Watanzania wengi hawali chakula cha asubuhi (breakfast). Chanzo ni umasikini

Watanzania wengi hawali chakula cha asubuhi (breakfast). Chanzo ni umasikini

Wakati wa utafiti wako bwana researcher wale jamaa tunaokunywa walau bia mbili asubuhi kama kifungua kinywa sisi ulituweka wapi ? Katika makundi yako ndugu ?
 
Milo mitatu wala siyo kanuni ya msingi ya lishe bora.
Hata katka maisha ya watanzania wengi lishe bora inapatikana,
Mihogo, ugali wa dona, viazi, uwele, mtama, ndizi za kupika,n.k,( wanga) mboga za majani kwa aina zake,( vitamini), jamii ya kunde kwa aina zake, dagaa, samaki, uyoga, karanga, nyama ( protini).

Vyakula hivyo vingine hata si ghali.

Asubuhi mtu anaweza kula boga, uji, viazi na karanga na akawa amekula mlo bora angalau kuliko chai ya rangi na mkate wa kukoboa au maandazi

Mchana ugali wa dona, dagaa na mchicha freshi tu.
Jioni ubwabwa maharage na ndizi za kuiva.
 
Familia nyingi hula milo miwili tu, asubuhi na jioni, mchana hupotezea wako bize au walipiga pasi ndefu asubuhi. All in all jioni ni lazima chakula kiliwe, potelea mbali asubuhi na mchana hakukuliwa chakula kutokana na hali ngumu ya maisha
 
Zaidi ya 50% ya watanzania kipato ni chini ya dollar moja kwa siku, utafiti wako inaonekana uko sawa na inawezekana hali ni mbaya zaidi
 
Huu ni utafiti wangu nimefanya kwenye miji mikubwa na hata vijijini kwenye kila mkoa hapa Tanzania

Ni Watanzania wachache sana ambao wanamudu kula milo 3 na hasa kipengele ni breakfast (mlo wa asubuhi)

Utakuta watu wanaenda mashambani, kazini na wanafunzi wanaenda shuleni hawajala chochote asubuhi. Kidogo baadhi ya maeneo wanakunywa uji wa chumvi.

Kutokana na ugumu wa maisha na vipato haba wengi hupiga pasi ndefu asubuhi angalau kuanzia mlo wa mchana na wa jioni ndio ambao kaya kadhaa zinakula.

Changamoto nyingine niliyoiona kwenye utafiti wangu nimegundua baadhi ya akina baba wa mjini ni watu wa ajabu sana.

Utakuta asubuhi yeye anakula kwa mama lishe supu au maharage na maandazi au chapati au mihogo akiwa kwenye mishe zake lakini nyumbani kwake watoto wanapiga pasi ndefu asubuhi.

Lakini pia nimegundua hata hao wachache wanaokula asubuhi wengi hawashibi ni kupasha tu matumbo.
Kwa hiyo lengo la utafiti wako uchwara ni nini?
 
Kuna Bibi mmoja alikua anapika chai sukari mtajijua kila mtu kivyake.
Wanapiga ndefu hadi sa moja usiku ndo unapikwa msosi.
Kulikuwa na mabinti kibao na watoto wao single maza,Haya mtoto ya kiume nayo mteja,vi baka,wapigwe debe ikizalisha huko inaleta wake zao na watoto mle ndani.
Ilikua vagalant nayumba km kituo cha kulea yatima.
 
Nchi ambayo 80% ya watu wake ni tegemezi, 20% ndio inazalisha unategemea nini hapo?
 
Back
Top Bottom