Watanzania wengi hawali chakula cha asubuhi (breakfast). Chanzo ni umasikini

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Huu ni utafiti wangu nimefanya kwenye miji mikubwa na hata vijijini kwenye kila mkoa hapa Tanzania

Ni Watanzania wachache sana ambao wanamudu kula milo 3 na hasa kipengele ni breakfast (mlo wa asubuhi)

Utakuta watu wanaenda mashambani, kazini na wanafunzi wanaenda shuleni hawajala chochote asubuhi. Kidogo baadhi ya maeneo wanakunywa uji wa chumvi.

Kutokana na ugumu wa maisha na vipato haba wengi hupiga pasi ndefu asubuhi angalau kuanzia mlo wa mchana na wa jioni ndio ambao kaya kadhaa zinakula.

Changamoto nyingine niliyoiona kwenye utafiti wangu nimegundua baadhi ya akina baba wa mjini ni watu wa ajabu sana.

Utakuta asubuhi yeye anakula kwa mama lishe supu au maharage na maandazi au chapati au mihogo akiwa kwenye mishe zake lakini nyumbani kwake watoto wanapiga pasi ndefu asubuhi.

Lakini pia nimegundua hata hao wachache wanaokula asubuhi wengi hawashibi ni kupasha tu matumbo.
 
Sahihi kabisa. Na hata wanaokula milo mitatu sio wote wanapika chakula fresh--wengi ni viporo.

Kwahiyo technically, kwa wastani watanzania wengi hupika mlo mmoja kwa siku.

Huu uzi wako ni research concept kabisa kwenye masuala ya Nutrition.
 
Sahihi kabisa. Na hata wanaokula milo mitatu sio wote wanapika chakula fresh--wengi ni viporo.

Kwahiyo technically, kwa wastani watanzania wengi hupika mlo mmoja kwa siku.

Huu uzi wako ni research concept kabisa kwenye masuala ya Nutrition.
Sahihi sana

Mfano mlo wa usiku hasa upande wa mboga huwa ni makombo ya mchana

Na asubuhi wachache hula viporo au makombo ya usiku

Technically Watanzania wengi wanamudu mlo mmoja kwa siku
 
Umesema vyema ukitembea hapa Tanzania ndio utagundua hilo tuna umasikini wa hali ya juu

Sio umasikini ule ni ufukara aisee ukiwa unapata mahitaji ya msingi mshukuru sana Mungu
Hata hivyo mkuu chai sio lazima, kukosa chai sio tatizo.

Maana ya breakfast ni breaking the fast yaani kuvunja mfungo, kwahiyo hata ukianza kula mchana umevunja mfungo tu.

Tunavyokosa huduma muhimu kama za afya ndo changamoto.
 
Mostly Africa mzima hawajui maana ya diet.
Umesema vyema

Wengi wanakula kama nguruwe, mfikirie yule baba mbinafsi anayekuka akiwa mishe pale kwa mama muuza

Kwenye meza asubuhi kaagiza chai, maharage (maharage kachanganya na sukari) na chapati pembeni ana soda kisha maji ya kiwandani

Jioni anapitia kwenye mchemsho wa kongoro na supu ya pweza na kabia kakuzugia

Imagine huo mchanganyiko huko tumboni mivitambi imeshamiri sana mjini kwa sababu elimu ya chakula hakuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…