MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Jana tarehe 14/08/2023 kupitia ukurasa wa ITV nimesoma habari ya kukamatwa kwa wahamiaji haramu huko Katavi waliokuwa wakisafirishwa kupitia tenki la mafuta. Ni habari ya kutisha sana. Kilichonitisha zaidi ni baada ya kusoma comments.
Kiufupi ni kuwa watu wengi wamelaumu mtu aliyewapa taarifa polisi hadi kufanikisha kukamatwa kwa watu hao. Baadhi wamediriki kusema kuwa dereva hana kosa bali ilikuwa ni jitihada za kutafuta riziki.
Madhara ya human trafficking ni mengi ila kubwa zaidi ni vifo. Watu wengi sana wanapoteza maisha kwenye hili jambo. Mchakato wake sio wa kibinadamu kabisa hivyo naunga mkono jitihada zinazofanyika kuzuia.
Ninasihi mamlaka zinazohusika kuendelea kutoa elimu kuhusiana na hili kuanzia shule za msingi.