😀
Mkuu kama wanaotaka mabadiliko wangekuwa wengi kuliko waliotaka leo hii yangekuwa yameshatokea hayo mabadiliko.
Tatizo ni kuwa wanaotaka mabadiliko hawafiki hata robo
Mkuu, wengi wanaogopa kufa, kufungwa au kupata madhara yoyote toka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama. Kwenye siasa za TZ kuna makundi makuu matatu.
1. Watu wanayoipenda CCM (ndani ya hili kundi kuna makundi madogo mawili (i) Wanayoiopenda ccm ukweli ukweli (ii) wanayoipenda kulinda/kutafuta maslahi)
2. Watu wa upinzani (hawaitaki ccm)
3. Watu waliopo katikati/vuguvugu/neutral
(Hili ndio kundi kubwa lililopo kwa sasa)
Ndani yake kuna makundi madogomadogo mengi mno
(i) ambao hawaitaki ccm (upinzani)ila wanaogopa kujulikana. Wanaogopa madhara ya hatari ambayo wanaweza kukutana nayo (waoga) ila wanajua hali halisi na wizi wa kura na matatizo yote
(ii) ambao wao hawaelewi chochote kuhusu kinachoendelea wao wako bize na mishe zao za kutafuta hela, wako bize na simba na yanga, wako bize na bongofleva na masupastaa wa mitandaoni, wengine wako bize na amapiano na misambwanda. Yaani wao hakuna wanachoelewa.
Sasa hayo makundi makuu matatu ndio yapo kwa sasa. Ila kundi la vuguvugu ndio wako wengi ila wanaogopa madhara ya hatari ambayo wanaweza kukutana nayo wakiwa upande wa upinzani.
Hofu ya vyombo vya ulinzi na usalama ndio inawapa watu hofu.