Siyo siri kuwa watanzania wengi wangependa kuona mabadiliko ya ungozi kwenye ngazi zote. Shamra shamra tulizokuwa tunazishiudia miaka hiyo kwa sasa hakuna. CCM inaonekana kuishiwa pumzi, ila wanaoikimbiza nao ni viwete.
Uchaguzi wa mwaka 2015 ulikiacha kilichokuwa chama kikuu cha upinzani katika hali mbaya ya kukosa kuaminiwa na wananchi baada ya kumpa Edward Lowasa apeperushe bendera yao. Wengi walivunjika mioyo yao. Imani ya wananchi kwa chadema haipo tokea wakati ule.
CCM 5 tena. Siyo kwa sababu wengi wanaipenda, ila hakuna mbadala.