Bill Lugano
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 1,210
- 6,774
Heri ya Mwaka Mpya. Nilikuwa nje kidogo na JF nikijikita katika shughuli zangu za uchumi hasa nje ya nchi katika kipindi hiki cha Corona. Kumekuwa na usumbufu kidogo hasa sisi tunaosafiri sana nje ya nchi.
Nimerudi TZ. Nikiwa ofisini leo kaja bwana mdogo mmoja ananambia amenunua gari jipya angependa nikaione. Niliona amefanya jambo zuri maana hapo mwanzo alikuwa anaendesha Subaru.
Kweli nimeenda kuangalia parking nikakuta ana gari kweli. BMW. Nilimpongeza sana. Sasa kwenye suala la upya ndo nikashangaa lile gari kumbe limetumika Japan. SI JIPYA. Mtu anashindwa toka usd 80,000+ kupata gari jipya? Huu ni ubahili au umaskini mkubwa.
Tena limetembea kms zaidi ya 20,000 jambo ambalo limenishangaza. Gari la mwaka 2014 yeye anasema jipya. Kwa mwaka na kms ni gari la zamani sana tu.
Ndio mtu mmoja akaniambia kwa Watanzania gari likitoka limetumika Japan wao wanaita jipya. Nilishangaa sana. Hivi kwanini watu wanapenda vitu used au vya muda mrefu? Teknolojia ya mwaka 2014 kweli uje ulinganishe na ya 2019, 2020 na 2021?
Unajisikia raha gani unapoendesha gari limetumika huko nje? Unakuta mtu ana mke second hand, girl friend second hand, nguo second hand, viatu n.k 2nd hand. Sasa huyu ana enjoy nini? Au anakuwa na vitu outdated bado anaenda nunua vitu ambavyo soko limevikataa.
Mimi nafikiri tuanze kuwaza kitajiri. Kataa mitumba, used stuff. Tumia kitu kipya ujisikie raha yake. Mimi huwa kwa kweli nashindwa kutumia kitu ambacho sikuanza nacho mimi. Nina kinyaa sana. Unatumia gari limeendeshwa na Wajapan huko wamechoka wanaamua kukuuzia wewe nawe unaona it's something?
Pia tuanze nunua magari brands za ukweli. Toyota VX nimeambiwa nazo si haba ila upate Lexus. Unaweza ukanunua hilo. Na kule Japan ukinunua jipya wanakupa na Rav 4 moja au Vitz mbili kama nyongeza.
Tusiishi na kuzoea umaskini. Tunapaswa kubadilika. Nchi yetu imekuwa kama jalala la magari na vyombo vya usafiri outdated. Hii si sawa hata kidogo. Tubadilike.