyewe....tunajidangana sana
 
Nimeipitia hii

Nimepitia hii dira inayokwisha, sijaona popote inaposema au kuonyesha kuwa iliandaliwa na Prof Mark Mwandosya

Tafadhali weka uthibitisho
Kama ulitegemea kukuta jina lake humo basi wewe hufikirr mambo sawasawa. Nitakupa mfano mwingine. Kipindi cha Raisi Mwinyi, sera ya Nishati ilitengenezwa na Prof. Mwandosya, na zaidi yeye binafsi kwa kiasi kikubwa sana. Uliona jina lake kwenye national energy policy?
 
Waliogopa kumtaja? Kichaa kingine kimezidi. Km unampenda sn umpatie kazi yako
Ttizo mmezoea kuwataja watu na kusema mpeni maua yake hata wakitumia hela za kodi ya wananchi. Mwandosya alifanya haya bila cheo chochote serikalini, sasa angetajwa kama nani? Na pia Mwandosya alikuwa ana kawaida ya kufanya mambo kimya kimya, sio kutafuta kiki kama hao watu mnaowashabikia siku hizi
 
Kama ulitegemea kukuta jina lake humo basi wewe hufikirr mambo sawasawa. Nitakupa mfano mwingine. Kipindi cha Raisi Mwinyi, sera ya Nishati ilitengenezwa na Prof. Mwandosya, na zaidi yeye binafsi kwa kiasi kikubwa sana. Uliona jina lake kwenye national energy policy?
Hapo najuwa yeye alikuwa Commissioner of energy na later on Katibu Mkuu wa Energy. Siwezi kuanza kutafuta jina lake hapo kwa vile alikuwa mhusika kwenye wizara ya sekta husika
 
Hapo najuwa yeye alikuwa Commissioner of energy na later on Katibu Mkuu wa Energy. Siwezi kuanza kutafuta jina lake hapo kwa vile alikuwa mhusika kwenye wizara ya sekta husika
Sasa ni hivi, huyu bwana huwa hana tabia ya kutafuta kiki. Na wala haingekuwa sawa kuandika jina lake kwenye Dira ya 2025 wakati hakuwa waziri. Aliacha waziri anaehusika wakati huo a-shine. Kwanza hakuwa na cheo chochote serikalini, sasa wangeweka jina lake pale kama nani?

Unajua kuwa uwanja wa ndege wa Mbeya ni juhudi zake binafsi ulianzishwa bila hata bajeti rasmi ya serikali? Unajua kwamba jengo kubwa la Mafuta House pale Posta mpya lilianzishwa kwa juhudi zake binafsi bila hata bajeti ya serikali? Umeshasikia akitaka aandikwe mahali?

Ni baada ya ufanisi wake huu katika Dira 2025 na mchango wake kwenye Umoja wa Mataifa kuhusu mambo ya climate change ndio Mkapa alimwambia lazima akagombee ubunge ili awe sehemu ya baraza la mawaziri.
 
Au Synthesizer ndiye Prof Mwandosya mwenyewe? Itakuwaje ujuwe vitu vya mtu binafsi deep namna hiyo??

Anyway siyo lazima ujibu post hii, ila tuliosoma Cuba tumeelewa
 
Ila huyu Mwandosya ana akili sana nasikia kwenye mambo ya umeme ni bingwa.Nakumbuka Jakaya alipomteua kuwa waziri wa maji alisema dunia inamtumia Prof Mwandosya na sisi tumtumie.
 
UKitaka kujua hii nchi Ina vilaza ambao wanajiita viongozi

Tazama Mabadiliko ya mtaala wa Elimu.

Serikali itakapofika mwaka 2028 kutakuwa na Wanafuzi wa Form one batch mbili .

Yaani itakuwa hivi wanafunzi waliopo darasa la nne mwaka huu wataingia form one mwaka 2028 kwakuwa wataishia darasa la sita .

Na wanafunzi waliopo darasa la tano mwaka huu wataingia form one mwaka 2028.

Je Serikali imejipangaje kuhusu madarasa, kuhusu walimu, kuhusu facilities n.k

Kumbuka haya ndo mawazo ya wasomi wanaojiita viongozi.
Doktori nini shida,hivi karibuni naona una lugha kali sana kwa serikali au umechoka kukaa uraiani
 
Dira yenyewe iko wapi na nini kimefanyika kutoka kwenye hiyo Dira?

Kama maisha haya ndiyo Dira yake basi akae huko huko.

Kwani 2025 imeshafika, Kama tayari basi Dira yake haikufanya kazi.
Kwa hiyo kama dira haikufanya kazi ni kosa la Mwandosya?

Kwa uchambuzi wako huu ni sawa na kusema Quran haifanyi kazi maana Waislamu wanakula kitimoto!
 
Mimi ninazo dira za taifaikiwemo ya wakati wa utawala wa awamu ya kwanza ambayo ilipanga kufikia mwaka 2000 kusiwepo tatizo la maji lakini mpaka sasa tubasikia mara mama mtue ndoo.
Hayo mambo ya dira tuziachie nchi zilizoendelea maana hapa kila rais akiingia anaanza mwanzo na mpangaji mkuu ni Rostam Aziz
 
Back
Top Bottom