BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Ukiwa na madhila utapata watu wengi sana wa kukushauri na kukupa nasaha.
Wengine watajifanya motivational speakers huku wakikupa usia wa mambo kadhaa ya kubumba.
Baadhi watajitutumua na kujifaragua kwamba wanakujali sana, ati wako tayari hata kufunga novena.
Lakini ukiwaambia nina milioni kadhaa nataka nifanye biashara wanavimbisha mishavu na kununa.
Au ukiwapa taarifa kwamba familia yako ina furaha na mnaishi kwa amani na upendo watajifanya kucheka usoni lakini wakitoka hapo wanatimua mbio wanaenda kufungua mikoba yao ya kichawi kukusambaratisha.
Kuna mmoja nilimfuma ananinafikia nikamzaba makofi matatu akabaki kujiliza na kuomba msamaha kwa wingi.
Watu wengi wanapenda kukuona ukifeli na kushindwa. Hata ndugu zako pia.
Wakijifanya kukutabasamia kaza uso. Wanaigiza.
MY TAKE: Tuishi kwa machale.